Mnaonaje kama watumishi wa serikali na taasisi kubwa binafsi wakianza kulipwa mishahara yao kila baada ya wiki mbili na sio wiki nne (mwezi mmoja)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Mnaonaje kama watumishi wote wa serikali pamoja na wale wa taasisi kubwa binafsi wakianza kulipwa mishahara yao kila baada ya wiki mbili na sio wiki nne (mwezi mmoja) kama ilivyozoeleka sasa?

Kwanini serikali pamoja na taasisi kubwa binafsi hulipa mishahara ya watumishi wao kila baada ya wiki nne (mwezi mmoja) na sio wiki mbili au wiki nane (miezi miwili)?

Huu utaratibu wa mishahara kila mwezi umetokea wapi? What's the logic behind all this?

Leo kuna mtoto wa shangazi yangu ameenda kuanza kazi katika Bank moja kule Mbeya baada ya kufaulu vema usaili wake, na swali la kwanza kuulizwa na wazazi wake pamoja na watu wa karibu ni kwamba, "wanakulipa mshahara kiasi gani kwa mwezi?"

Kwanini mshahara ni wa mwezi (wiki 4) na sio wiki 2 au wiki nane (miezi 2)?

Yaaani kama mtu kwa mwezi take-home salary yake ni 700,000/= basi apewe 350,000/= tarehe 14 kisha nusu iliyobaki tarehe 28 kwa maana kuna miezi haina tarehe 29, 30 na 31.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Wiki mbili Ni ngumu aisee. Serikali ina idara nyingi Sana ku organise makusanyo, pamoja na pay list ni ngumu. Imagine paylist inatumwa tarehe 15 labda na salary inatoka after one week. It means one week inakuw ni ya maandalizi na michakato ya kuwalipa watumishi.

Itawezekana, Kama mifumo ya teknolojia na sayansi itakuwa yakisasa,pamoja na kuwa na makusanyo makubwa ya fedha, pamoja na akiba kubwa hazina.
 
Hela wanazitoa wapi angalau mwisho wa mwezi kuna vipato vinapatikana kama sehemu ya faida au gawio
Mkuu, kwani hivyo vipato kama sehemu ya faida na gawio haviwezi kupatikana ndani ya wiki 2 au wiki 8? Nini mantiki ya kuwa na mishahara kila baada ya wiki 4?
 
Mkuu, kwani hivyo vipato kama sehemu ya faida na gawio haviwezi kupatikana ndani ya wiki 2 au wiki 8? Nini mantiki ya kuwa na mishahara kila baada ya wiki 4?
Haina uhakika kwa ndani ya week2, usiseme kama huna uzoefu ni heri uulize, malipo ya masaa na weekly ni football clubs ndiyo ziliweza tena vilabu vya nje ya nchi kwa kuwa mzunguko wa pesa ni mkubwa, hoja ya msingi ni mzunguko wa pesa, hebu nikuulize swali wewe ni mwajiriwa au mwajiri
 
Mshahara hata wakilipa kila wiki malipo unayolipwa kila mwezi hesabu yake ni ile ile. Kikubwa wametusaidia ambao hatuwezi kujibana tukadunduliza hadi mwisho wa mwezi.

Anyway Hesabu wengi tulipata F
 
Haina uhakika kwa ndani ya week2, usiseme kama huna uzoefu ni heri uulize
Ndio maana nimeuliza kwa maana mimi sina uzoefu na hayo mambo. Kwanini mfumo wa malipo hapa Tanzania umekaa wiki 4 na sio wiki 2 au wiki 8? Logic ni nini? Ni nani alikuja na huu mfumo wa wiki 4?
 
Nafkiri huu ni utaratibu wa kibajeti ambao umewekwa sambamba na taritibu nyingine za ukusanyaji kodi na mapato ya serikali!
Mimi binafsi naishauri serikali hao wafanya kazi nao wawe wanalipwa mafao ya kiinua mgongo kila baada ya miaka 5 kama ilivyo kwa wabunge, Kisha wanaendelea na mikataba yao kama kawaida!

Hali hii ingesaidia watumishi wengi kujenga nyumba zao wenyewe mapema na kufaidi kuishi katika nyumba bora mtumishi akiwa bado katika utumishi, Tofauti na sasa ambapo wengi hujenga au kununua nyumba za maana baada ya kustaafu kazi!
 
Ndio maana nimeuliza kwa maana mimi sina uzoefu na hayo mambo. Kwanini mfumo wa malipo hapa Tanzania umekaa wiki 4 na sio wiki 2 au wiki 8? Logic ni nini? Ni nani alikuja na huu mfumo wa wiki 4?
We jamaa banah, kwa kifupi ni sawa na kuuliza tu kwanini umezaliwa ukakuta watu wanavaa nguo na sio majini au ngozi ilihali zamani watu walivaa majani, je tunavaa nguo ili iweje.
 
kwa kifupi ni sawa na kuuliza tu kwanini umezaliwa ukakuta watu wanavaa nguo na sio majini au ngozi ilihali zamani watu walivaa majani, je tunavaa nguo ili iweje..
Hili pia ni swali zuri sana na lina mantiki kubwa ndani yake sema sio la kujadili katika mada hii.
 
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
We jamaa banah
emoji1787.png
emoji1787.png
Hahahahaaaaa, wewe endelea tu kunishangaa na mimi nipo hapa ninatafuta mantiki/logic ya suala hili mkuu.
 
Back
Top Bottom