Mnaonaje Baraza hili jipya la Mawaziri linalotarajiwa?

Kikwete awe jasiri amuombe Lipumba awe waziri wake wa fedha kwa kipindi chake kilichobaki!! Lipumba ni mzalendo anaweza kukubali kubeba huo msalaba!!
 
Yani ni sawa na kufuta SIFURI na kundika "O"

kwani mara ngapi kawabadili?
Watendaji na wenye maadili walishaisha siku nyingi CCM.










Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?
 
Back
Top Bottom