Mnaonaje Baraza hili jipya la Mawaziri linalotarajiwa?

Hiyo na. 10 nitamshangaa sana kama Pinda hajaomba kupumzika! Kufanywa kote kama mtoto then bado awe na hamu na uwaziri wa jk-ni utaahira!

Si vizuri kususa kulitumikia taifa lako mm sikubaliani nawe Mh Pinda kupumzika,Mm nashauri Mh Pinda aendelee kutumikia taifa letu kwa cheo chake hicho hicho cha uwaziri mkuu anao uwezo mzuri wa kufanya kazi na ni muadilifu mkubwa!
 
Wakuu wana JF,naomba tumsaidie Rais Juu ya nani abaki na nani aondolewe na nani abadishiwe wiraza kwenye baraza jipya linalotarajiwa soon:

mawazo yangu:
1.Ngeleja na Malima OUT,wametusababishia madeni makubwa yakiwemo DOWANS
2.Nundu na Naibu wake wabadilishiwe wizara,cant work together kila sikumigogoro
3.Ciril na Nyalandu watenganishwe,na kama nafasi mpya ni chache Nyalandu OUT
4. waziri wa afya abadilishiwe wizara,ya afya imemshinda ila kwa kuwa bado ni kijana mdogo with limited experience apelekwe wizara ndogo ndogo kama ile ya Simba.
5.Sophia Simba OUT-> none existent
6. Mwakyembe na Magufuli should be separated,kila mmoja awe waziri kamili.
7. Kabaka OUT none existent
8. Magembe abaki na wizara yake
9. Mali asili na Utalii OUT
10.Pinda abakie waziri mkuu. SIO FISADI.
11.MKULO OUT ameshindwa kuthibiti matumizi ya dollar nchini.
12.

endeleeni wadau

Mkuu naona umefanya home work nzuri sana labda niongezee YAFUATAYO:


  • Mh. Nundu abaki wizara ya Uchukuzi (kwa kuwa ni muhandisi ataiweza sana) naibu wake ahamishiwe wizara nyingine.


  • Prof. Maghembe abaki kilimo kwa kuwa yeye ni mtalaamu wa KILIMO na mwadilifu, wizara ibadilishe watendaji wakuu, bila kufanya hivyo kilimo kitabaki nyuma, hawa watu hawako committed na kilimo hata kidogo; na ndio wanamuwekea spana Prof.Maghembe, namshauri awe mkali kidogo asikae kipadri padri (Sheikh). Vile vile atupie macho Crop Boards afanye mabadiriko makubwa katika uongozi wake, na Board members wa Crop boards wawe wanakuwa interviewed na kuwa vetted, asikubali kupewa ushauri na viongozi waliokutangulia uwezi kujua wana agenda gani za siri we chapa kazi na umshirikishe Mungu vile vile wewe kama mtalaamu wa kilimo asikubali kabisa Wakurugenzi wakuu wa Broads hizi kuongozwa na watu ambao hawakusomea kilimo, mbona nchi hii ina wataalamu wengi wa kilimo, kuna mantiki gani ya kuwateua wakurugenzi wakuu mbumbumbu wa kilimo kama vile wana siasa na wanasheria, mtu utategemea nini katika hilo - ni vurugu tupu tu kazi kugombania vyeo na hujuma, mfano tunayo ajaribu kuangalia Crop Boards zilizo wahi kuongozwa na wataalamu wa kilimo kama walihai kupata matatizo, hakuna; wavamizi wa fani hii ndiyo wenye matatizo wako pale kujinufaisha tu na kuwahujumu watalaamu wa kilimo katika Mashirika yao - wanatafuta kila mbinu kuwaondoa kazini kwa hila wataalamu wa kilimo ambao wanawaona ni tishio kwao.


  • Mugufuli na Mwakyembe - mimi naona Magufuli abaki katika wizara yake, Mh. Mwakyembe ahamishiwe wizara ya Utalii na mali Asili, msomi huyu ambaye ni mzaledo kweli kweli ndiye mwenye uwezo wa kubadirisha wizara hii kotoka kwenye ufisadi uliyo kubuhu kwenda kwenye neema, hivi kuna sababu yoyote ambayo inaifanya Kenya itupiku kwenye mambo ya Utalii wakati wao wana vivutio vichache tu lakini Taifa lao linanufaika sana, kwetu je?


  • Maziri Mkuu abaki yule yule mwana wa MKULIMA, amevumilia mambo/vituko vingi sana.

Majina yaliyo baki na mapendekezo yako yote ni SPOT ON.
 
Mkuu hapa hakuna wa kubaki wote wameoza tunataka sura mpya kabisa na wachache wazuri
Mimi nashauri JK, amteue ubunge Kinana, na awe PM,he is a decesive man mwenye uamuzi, alivyo iendesha wizara ya ulinzi ni reference ya kutosha, na anauwezo mkubwa.
 
kama kweli siye wa mbozi tumemkosa mtetezi wa pembejeo hususan mboleaaaa tutegemee viroba vya chumvi badala ya mbolea rip pembejeo @ zambi
 
none of the above kwa kweli
wote wameharibika na damu ya magamba
apunguze baraza wabaki 20 tu
kama ni utendaji wapo makatibu wakuu wanatosha.
 
Pinda OUT for good, he is too good for nothing; Sitta au Magufuli mmoja wao awe Waziri Mkuu, Madini, Kabaka Elimu.

Wasira OUT; Lukuvi OUT, Ngeleja OUT, Nundu OUT, Magembe OUT, Kawambwa OUT, Maige OUT
 
naitafuta hiyo email ya dada yake january makamba kwenada kwa basha wake wa barick mwenye nayo naomba apost nami niweze kujiridhisah yasemwayo!
 
Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

Tzeba ni mwizi aiye hata na aibu, alipokuwa mwajiliwa wa halmashauri ya jiji la DSM, alikuwa anatoa vibali kwa rushwa hata kwenye maeneo yasiyotakiwa, hali iliyomfanya mkurugenzi wa jiji kumtimua hapo, na ndipo akapelekwa Mwanza. akiwa Mwanza akarudia yale yale, kwa kutoa kibali katika kiwanja ambacho hakikutakiwa kwa hongo kwa mfanyabiashara mmoja, kitu ambacho kilifanya akosane na Mh Magufuli, na kuliingizia taifa hasara kubwa.

Amewahi kushiriki katika malipo hela hewa katika idara ya maji akishirikiana na aliyekuwa mhasibu wa maji hapo Mwanza Bw Mbatta.

Akiwa mbunge na mkuu wa wilaya Sikonge, alikuwa akitoa hata kuonyesha mawasiliano na mkuu wa kaya kwa watu na hata malaya.

Haya tunayoyaona leo ya akina Maige, Ngeleja, huyu jamaa akiingia mtaomba anyongwe ni mwizi wa asili, na mla rushwa mkubwa saana.
 
Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

Tanzania, as a nation, seems to be non-existent; it is just a chunk of land where averyone can do anythying.
 
Kama hakuna mabadiliko ya kitaasisi hata baraza la mawaziri la malaika likishushwa litashindwa.
 
Sita angepewa tamisemi akapambane na wakurugenzi wilayani huko maaana ndiko ubadhirifu umekithiri.
Magufuli apewa nishati na madini
 
Wapendwa wadau,
Kipindi akiwa spika wa bunge na hata siku za mwanzo wa uwaziri wake Sitta alionekana mpinga ufisadi na mtetezi wa wanyonge.
Wadau mtakumbuka mwaka jana Sita alipewa nafasi ya kukaimu uwazili mkuu. Na hapa ndo kajionesha yeye ni nani. Akikaimu uwazili mkuu alitetea nyongeza za posho za wabunge kwa nguvu zote. Alifanya hivi akijua taifa lilikuwa ktk hali mbaya sana, mfumuko wa bei ulikuwa juu mno na watu walikuwa wanaishi kwa mlo mmoja. Moja ya hoja zake ilikuwa ni kupanda kwa gharama za maisha, Je, alikuwa amefanya nini kuwasaidia watanzania walio wengi, zaidi ya kuwaacha interns bila chochote wafe kwa njaa.

Huu ni unafiki na uzandiki mkubwa wa sita. Kumbe kelele za awali zililenga kumpa umaharufu wa kisiasa na akishapanda awageuke walomwamini!

Sita hafai ktk Baraza jipya.
 
Back
Top Bottom