Mnaomiliki na kutumia Volkswagen 'chuma ya mjerumani' ni gereji zipi mnafanyia service & repair? Popote pale nchini

Kwa kuzingatia viwango vya safety, stability, comfortability, inaonekana wazi kabisa kuwa watu wengi wanatamani sana kumiliki magari ya Ulaya. Lakini wanaogopa kuyamiliki kwasababu kuu tatu:

  • Uhaba wa mafundi/garage for European cars.
  • Uhaba wa spea (kupata spea ni shida, sometimes inakulazimu kuagiza spea nje ya nchi!!).
  • Spea ni aghali sana (expensiveness).

Ukiomba ushauri kwa mtu yeyote wa magari au fundi, kuhusu kumiliki magari ya Ulaya, utapewa jibu moja tu common: "Hizo gari ni pasua kichwa, achana nazo kama una hela ya mawazo".

Kuna kauli mbiyu hii maarufu sana kwamba "ukitaka speed, stability, na nguvu, nenda kwa Mjerumani" yes, chuma ya mjerumani! Na hii ni kweli tupu. Jaribu kulinganisha kati ya baby-walkers za mjapan na baby-walkers za mjerumani in terms of speed & stability... utofauti ni mkubwa mno between the two! Mfano tu VW polo/golf Vs Toyota IST/Passo/Starlet... ni mbingu na ardhi, in terms of speed & stability.

Hivyo basi, kwa wadau ambao tayari wanamiliki na kutumia mikoko ya mjerumani hapa Bongo, specifically 'VOLKSWAGEN', huwa mnaenda garage zipi for service na matengenezo?

Uzi huu uwe ni msaada kwa wale wote wanaotarajia kumiliki gari za mjerumani 'Volkswagen' ila wapo puzzled kuhusu upatikanaji wa mafundi/gereji na spea.

Kwa kila jiji, tutaje fundi au gereji inayoaminika for Germany cars' services & repairs.

Tuanze na miji mikubwa yote Tanzania...

*DAR- gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*MOSHI - gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*ARUSHA - gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*MWANZA - gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*DODOMA
*MOROGORO
*KAHAMA
*TANGA
*BUKOBA
n.k

Karibuni wamiliki wa Volkswagen mtupe ramani za machimbo ya services & spare parts for the mentioned vehicle. Feel free to share your real experience kuhusu hii chuma ya mjerumani regarding 'where to go service'.


N.B: Please mods msiunganishe hii thread. Lengo la uzi huu is to possibly single out the best garages and/or motorheads for Germany cars' maintenance & repair around Tanzania, of which are very scarce in the country.
Well, mkombozi amepatikana.
1) Hizi chuma za mjerumani sio kwamba zote ni perfect. Kuna generations korofi pia za ku avoid. The same kwa Toyota, honda n.k
2) Mafundi wengi bongo wababaishaji na watakuharibia chimbo chako usipokuwa makini.
3) Namna gani utaishi nayo ni suala lingine pia. Wengi hatujui

East_cars wamekuja na suluhisho. Hawa jamaa wanazunguka Tanzania nzima kufanya background check na partnership na garage zinazojielewa. Wana group lao telegram, members wanapata access na reviews za magari, recommended garages kwa mkoa uliopo, kujua generations zipi nzuri, namna ya kuishi nazo, experiences za members, ushauri n.k
Whether una gari, una plan ya kununua, una hobby na magari, hautojutia kujiunga na hii familia.
Instagram: @east_cars
YouTube: https://youtube.com/channel/UCRTVoQHdZzmWc7-cQxxAFHw
 
Watu weshafunga ndoa na gari za Japan. Mjapan katushika kwakweli.

Afu ukitembelea nchi za jirani, gari za Ulaya ni nyingi sana mkuu. Nishawahi fika Lusaka Zambia, kule Toyota ni za kutafuta road. Nilikuwa naona brands za Ulaya tu BMW, Range, VW, kwa kiasi kikubwa.

Ila bongo, Toyota ni mafuriko road.
... kuna vitu kadhaa vinavyochangia watu "kufunga ndoa" na gari za mjapan; mosi, upatikanaji wake ni rahisi, pili, bei sio mbaya, tatu, hayo mawili ya kwanza yamepelekea spea kupatikana kwa urahis na be nafuu pia;

nne (muhim sana hii), upande wa uendesjaji wa Japan ni sawa na ilivyo kwa Tanzania, wanaendeshea kushoto kwa barabara hivyo usukani uko kulia. That means, ukiagiza gari iliyotumika Japan ni mkataba utapata RHD. Hili ni tatizo kwa gari zilizotumika Ulaya (except UK) nyingi ni LHD ambapo huzifanya zisiwe convenient sana kwa mazingira ya Tz.
 
Pasipo kuelezana wapi pa kupata spea na mafundi wazuri, hizi gari za mjerumani tutaendelea kuziogopa sana hapa bongo!
Chuma za Mjerumani siku hz Nyanya Sana. Yupo Mjerumani Mweusi hapo Sauzi anafyatua tu kama mwehu. Mercedes haielewek
 
Sema gari yangu ilienda kwenye mambo ya kampeni.

Ikarudi imeharibika vitu vingi sana hasa vya chini. Ilibidi nibadilishe vyote. Ila service za kawaida bei ni reasonable na spares bei ni kama mara 2 ya Toyota Used kwasababu hata bei ya genuine parts za Toyota zinashindana na hizo za Europe.

Pia yeye anadeal na gari almost zote za European. Ukitaka na spares anakuagizia yeye mwenyewe.
Ni kweli, vitu Genuine ukienda kwa dealer wa Toyota ni bei ghali sana! Mfano shockup za miguu ya mbele za Allex niliambiwa 1.3M kwa pea, wakati huku mtaani ni laki na ishirini kwa zote mbili za mbele. So spea zisizo genuine kwa Toyota ni nyingi sana ndio zinaturahisishia maisha
 
Ni kweli, vitu Genuine ukienda kwa dealer wa Toyota ni bei ghali sana! Mfano shockup za miguu ya mbele za Allex niliambiwa 1.3M kwa pea, wakati huku mtaani ni laki na ishirini kwa zote mbili za mbele. So spea zisizo genuine kwa Toyota ni nyingi sana ndio zinaturahisishia maisha
Mkuu hizo shock up ni complete ama? Ni units tu? bila coil spring na kile kikofia chake? Ni KYB? Auto express wanauza 245,000-235,000 kwa unit moja inategemea na gari lako zipo hadi za 135,000 unit (bila coil spring)
 
Back
Top Bottom