Mnaomiliki na kutumia Volkswagen 'chuma ya mjerumani' ni gereji zipi mnafanyia service & repair? Popote pale nchini

kayanda01

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
1,086
913
Kwa kuzingatia viwango vya safety, stability, comfortability, inaonekana wazi kabisa kuwa watu wengi wanatamani sana kumiliki magari ya Ulaya. Lakini wanaogopa kuyamiliki kwasababu kuu tatu:

- Uhaba wa mafundi/garage for European cars.
- Uhaba wa spea (kupata spea ni shida, sometimes inakulazimu kuagiza spea nje ya nchi!!).
- Spea ni aghali sana (expensiveness).

Ukiomba ushauri kwa mtu yeyote wa magari au fundi, kuhusu kumiliki magari ya Ulaya, utapewa jibu moja tu common: "Hizo gari ni pasua kichwa, achana nazo kama una hela ya mawazo".

Kuna kauli mbiyu hii maarufu sana kwamba "ukitaka speed, stability, na nguvu, nenda kwa Mjerumani" yes, chuma ya mjerumani! Na hii ni kweli tupu. Jaribu kulinganisha kati ya baby-walkers za mjapan na baby-walkers za mjerumani in terms of speed & stability... utofauti ni mkubwa mno between the two! Mfano tu VW polo/golf Vs Toyota IST/Passo/Starlet... ni mbingu na ardhi, in terms of speed & stability.

Hivyo basi, kwa wadau ambao tayari wanamiliki na kutumia mikoko ya mjerumani hapa Bongo, specifically 'VOLKSWAGEN', huwa mnaenda garage zipi for service na matengenezo?

Uzi huu uwe ni msaada kwa wale wote wanaotarajia kumiliki gari za mjerumani 'Volkswagen' ila wapo puzzled kuhusu upatikanaji wa mafundi/gereji na spea.

Kwa kila jiji, tutaje fundi au gereji inayoaminika for Germany cars' services & repairs.

Tuanze na miji mikubwa yote Tanzania...

*DAR- gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*MOSHI - gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*ARUSHA - gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*MWANZA - gereji zipi au fundi gani mzuri for Volkswagen?

*DODOMA
*MOROGORO
*KAHAMA
*TANGA
*BUKOBA
n.k

Karibuni wamiliki wa Volkswagen mtupe ramani za machimbo ya services & spare parts for the mentioned vehicle. Feel free to share your real experience kuhusu hii chuma ya mjerumani regarding 'where to go service'.


N.B: Please mods msiunganishe hii thread. Lengo la uzi huu is to possibly single out the best garages and/or motorheads for Germany cars' maintenance & repair around Tanzania, of which are very scarce in the country.
 
Huu Uzi unatunyima UHURU wa kuchangia.
Kwasabb ya kulogwa na Toyota watu wengi tunayaona Tu barabaran haya Magari ya mjerumani

Watu weshafunga ndoa na gari za Japan. Mjapan katushika kwakweli.

Afu ukitembelea nchi za jirani, gari za Ulaya ni nyingi sana mkuu. Nishawahi fika Lusaka Zambia, kule Toyota ni za kutafuta road. Nilikuwa naona brands za Ulaya tu BMW, Range, VW, kwa kiasi kikubwa.

Ila bongo, Toyota ni mafuriko road.
 
Back
Top Bottom