ostrichegg
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 12,062
- 6,197
Picha unayotoa ni kuwa wewe ni wale wa kuhadithiwa kila kitu kwenye kijiwe tu na kushangilia. Ungependa pia kila mtu awe afurahie hali hiyo kama wewe na wenzio wa lumumba.Wanabodi JF!
Naomba niseme wazi hapa, bila kupoteza muda wenu mwingi.
Mojawapo ya mambo yanayotamkwa sana humu JF, ni pamoja na urushaji wa vikao vya bunge live.
Wanaotaka hivyo wanadai kwamba kutoonyeshwa live ni ukiukwaji na uminyaji wa demokrasia.
Sasa mimi nimejaribu kutafuta nchi mbalimbali hususan za jumuia ya madola,sikuona hata moja ambayo inaonyesha live vikao vyake vya bunge, tofauti na utaratibu unaotumika hapa kwetu kwa sasa.
Ila kama nyinyi mmeziona ebu tuziweke humu ndani ili tuondowe ubishi!
Karibuni....
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaogopa kuuliza, kutafakari lolote, wapo wanaotafakari kwa niaba yako. Na nyie NDIO mliyojaa hapa tz na mwaitwa wazalendo. Poleni.
Sent using Jamii Forums mobile app