• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mnaokwenda kuoa mkoa wa Tanga tafakarini mara mbili

Ligaba

Ligaba

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Messages
385
Points
1,000
Ligaba

Ligaba

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2018
385 1,000
Ujumbe wangu huu hauwahusu wanaume wa Tanga wanaoa mabinti wa kitanga naamini wao wanaendana kitabia hivyo sio issue kubwa sana kuishi katika ndoa.

Tuje kwetu sisi ambao si wenyeji wa Tanga na tungependa kuolea huko, hapa nakushauri jifikirie kabla hujaamua. Jifikirie Mara mbili kwa sababu kuna vitu ambavyo wewe kama si mwenyeji vitakutesa sana na utajikuta upo kinyume na dhumuni lako.

Kwa kipindi ambacho nimeishi na kuona utamaduni wa watu wa Tanga nimegundua kwamba wanawake wa Tanga wanapenda sana ushirikina wa ndoa huu mnaoita limbwata. Amini usiamini ukioa Tanga mwanamke hata awe PhD bado anathamini waganga kuliko Mungu. Yaani usiombe uwe tajiri kisha oa mwanamke wa Tanga utajuta. Achana na hii slogan mapenzi yameanzia Tanga hakuna lolote si Mzigua, si mdigo, si Msambaa wala msegeju hao wote ni wamoja. Najua kuna wengine mtabisha ila ubishi wawezekana kwa sababu si mzoefu. Uliza Wagogo, Wanyamwezi na Waha waliokwenda kutafuta maisha kama wamewahi kukumbuka walipotoka.

Kingine ni kwamba jamii za watu wa Tanga wanapenda kuishi kijamaa kupitiliza. Wanapenda kila tukio hata kama ni dogo vipi basi ukoo wote popote mlipo muje mshiriki asikose hata mmoja. Fikiria kuna kaharusi tu haka kakuweka ubani tu ndoa tayari bhasi hata ukiwa Kigoma wadigo watakuta uje Tanga kwenye hako kaharusi na usipokuja wamefura. Hebu fikiria maisha haya kila Siku uwe kiguu na barabara utaweza?

Katika ujamaa huohuo usishangae nyumbani kwako kukuta una watu hata kumi wamejaa kwako na hawana hata tarehe ya kutoka na wengine wanaweza hata kuoa wakataka na wake zao walete hapohapo kwako na wao hawaoni kama ni tatizo. Ushawahi kusikia msemo wa "Mdigo Mzigo?" Ukiona umeoa Tanga na nyumbani kwako hawaji kwa wingi ujue labda wamekudharau masikini au una roho ngumu zaidi ya Jiwe.

Hizi ni chache ila yakupasa utafakari sana unapofikiria kuoa binti wa Tanga asilia. Kama una roho mbaya usithubutu. Kama sio mtu wa kupenda masafari acha kabisa, kama unaogopa ushirikina ndugu epuka mapema kifuatacho ndugu zako watakusikitikia tu na wasijue la kufanya.

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
Mimi nina mtanzano wangu ni tofauti,
Nimeoa Tanga lakini mke tulikutana mkoa mwingine na makuzi ya Binti hayakuwa ya Tanga huenda hilo limesaidia. Kimsingi kwangu hakuna ndugu zake hata wakija ni mara moja wanarudi walikotoka in few days!

Kuhusu Ushirikina sina pia exprience coz sijawahi ona hayo lakini ninachojua Familia ile ni ya wacha Mungu, wana kaka ambaye ni mchungaji na wazazi wanaabudi kwa mtumishi mmoja wa Mungu maarufu na mwenye hofu ya Mungu kwelikweli!!

Tumejenga, tuna kajiusafiri watoto wanasoma shule nzur nk.

Sifa kubwa ni ujuzi wa kupika aisee hapo ndio nawavulia kofia!
===
adolay,
Mkuu,
uko sahihi sana. Mazingira ya maisha unayatengeneza mwenyewe. Sherehe, shughuli unaweza ukaziondoa ki sakolojia.
Nimeona wanawake wa Tanga they are the Best ukimtimizia mahitaji yake. Mchele wa kunukia liwepo gunia, Nazi isikosekane, hiliki, mdalasini na vinginevyo viungo.

Kwa week kama no mdogo asikose samaki Mara mbili. Ukimtimizia hivyo hawana gharama kubwa kama wachagga.
Kasoro iko kwa msambaa ni sex maniac unatakiwa uwe vizuri vinginevyo hizo ni community city centre.
PIA SOMA
- Historia ya mkoa wa Tanga
 
Ligaba

Ligaba

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Messages
385
Points
1,000
Ligaba

Ligaba

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2018
385 1,000
Kwenye 6 kwa 6 nasikia wapo vizuri sana na mimi ndio ugonjwa wangu mabinti wa kitanga wapo vizuri hayo mengine si kitu nita vumilia mapenzi si mavuz kwamba kila mtu mzima anayo
Hamna hamna tofauti na wengine, sema tu labda wao wanajali mapenzi kuliko kitu chochote,
 
A

adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
10,991
Points
2,000
A

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
10,991 2,000
Kila makabila, maeneo na changamoto zao

Nimeishi mikowa mingi na ukweli nikwamba

-Mwanaume ndiyo chanzo kikuu kwa mwanamke kutafuta ushirikina

-Mwanaume unapokuwa macho jujuu nakutoeleweka kwa mkeo basi utalishwa vitu vingi vya hovyo.

-Mwanaume ukishindwa ku-prove beyond reasonable doubt kwa mkeo kuwa unampenda basi utaendewa kwa waganga mpaka uchanganyikiwe

Wapendeni wake zenu, prove that she is one and no one....hapo hutasikia mwanamke anatafuta uganga na dawa za mapenzi
 
Twilumba

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Messages
7,377
Points
2,000
Twilumba

Twilumba

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2010
7,377 2,000
Mimi nina mtanzano wangu ni tofauti,
Nimeoa Tanga lakini mke tulikutana mkoa mwingine na makuzi ya Binti hayakuwa ya Tanga huenda hilo limesaidia. Kimsingi kwangu hakuna ndugu zake hata wakija ni mara moja wanarudi walikotoka in few days!

Kuhusu Ushirikina sina pia exprience coz sijawahi ona hayo lakini ninachojua Familia ile ni ya wacha Mungu, wana kaka ambaye ni mchungaji na wazazi wanaabudi kwa mtumishi mmoja wa Mungu maarufu na mwenye hofu ya Mungu kwelikweli!!

Tumejenga, tuna kajiusafiri watoto wanasoma shule nzur nk.

Sifa kubwa ni ujuzi wa kupika aisee hapo ndio nawavulia kofia!
 

Forum statistics

Threads 1,403,647
Members 531,313
Posts 34,430,187
Top