Mnaokataza maandamano na mijadala ya Katiba, someni historia

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Siku za karibuni kumekuwa na vitisho vingi kila mara wadau mbalimbali wanapotaka kuandamana, kufanya mikutano ya hadhara, midahalo hata kujadili mchakato wa katiba mpya ambayo imepitishwa kinyemela na wabunge wa ccm na kusainiwa na mwenyekiti wa ccm ambaye pia ni Rais wa JMT.

Vitisho vimekuwa vingi kutoka polisi na vyombo vya sheria, na hatimaye kutamkwa hadharani ya kuwa atakayepinga suala la kupitishwa kwa katiba hiyo kinyemela, basi sheria itachukua mkondo wake na atafungwa au kutozwa faini.

Hii yote inaonyesha kwa ufinyu mkubwa wa upeo wa hao waliopo madarakani na kukosa ukomavu wa kisiasa. Kwa kiingereza ninaweza kuita 'lack of maturity' katika upeo wao wa kutathmini ukweli wa mambo. Leo hii tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania) na inaelekea watu wengi wakiwemo viongozi wa nchi hii hawajui au hawakusoma historia ya nchi yetu.

Mbinu wanazotumia wao leo hii ni sawa sawa na zilizotumiwa na wakoloni wa kudai uhuru. Chama cha TANU kilipoanzishwa mwaka 1954, serikali ya wakoloni iliweka vikwazo vingi sana vikiwemo kuzuia wafanyakazi wazawa wa serikali ya kikoloni kutoruhusiwa kujiunga na chama hicho.

Hawakufua dafu. Wakazuia mikutano ya hadhara ya TANU, matokeo yake ikawa wanachama wa TANU wanakutana kwenye migahawa. Hapo ndipo bibi Titi Mohamed alipåoingia TANU. Yeye alikuwa na mgahawa wake Temeke, na pale ilikuwa sehemu muhimu sana kwani wanachama wa TANU waliweza kukusanyika na kufanya vikao vyao bila bugudha. Akiingia mpelelezi wa wakoloni watu wako kwenye kunywa chai na vitumbua.

Hiki kitu wale wote wanaolala usingizi mzito na kudhani kuwa wananchi wataacha kuijadili katiba mpya kwa kuwa mnawatisha mjue wataenda undergound, na katiba wataijadili! Tanzania siyo yenu, ni yetu sote.

Ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo! Hamwezi kuwanyima haki yao wakakaa kimya. Wahenga walikufa kuipigania nchi hii ambayo ninyi mnaifilisi na mnatumia katiba hiyo hiyo kujilinda. Kama ambavyo moto wa TANU haukuweza kuzimwa na wakoloni, moto uliowashwa na wanaharakati na vyama vya upinzani hususan CHADEMA utaendelea kuwaka. Hilo mlijue!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom