Mnaokaa Mwanza, mnaoifahamu Mwanza vizuri msaada wenu tafadhari kwa mdogo wenu

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,097
2,000
Habarini za asubuhi hii ndugu zangu, poleni na miangaiko ya hapa na pale kwa jumatatu hii ya leo.

Niende kwenye maada moja kwa moja.

Baada ya kuangaika kutafuta ajira kwa mda mrefu atimae nime-bahatika kupata sehemu ya kujishikiza kwa muda mfupi kidogo (ni project), Niliachoamua mpaka sasa ni kifuatacho.

nataka nitunze pesa kadri ya uwezo wangu (maana kwa msoto wa kutafuta ajira niliouona sitaki kuchezea kabisa pesa ntakayo-ipata).

baada ya hii project kuisha tu (mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao project hii ninapofanya kazi inatarajia kuisha)...nataka kwenda mkoa wa mwanza kutafuta eneo (ardhi) naitaji eka moja/mbili kulingana na bei na kiasi nitakachokuwa nacho eneo liwe zuri kwa makazi na eneo liwe na makadilio kuwa ndani ya miaka mitatu au mitano kutoka sasa linaweza kuja hot-cack.

ndani ya izo eka mbili au moja, nataka kujenga nyumba ndogo yenye vyumba viwili, sebure, na choo (kwa kutumia tofali za kuchoma), nataka nifanye kilimo kidogo cha mboga za majani, na ufugaji mdogo na project zinginezo.

ndani ya iyo nyumba ntakayojenga, ntatafuta mtu mzima mwenye heshima zake atakayeweza kunisimamia project zangu nakazozifanya ndani ya eneo langu akae hapo free pasipo kunipa chochote ila kikubwa asimamie na kuniangalizia project zangu zozote ntakazoziwekeza katika eneo langu.

Wakati huo mimi nikiwa katika harakati zingine za kupambana na maisha, na endapo mapambano yakienda mrama narudi kwangu kwaajili ya kufanya implementation za usimamizi wa project zangu mimi mwenyewe kwa kukaa na kuanza maisha rasmi katika eneo langu.

Nninachoomba ni kutoka kwenu wadau, je ni target ya kiasi gani natakawa kuiandaa kwaajili ya kupata eneo lenye ukubwa nilioukusudia (eka mbili/moja), ni gharama kiasi gani ntatumia kujenga nyumba iyo ndogo niliokusudia ndani ya ilo eneo, ni mwanza sehemu gani ntapata eneo la namna iyo ninayoitaka

Karibuni kwa michango yenu, ushauri wenu, na mawazo yenu kwa mimi mdogo wenu ninyepambana na maisha aya.

Mungu awabariki sana.
 

nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
1,088
2,000
Karibu mwanza. Njoo eneo linaloitwa Mayolwa liko barabara kuu ya Usagara Kigongo Ferry . utapata eka 2 kwa milioni 4 au nne na nusu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom