mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,760
- 35,205
CHADEMA na Vyama vingine vya upinzani wakati umefika sasa mkae chini na kujitafakari!
Tena mjitafakari na kuwa wakweli nafsini mwenu kwamba siasa mnazofanya ni kwa maslahi ya familia zenu huku vyama vyenu vikiwa havina hata misingi imara kwa jamii
Hakuna mtanzania anayekataa au asiyejua umuhimu wa upinzani katika taifa lakini hakuna mtanzania anayeweza kukubali upinzani usio na dira wala maslahi kwa wananchi walio wengi.
Vyama pinzani Tanzania vimekua vyama vya watu wachache ambao ni viongozi wa vyama hivyo. Vyama pinzani havina msingi imara sababu nguvu yao kubwa iko kwa viongozi huku wananchi wakiwa hajui wala kuona maslahi yoyote toka kwa vyama hivyo zaidi ya wao kutafutwa tuu wakati wa kupiga kura.
CCM wanaielewa jamii ya watanzania kwa uzuri sana ndio maana upinzani mnaishia kupumilia mashine kila uchaguzi.
Na kinachozidi kuwapoteza ni kwamba viongozi wote wa vyama vya upinzani sio wakweli kwa vyama vyenu wala kwenu wenyewe. Mmeshindwa kuwa wakweli sababu hamuangalii nyie na vyama vyenu vinawafanyia nini watanzania na nchi yetu kwa ujumla Ila mnaangalia tuu vyama vinawawezeshaje nyie binafsi na familia zenu kuishi maisha mazuri.
Watanzania wameshawaelewa na wanawapuuza sababu ubinafsi wenu umewafanya mjifikirie wenyewe na kusahau kwamba wananchi ndio mtaji wenu
Upinzani unapogeuka kuwa sehemu ya kujipatia rizki lazima malengo ya chama yasahaulike ili kufanikisha kwanza maslahi ya wachache.
Watanzania sio wajinga mnavyofikiria, ushirikiano wapinzani mliofanya na ccm hadi kufanikisha kumuondoa Lowasa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu uliwajengea heshma kubwa na imani kwa jamii, na maana halisi ya upinzani ilidhihirika! Ila sasa, usaliti mlioufanya kwa wananchi kumpa huyohuyo jamaa nafasi ya kugombea urais haujasahaulika, hautosahaulika na hamjasamehewa
Wananchi wanajiuliza, kama Lowasa aliweza kuwanunua chadema wakageuka wasaliti kwao si taifa lolote lenye fedha linaweza kuitumia chadema kuwanunua watanzania?
Mkiweza kupata wataalamu wa siasa na uongozi nje ya vyama (wasiokua na maslahi binafsi) watakaoweza kufanya utafiti wa kueleweka jinsi ya kuimarisha chama na kujenga imani kwa wananchi. Mkamwacha huyo mtaalamu awatengenezee mfumo na mbinu za kujenga vyama
Mkamwacha awasimamie nyie viongozi ili kuhakikisha mnatimiza kile anachowaambia kwa muda uliopangwa mtainuka tena na kuwatumikia wananchi
Vinginevyo CCM itaendelea kuwa chama pekee chenye nguvu Tanzania na wapinzani mtaendelea kulalamika kwa tatizo lilelile miaka30
Na sisi kina mama D tutaendelea kusema KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan🙏