Mnaojenga nyumba, kuweni makini na watu mnaowaomba wawalindie nyumba zenu

Kuna watu wengi sana wamefanyiwa hivyo na wala hawajijui mpaka watakapofunguliwa kwa Neema za Mungu.

Na labda iwe bahati yako vinginevyo kama ameuza na kuondoka na majirani hawakujui ndo Basi tena
 
Miji inakuwa kila siku, eneo ambalo ni shamba baada ya muda huwa mjini.

Mfano maeneo mengi awamu hii kuna zoezi la upimaji wa jumla wa maeneo watu kuchangia shilingi 150,000 kwa kila kiwanja baadae taratibu za hati kufuata,

Lakini cha ajabu Eti kuna wenye maeneo hawana hata taarifa ya kinachoendelea sababu waliowaacha kwenye maeneo hawajawapa taarifa yoyote na wao kwa kuwa huwa hawaendi na kusalimia majirani hata kwa simu wanakuwa hawajui chochote
 
Sasa hivi maeneo kama vile Bunju, Madale na viunga vyake n.k upimaji umefanyika kwa gharama ambayo kidogo ni nafuu ukilinganisha na zamani.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amekuwa akiongea na wananchi kuhusu urasimishaji wa maeneo hayo.

Wengine ambao wako siriasi wametumia hiyo fursa vizuri na hati wameshapata hata kama unaviwanja vingi kiasi gani haijalishi.

Mkuu wa Wilaya amesimamia vizuri Yani ukishalipa hakuna Usumbufu kabisa,

Ukienda pale Manispaa ya Kinondoni kufuatilia wanakusikiliza vizuri na yule afisa ardhi ni msikivu kwa wananchi na team ya maofisa wake isipokuwa wachache tu ndo wanavisirani kwa wateja/wananchi.

Ikishatumwa wizarani unapata meseji ya kulipia popote ulipo unalipia baada ya wiki mbili tatu unapata ujumbe wa muamala wako kusajiriwa na hati tayari unazifuata wizarani unapewa bila usumbufu.
 
Si tulipohamia tukawa hatulali usiku, Yaani nyumba kelele hatari, mara milango inafunguliwa Mara geti linabamizwa nk. Imechukua kama 4 years ikaisha.

Huyo tuliomuweka alikaa for 4 yrs, kila tukitaka kuhamia tunasita, tulihamia gafla. Ndio kuja kupata stori kwa Majirani kuwa alikua anajitapa eti hatutakuja kuhamia kamwe! Tukaambiwa waganga mbalimbali walikua wanashinda katika nyumba..

Afadhali ukodi kampun ya ulinzi kuliko Hawa wa mitaani...

Sasa hii ndo kali zaidi, Kuna jirani yetu eti kajenga tangu 1985. Ni mtu mzima, anakujaga anaikarabati nyumba anaondoka
Imagine nyumba zipo 2 ktk kampaundi moja hata hajazipanisha anayeishi ni Hawa wababu hahaha, nyumba nzuri mno.

Yaani watu humuonea huruma sana. Babu anayetunza kashaoa Mara 5 kazaa na watoto kibao hapohapo, mwenye nyumba anakuja na kuondoka yaani huwezi kuamini kabisa.
 
Kuamini kwenye nguvu za giza lazima kwanza nawe uwe Mshirikina.

Pili kuamini kwamba binaadamu mwenzako mnayefanana kwa kila kitu kwamba ana uwezo wa kuhusika na hisia au nafsi yako ni kumtukuza kulikopitiliza.

Kama huyo anayetuhumiwa ana huo uwezo wa aina hiyo kwa nini asiweze kupata mali tena kwingine?, au la basi angekuwa na mali zaidi ya hiyo.

Tunaposema kupambana na umasikini, ujinga na maradhi, basi tukumbuke ya kuwa huwezi kuondoa ujinga kama bado una mamilioni ya Watu wanaoamini kwenye mambo ya kusadikika. yaliyokosa uhalisia.
 
Unajua watu wengi hawafahamu kuwa wachawi wapo mjini mfano angalia nyumba nyingi ukianza kujenga ikafikia sehemu ya finishing ukaweka mmasai mlinzi au mmakonde na wengine ujue nyumba hiyo huwezi kuimalizia itakaa hivyo hivyo mda mrefu utakuwa umeisahau kabisa...
Nipe kazi ya kupangisha halaf nitakuwa nakuletea pango ili tupate hrla kama wewe unaogopa
 
Kuna bro wangu ingawa scenario yake ni tofauti kidogo yeye yupo nje alijenga nyumba yake Makongo halafu akaweka mlinzi kwa miaka kadhaa amlindie yule mlinzi baadaye bro alipotaka kuweka mpangaji jamaa akagoma akidai nyumba ni yake hawezi kutoka au alipwe ilikuwa issue nenda mpk mahakamani huko ndiyo kushindwa akatolewa

Ni makosa sana kumwachia nyumba mtu bila maandishi ya kisheria, binafsi nimeshuhudia ndugu za marehemu wakiinunua nyumba iliyokuwa chini ya uangalizi wa mtu baki kwa gharama kubwa ya kilichoitwa ....ULINZI
 
Back
Top Bottom