Mnaojenga nyumba, kuweni makini na watu mnaowaomba wawalindie nyumba zenu

Haya mambo yapo tena miaka ya nyuma yalishamiri sana hasa nduguzetu makonde chale waliteka sana nyumba na viwanja huko Msasani lakini baada ya wamiliki kushtuana walilazimika kurudi kwao Msumbiji maana sio kwa kudhalilika kule, haiwezekani ujenge nyumba uweke mlinzi. Imekula kwako, jenga hamia mwenyewe hata kama mbavu za mbwa vinginevyo imekula kwako.
 
Ila baada tu ya kumuweka huyo jamaa kama mlinzi ALISAHAU kabisa kuhusu ile nyumba na hakuwahi kukumbuka kama ana ile nyumba mpaka alipobahatika kwenda kuombewa huko kwenye makanisa ya walokole (though alienda kwa shida nyngne)

Dunia ina mambo mengi sana, TUWENI MAKINI JAMANI
Mimi na jamaa yangu tulisahaulishwa mashamba yetu Bagamoyo toka mwaka 2014 mpaka leo hatujawahi kurudi hata sikumbuki ni eneo gani. Watu wako vizuri sana huenda hata walishayauza kwa wengine.
 
hata nyie ambao mna biashara mmeweka watu wasimamie angalieni sana tuna ushuhuda mwenye mali haongei chochote kwa mfanyakazi wake inafikia hatu mwenye mali anamuachia mfanyakazi ile mali

watu wanaloga nyie acha yani boss unalogwa mpaka unasusa mali yako kama unatakiwa kagua hesabu ukagui ukifika unaishia kwenye gari tu ushuki
 
Atakua na nyumba nyingi huyo jamaa.

Masikini/choka mbovu mwenye kuishi kwny ka-banda ka-mbwa ka kupanga huko uswazi hawezi kusahau nyumba yake anayoijenga kamwe.
Mkuu usipende kubisha jambo ambalo hujawahi kukutana nalo ktk maisha ya duniani. Pengine mtoa post ameshindwa kueleza vizuri tukio lilivyo Lakini ni kweli baadhi ya watu wanaokabidhiwa nyumba kulinda sio watu wazuri. Zipo nyumba nyingi hadi leo zinamilikiwa na walinzi wa kimakonde na wenye nyumba zile hawajulikani walipo. Na wao kujimilikisha kama ni zao.

Ipo nyumba moja Magomeni nyuma ya police Magomeni, Ile nyumba tangu miaka ya 1980 hadi leo ipo vile vile, Ilikuwa inaishi family fulani ya Mzee wakimakonde. kila mtu alijuwa kama ni mlinzi na wenyewe hajulikani. Ilikuwa nyumba nzr sana na mjengo wa kizungu na bati fulani za design ya pekee kabisa, inaonyesha mwenye nyumba ile alikuwa na nguvu sana kipindi kile.

Lakini hakuna ambaye aliyekuwa anamjuwa mwenyewe zaidi ya yule babu mlinzi pekee. Tangu 1980 mwenyewe hajawahi kukanyaga pale kwenye nyumba hata yule mlinzi alipokufa miaka ya 2000 bado mwenyewe hakutokea. Mzee alipokufa, wakaibuka watu wanaojuwa history ya nyumba ile wakiwa na documents fake.

wakawatingisha family ile ya mlinzi na kusema nyumba ni yao. Walipoulizwa miaka yote mlikuwa wapi? Jamaa akasema
kwamba miaka yote alikuwa ng'ambo kakimbia uhujumu uchumi kipindi cha nyerere. Miaka ile ilikuwa mambo ya azimio la arusha na mafisadi kupokonywa mali. Sasa amerudi anataka nyumba yake.

Jamaa akiwa na documents zote za nyumba.

Ile family ikalipwa kiasi cha pesa fulani kama malipo ya baba yao kulinda nyumba hiyo kwa miaka yote. wakahamishiwa kinondoni Moscow, Jamaa wakaanza ukarabati wa nyumba. Baada ya mwezi nyumba ikapigwa stop na serikali. Hilo ni baada ya kugunduwa kuna utapeli wa umiliki halali wa nyumba ile. Hadi leo nyumba imezungushiwa mabati ipo vile vile bado mwenyewe halisi hajulikani.

Aliyekuwa anamjuwa mwenyewe ni yule mzee mlinzi wa kimakonde pekee. Haya mambo ya uchawi na ulozi wa sahau nyumba au shamba yapo mkuu. Kinachofanyika ni mlinzi kukupiga kijini sahau au unapigwa kijini usingizi, Kukufanya uipuuze nyumba yako, hata usiimalizie tena na yeye aendelee kukaa maisha yote kwenye nyumba ile.

Kila ukikumbuka kwenda kwenye nyumba unasema utaenda kesho, kila siku utakwenda kesho na hufiki wala hufanyi chochote cha maendeleo pale ndani, miaka inakatika tu. Na hata siku ukikumbuka kufika pale,,zile gharama za kumtoa mle ndani ni kumjengea mlinzi nyumba ingine aishi.

Dunia ina mambo mengi sana usiyoyajuwa.

Kama bado hujakutana na jambo basi usikatae lolote jipya unalosikia.
 
Tena mkuu umenizinduwa usingizini, wacha nijiandae nielekee Kibaha. Nina jambo langu kule lakini sijakanyaga huu mwaka wa 5 tangu 2015 sijafika pale.

Huyu bibi jirani niliyemkabidhi eneo langu anitizamie naishia kuongea nae kwenye Simu tu miaka yote.

Kila nikitaka kwenda nasita sana.

Leo nakwenda na sijuwi kama nitakwenda kweli naona moyo bado mzito sana.
 
Unajua watu wengi hawafahamu kuwa wachawi wapo mjini mfano angalia nyumba nyingi ukianza kujenga ikafikia sehemu ya finishing ukaweka mmasai mlinzi au mmakonde na wengine ujue nyumba hiyo huwezi kuimalizia itakaa hivyo hivyo mda mrefu utakuwa umeisahau kabisa...
Yani una akili ya kujua fremu iko wazi na wateja wapo halafu unasema umelogwa. Labda kama una wadudu unawafuga huko kwenye hizo fremu.
 
Wasalaam,

Naomba tu kutoa wito kwa wale wenzangu na mimi tunaojidunduliza ili kujenga nyumba za kuishi na familia zetu kuwa MAKINI sana na WATU tunaowaweka wawe walinzi wa nyumba zetu..
Hapo umakini wa kibinadamu hautasaidia lolote. Yesu hakuja duniani kuzurura.Alikuja akijua fika tunamuhitaji sana,hasa kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wetu wa kibinadamu kama haya.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Wasalaam,

Naomba tu kutoa wito kwa wale wenzangu na mimi tunaojidunduliza ili kujenga nyumba za kuishi na familia zetu kuwa MAKINI sana na WATU tunaowaweka wawe walinzi wa nyumba zetu....
nimecheka saaana. Nimekumbuka enzi hizo kuna mwenye nyumba aliipangisha nyumba yake yote kwa familia fulani. Ila baada ya kupita kipindi fulani na kodi ya mpangaji kuisha, mpangaji akawa halipi kodi.

Mwenye nyumba akaamua kumfata kule kule. Ila kila akienda, anapotea njia, atazungukaa wee karibia siku nzima alaf anaamua tu kurudi home. Hiyo hali ikajirudia karibia miez 4 mfululizo, hadi siku hiyo akaamua kwenda na mganga, ndio akabahatika kuiona njia.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom