Mnaojenga hoja za UDINI kwenye uchaguzi kwa maslahi yenu hamuitakii mema nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaojenga hoja za UDINI kwenye uchaguzi kwa maslahi yenu hamuitakii mema nchi yetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Aug 6, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nimesoma posts nyingi sana humu za baadhi ya watu na naona ni wale wanaompinga Dr. Slaa. wengi wao wanasema huyu ni mkatoliki mara ni padre n.k.
  napenda kutoa angalizo kwa watu hawa, unapo-propagate udini na kuwafanya watanzania wamchague raisi wao kwa misingi ya dini madhara yake yatakuwa makubwa sana. kwa sasa unaweza kufikiri ni mbinu nzuri ya kumdhoofisha mgombea mmoja dhidi ya yule unayempenda. VITA ya kidini itakapoanza usifikiri wewe utapona - As long as wewe ni mtanzania na unaisha Tanzania utakuwa victim wa vita hiyo na hata kama utakuwa unaishi nje ya tanzania bado utakuwa victim tu hata kama ni indirectly.

  Nchi ikiingia kwenye vita ya kidini hutapona na machafuko yake ni vigumu sana kuyazima kwa maana ni suala linalohusu imani za watu.

  Hivi unaweza kumpata raisi Tanzania asiye na dini? kama hatakuwa muislam atakuwa mkristo ama mhindu ama mwenye dini ya kipagani! Mnaposema aaa huyu ataongoza kiislam au kikristo / kikatoliki ama kidini yoyote ile, hivi tanzania haina katiba? Akiongoza atakavyo si atakuwa amevunja katiba?

  Hebu mpigieni kampeni mtu kwa merits zake za kiuongozi na maadili mema siyo dini yake?
  mbona wote waliotajwa kuwa mafisadi wana dini zao? wengine waislam wengine wakristo na wangine wana dini nyingine mbalimbali lakini wote hawakuwa na maadili mema.

  Just imagine, kundi moja likiinuka na kusema Dr. Slaa ni mkristo-mkatoliki asichaguliwe na lingine likaja na kusema Kikwete ni muislam ataisilimisha nchi tusimchague kweli tutampata raisi?

  Tuachane na mambo ya kidini katika kumchagua raisi. Jengeni hoja zenye nguvu katika kumnadi mnayempenda siyo kutuletea machafuko nchini mwetu.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  hivi kunasheria inayokataza kiongozi wa dini kuwa Kiongozi wa serikali,

  Malaria Sugu na Tumaini hebu niambieni

  KIKWETE ALIPOMCHAGUA MCHUNGAJI (MAMA RWAKATARE) KUWA MBUNGE, MBONA WAISLAMU PAMOJA NA NYIE (MALARIA SUGU na TUMAINI) HAWAKUPIGA KELELE, HAPA TATIZO NI NINI KWA PADRI WA ZAMANI KUGOMBEA URAISI, HATA SHEE SIMBA NA KADINALI PENGO WANA HAKI YA KUGOMBEA NAFASI YOYOTE YA UONGOZI TANZANIA, KWA MUJIBU WA KATIBA ILIYOPO
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ole wenu MS na magazeti uchwara ya Habari Corporation kwa tabia zenu za kupiga kampeni kwa njia ya kulazimisha siasa za udini, ipo siku historia itawahukumu wazandiki na wafitini wakubwa.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Ni kweli humu ndani kumekuwa na hoja zenye basis ya udini, na wasiwasi wangu ni kwamba hawa members ni wabaguzi si wa dini tu hata ukabila, rangi na mwenye nacho na asiye nacho. Humu members wote wanatakiwa kuwa interectuals wenye at least bachelor degree iliyopatikana bila 'kudesa'. Wenye uwezo wa juu wa kuchambua mambo na kutoa theses zenye mantiki.

  Hivi kwenye kujiunga tuna kipengele cha level of education (sikumbuki nitaangalia baadaye!)? Kama hakuna, Invisible please add it as a requirement! Moderation ifanyike kwa makini ingawaje ni kazi kidogo!!

  Tumjadili mgombea urais yeyote kwa uwezo wake na kama anaonesha kutaka back-up ya msikiti au kanisa au Bagamoyo mlingotini basi tumshutumu kwa hilo, lakini kama haoneshi hayo kwa nini kumpaka matope?
   
 5. m

  mkenda1000 Member

  #5
  Aug 6, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,651
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  Hawa wanaojenga hoja za udini siyo wadini ki hivyo, hawa wametumwa na CCM kwa nia ya kupunguza kuungwa mkono Dr Slaa na watz wengi. Huu ni mpango mahsusi ulioandaliwa Taasisi nyeti ya dola , na katika utekelezaji wake inafadhiliwa na RA(muajemi) kupitia waandishi wa habari uchwara wa vyombo vyake vya habari na baadhi ya mitandao, na wengine wako humu jamvini.Lakini waelewe kuwa huyu bwana wao siyo raia, siku kikiwaka moto hapa anapanda ndege anaondoka sisi wote pamoja na wao ndiyo tutakuwa wahanga wa vurugu wanazozipanda sasa kwa sababu ya njaa zao.Mtu yoyote anayeendekeza udini ni mpuuzi, amefilisika ki****, kwani dini ni jambo binafsi la mtu na Mungu wake anayemuamini na kumuabudu. Hawa wote ni wahaini tu wanastahili kupigwa risasi.
   
 7. A

  Audax JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  dini isiwe kigezo caha uchaguzi-tuchague na kumnadi mgombea kwa sifa ya kutuletea maendeleo na c vinginevyo.Vita cyo nzuri jamani, Hili muombe kulickia huko lkn likipiga hodi haliishi ndugu zangu.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mtu yeyote anayeingiza udini katika nchi yetu basi amefirisika kifikra. Tunampima kiongozi wetu kwa uwezo wake wa kuongoza na si kwa kabila lake au dini yake - uwezo wa DR. Slaa unaonekana waziwazi - kiongozi makini anayehitajika kwa sasa kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa taifa letu. MS na wenzake hawana hoja za msingi ndiyo maana wameamua kukimbilia kwenye udini ili kujustfy uhafifu wa fikra zao.
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,651
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  Toa ushahidi wa Chadema kuungwa mkono na maaskofu, tumechoka na kelele zenu zisizokuwa na mashiko, acheni uhaini huu kwa vipande vya fedha, wekeni maslahi ya nchi mbele.
   
 10. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tumain, jaribu kutumia akili angalau kidogo! Profession ya Nyerere ilikuwa ni ualimu na siyo uraisi na ndiyo maana alikuwa anajulikana kama mwalimu nyerere. Ualimu wake haukutufanya wote tuwe walimu. Mwinyi ni mtaalamu wa kiswahili hakusomea uraisi na wala hakutufanya wote tuwe wataalamu wa kiswahili! Kikwete ni afisa mkubwa wa jeshi hakusomea uraisi na hajatufanya wote tuwe wanajeshi!! jaribu angalau kutofautisha professional skills na leadership skills. Kwani Dr. Slaa alipokuwa bungeni alitekeleza mambo ya TEC? Kama kupinga ufisadi na kutetea wananchi ni kutekeleza mambo ya TEC na ni kwa sababu ya PHD ya kanuni za kuongoza kanisa basi I would prefer that.
   
 11. F

  Fanta Member

  #11
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kigezo cha dini hakina mashiko kabisa.........awe mkristo au mwislam au mpagani sio sifa pekee ya kumfanya mtu awe kiongozi bora.

  najaribu kujiuliza hata hao marais walopita si walikuwa na taaluma zao ambazo hazikuwa 'za kidini', je wamelifanyia nini taifa?
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tukianza kuleta siasa za udini ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu,hivi hatuoni mifano?Nigeria kulitokea nini kutokana na haya haya tunayojaribu kuyashikia bango kama vile ni watu tusiokwenda shule na kuweza kuchambua jema na baya,hivi mtanzania wa leo unapozungumzia udini una maana gani?Mimi nadhani wote wanaozungumzia udini humu ndani si watanzania wazalendo wenye kuitakia amani nchi yetu na inatakiwa tuwatenge na ikibidi kuwasambaratisha kabla hawajatugawa.
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,651
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  Lete ushahidi,
   
 14. F

  Fanta Member

  #14
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli inashangaza, tumeanza lini haya mambo na yana manufaa gani? dini inaweza kumfanya mtu akawa bora kuliko mtu wa dini tofauti na yake kweli?
   
 15. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Tukilalamika eti Slaa ataifanya nchi hii ya kikatoliki..tukumbuke mifumo yetu ya sheria ina pancha...
   
 16. m

  masasi Member

  #16
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tumaini umesikia kuwa wenye phd za kikete type wananyanganywa?ni wakati wako kujenga hoja juu ya mgomea wako jk kwanza,maana huwezi kuondoa kibanzi wakati jicho lako lina boriti
   
 17. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono mkuu. Sasa hivi kuna watu wana matatizo ya akili. Nashindwa kuelewa utamaduni tulioujenga siku nyingi wa kuheshimiana na kuaminiana bila kujali dini wala kabila ya mtu unaanza kuchafuliwa. Natumaini hawa watakuwa ni vijana ambao hawajapita JKT. Nafikiri JKT ingerudi vijana wangekuwa na nidhamu ya kuheshimiana. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 18. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono kwa asilimia 100%. Lakini jambo la kupinga hoja za kidini lisiishie kwa Dr. Slaa tu!!! maana hapo nyuma kuna watu walikuwa wakihoji dini za watu katika kila sector bila kujali uwezo wa watu hao.
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Tumaini na Malaria Sugu Je na wakristo wakisema nchi haiwezi kuongozwa na waislamu Bara na Zanzibar kwa miaka 10 watakuwa wamekosea, Rais Mwislamu, Makamu Mwislamu na Rais wa Zanzibar Mwislamu na hapo je? si chuki tayari hizo.

  Ni kweli hawa jamaa wanaongea bila kujua impact yake, sisi tunamchagua DR. Slaa kwa utendaji wake wa kazi na si vinginenvyo, wao na kundi lao wanakuja na hoja ya upadri wa katoriki... endeleeni mnafikiri hiyo propaganda yenu lakini mjue mnaiweka nchi kwenye matatizo makubwa - mnapandikiza chuki kwa wananchi kupitia udini. Tumaini na Malaria Sugu na kundi lao lazima waonywe mapema wasiendelee kupandikiza chuki na uchochezi bila sababu za msingi.
   
Loading...