Mnaofuatilia Sultan, msisimke sana.. Hurrem, Pasha na Mustafa ni expendables!

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
DISCLAIMER: Tamthiliya hii sio ya kimama kama wengi wanavyoichukulia. Ni historical fact so nikisikia watu wanawabeza wanaume kuitazama nabaki kusikitika tu. Nakumbuka niliisoma hii historia kwenye mafundisho ya dini miaka ya nyuma. Nikaja kuisoma tena kwa undani kutoka kwenye mtazamo wa kihistoria kuhusu tawala zilizotikisa ulimwengu - Ottoman ikiwemo. Ni historia ya kibabe sana na miamba iliyowahi kutikisa dunia hii. Tusiichukulie poa!

Back to the topic

Ni historia ya kusisimua sana. Naamini na tamthiliya nayo itakuwa vivyo hivyo. Huu ni utawala ambao umeacha alama kubwa kutokana na kutawaliwa na vituko kuliko tawala zote za Ottoman zilizopita. Ni visa vya mapenzi, urafiki na utawala.

Historia hii pia inahuzunisha sana. Vifo, usaliti, fitna vimetawala ndani ya hekalu la Mfalme.

Kwa mfano:

Matukio ya hivi karibuni
  • Mustafa atamuoa binti Hellena
  • Nigar kalfa atafanikiwa kutoroshwa. Mtoto wake atakulia sehemu nyingine kwa kufichwa. Jina lake ataiwa Kadar/Kadir.
  • Hurrem atamuagiza Rustem Pasha amuue suria Feruze. Rustem Pasha atagundua siri ya tattoo ya Feruze shingoni, atamwambia Hurrem naye atamwambia Sultan kisha suria huyo atafukuzwa.
Matukio ya baadaye
  • Ibarahim Pasha ataalikwa dinner/futari na kuuwawa na Mfalme Suleyman na kurithiwa nafasi yake na Ayas Pasha
  • Mustafa atauwawa na Mfalme Suleiman kutokana na fitna za Hurrem, watu kumpenda na hofu ya kupinduliwa itakayomkumba Sultan.
  • Hadija Sultan atajiua kwa hofu ya adhabu ya Sultan baada ya kufanya mchezo hatari wa kumuweka mateka Hurrem.
  • Hurrem atafariki dunia kwa maradhi
  • Watoto wa Hurrem watauwawa. Bayezid na Selim 2 watakuwa na bifu wakigombea madaraka. Jihangir atakufa kwa sonono kufuatia kifo cha kaka yake, Mustapha.
  • Sultan Suleiman ataugua na kufariki dunia. Selim 2 (cha pombe) atamrithi.
Hiyo ni kwa mujibu wa Historia ninayoifahamu. Utawala wa 10 wa Suleyman pale Ottoman. Mfalme ambaye alibadili kanuni nyingi za utawala katika kipindi chake.

Sijajua Azam Two watatufikisha wapi lakini angalau nimeona wanaingia mule mule. So, natoa fursa kwa wanaopenda kujua yajayo, waniulize maswali nami nitajibu kwa kadri ya kumbukumbu zangu.

Poleni team Hurrem na team Pasha in advance.
 
Teh teh mwanaume wa dar ukijaribu kuwachambulia tamthilia wanaume wenzako wa dar,teh teh natania mkuu msije kunipiga na kipande cha kanga arifu.
Hahah Sultan alikuwa zaidi ya wanaume wa mikoani mkuu.. Undava mwingi sana!
 
Wanaume wanaoangalia Sultan
IMG-20181013-WA0002.jpg
 
Sasa mbona unaharibia watu burudani zao mkuu na hii spoiler?
 
Wachache watakuelewa hasa kwa upande wa wanaume

Ila hata kama huangalii ya nini tupangiane namna ya kuishi majumbani mwetu???

Kwa mfano mtu ukaamua kuishi maisha yako kipi kitapungua?? Mwanaume ameamha kuketi na kutazama tamthilia shida iko wapi????? Tunapenda kufatana fatana kama mikia, kama mtu ameamua kutazama atazame kwa starehe yake
 
Wachache watakuelewa hasa kwa upande wa wanaume

Ila hata kama huangalii ya nini tupangiane namna ya kuishi majumbani mwetu???

Kwa mfano mtu ukaamua kuishi maisha yako kipi kitapungua?? Mwanaume ameamha kuketi na kutazama tamthilia shida iko wapi????? Tunapenda kufatana fatana kama mikia, kama mtu ameamua kutazama atazame kwa starehe yake
Ndio madam umenena vyema siwaungi mkono na wala siwapingi
 
DISCLAIMER: Tamthiliya hii sio ya kike kama wengi wanavyoichukulia. Ni historical fact so nikisikia watu wanawabeza wanaume kuitazama nabaki kusikitika tu. Nakumbuka niliisoma hii historia kwenye mafundisho ya dini miaka ya nyuma. Nikaja kuisoma tena kwa undani kutoka kwenye mtazamo wa kihistoria kuhusu tawala zilizotikisa ulimwengu - Ottoman ikiwemo. Ni historia ya kibabe sana na miamba iliyowahi kutikisa dunia hii. Tusiichukulie poa!

Back to the topic

Kutokana na wife kuwa mfuatiliaji mzuri wa tamthiliya hii inayoendelea kushika kasi nchini kupitia Azam Two. Nimejikuta nikiwa naungana nae siku moja moja kuitazama.

Ambacho nashindwa kumweleza ni kwamba nafahamu mtitiriko mzima wa historia hii so najua kila kitakachotokea. Wasiwasi wangu, nikianza kumsimulia yajayo atakata mzuka kwa sababu yeye ni shabiki namba moja wa muigizaji Hurrem Sultan.

Kwa kuwa yeye si MwanaJF, nimeona nije kuwagusia kidogo Wadau wa tamthilia hii mlioko humu kwamba msiwe excited sana maana yajayo hayafurahishi sana.

Kwa mfano; matukio ya hivi karibuni..
  • Mustafa atamuoa binti Mihrunissa kwa siri
  • Nigar atafanikiwa kutoroshwa. Mtoto wake atakulia kwenye mji mwingine. Jina lake ataiwa Kadar.
  • Hurrem atamuagiza Rustem Pasha amuue suria Feruze. Rustem Pasha atagundua siri ya tattoo ya Feruze shingoni, atamwambia Hurrem naye atamwambia Sultan kisha suria huyo atatoswa na kupelekwa mbali.
Matukio ya baadaye;
  • Ibarahim Pasha ataalikwa dinner na kuuwawa na Mfalme Suleyman hivi karibuni na kurithiwa nafasi yake na Ayas Pasha
  • Mustafa atauwawa na Mfalme Suleiman kutokana na watu kumpenda na hofu ya kupinduliwa itakayomkumba Sultan huyo.
  • Hadija Sultan atajiua kwa hofu ya adhabu ya Sultan baada ya kufanya mchezo hatari wa kumuweka mateka Hurrem.
  • Hurrem atafariki dunia kwa maradhi
  • Watoto wote wa Hurrem watauwawa kwa makosa ya uasi na kubaki wawili tu; Selim 2 na Bayezid.
  • Sultan Suleiman ataugua na kufariki dunia. Selim 2 atamrithi.
Hiyo ni kwa mujibu wa Historia ninayoifahamu. Utawala wa 10 wa Suleyman pale Ottoman. Mfalme ambaye alibadili kanuni nyingi za utawala katika kipindi chake.

Sijajua Azam two watatufikisha wapi lakini angalau nimeona wanaingia mule mule. So, natoa fursa kwa wanaopenda kujua yajayo, waniulize maswali nami nitajibu kwa kadri ya kumbukumbu zangu.

Poleni team Hurrem na team Pasha in advance.


Mi ndo wala sijali, tena huwa ninaomba nistuliwe muda ukifika.Kuna watu hatunaga ukike au ukiume kwenye mambo ya kutengenezwa na binadamu.Eti nguo inatengenezwa na kuitwa hii ya kike na ile ya kiume.Kwenye mavazi kinachonizuia ni kanuni tu za kijamii na kitaasisi.Kwa mfano,kazini ninapangawa nivae nini,kwenye dini ninapangiwa nivae nini.

Mimi ninaheshimu masuala ya kibaiolojia tu, mfano, siwezi kulazimisha nibleed, siwez kuvaa ukikike kibaiolojia maana hii ni nature. Lakini nurture nyingi mimi ninaviolate.Hata marashi/uturi, nikinogewa na zile wanaita za kike natupia.

Natazama saaaana Sultan, machizi wangu ni Sumbla na Berbei(hawamuoneshi tangu atimue) dah!

Additionally, hadi leo ukienda Ankara, baadhi ya majengo ya wa-Ottoman yapo,mfano, ofisi ya Ibrahim Pasha, ipo na inatumika kama kivutio cha utalii.

Asante
 
Back
Top Bottom