LEGE
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 5,123
- 9,168
Kuna tabia imezuka ya watu kwenda na magari Mlimani City bila kuwa na shughuli maalum bali wao wamekuwa wanafika na kuyapaki tuu pale wanayatelekeza na wao wanaendelea na mizunguko yao jijini.
Na jioni wanapomaliza mizunguko yao wanapitia kuchukua magari na kuelekea majumbani kwao.
Na hii imegeuka tabia hasa kwa wakazi wanaotoka Mbezi, Kimara, Goba na Makongo juu na changanyikeni. watu hawa wamekuwa wakikatisha njia ya chuo au ya changanyikeni ya kwenda goba wanapita huku kukwepa foleni sasa wakishafika Mlimani City wanapaki magari yao na kuendelea na shughuli zao kama kuelekea maofisini au sehemu zao za biashara na jioni wanapitia kuchukua magari yao.
Kutokana na tabia hiyo, Mlimani City yanajengwa mageti ya kulipia amabayo ukiingia na gari yako utakuwa unalipia kutokana na mda utakaokuwa umepaki gari lako kama wanavyofanya uwanja wa ndege.
Na kwa upande wa geti la juu kama unatoka Ubungo tayari lishaanza kujengwa hivyo wadau kaeni mkao wa kujiandaa kulipia.