Mnaoenda na magari Mliman City jiandaeni kuyalipia

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Messages
5,091
Points
2,000

LEGE

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2011
5,091 2,000
Kuna tabia imezuka ya watu kwenda na magari Mlimani City bila kuwa na shughuli maalum bali wao wamekuwa wanafika na kuyapaki tuu pale wanayatelekeza na wao wanaendelea na mizunguko yao jijini.

Na jioni wanapomaliza mizunguko yao wanapitia kuchukua magari na kuelekea majumbani kwao.

Na hii imegeuka tabia hasa kwa wakazi wanaotoka Mbezi, Kimara, Goba na Makongo juu na changanyikeni. watu hawa wamekuwa wakikatisha njia ya chuo au ya changanyikeni ya kwenda goba wanapita huku kukwepa foleni sasa wakishafika Mlimani City wanapaki magari yao na kuendelea na shughuli zao kama kuelekea maofisini au sehemu zao za biashara na jioni wanapitia kuchukua magari yao.

Kutokana na tabia hiyo, Mlimani City yanajengwa mageti ya kulipia amabayo ukiingia na gari yako utakuwa unalipia kutokana na mda utakaokuwa umepaki gari lako kama wanavyofanya uwanja wa ndege.

Na kwa upande wa geti la juu kama unatoka Ubungo tayari lishaanza kujengwa hivyo wadau kaeni mkao wa kujiandaa kulipia.
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,090
Points
2,000

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,090 2,000
hizo mambo zipo marekani ukienda kanisani unaona magari mengi,ukiingia ndani hakuna watu wazee wachache tu kumbe watu wanapaki na kwenda mishe zao
 
Chagga King

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Messages
1,777
Points
2,000

Chagga King

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2011
1,777 2,000
...ila kwa kusema wakazi wa maeneo uliyoyataja ndo wenye tabia hizo si kweli, kwa reasoning ya kupita chuo kukwepa foleni ndo ukapaki gari mlimani city, labda ungesema watu wanaofanya kazi jirani na mlimani city, au watu wenye mishe maeneo hayo kama mwenge ingawa kimsingi tu, maeneo hayo hayana shida za parking. Wenye hayo mambo ni wauza sura tu wa mliman city ndo itawakomesha.
 
Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
52,998
Points
2,000

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
52,998 2,000
Mmh!!
Mwanzoni nilipoona ule ujenzi nikajua wanataka kuboresha ukaguzi wa magari uwe wa kielekroniki zaidi kujilinda na matishio ya kigaidi...

Ingawaje kuna mantiki katika hili lakini bado nahisi kuna mkono wa mtu kwenye kutaka kuvuna hela hapa...

Kwa nini wasiweke grace period, mathalani muda ambao mtu anatakiwa kupark gari pasipo kulipia iwe masaa mawili au matatu then anayezidi hapo ndio apewe tozo?
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,090
Points
2,000

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,090 2,000
Mmh!!
Mwanzoni nilipoona ule ujenzi nikajua wanataka kuboresha ukaguzi wa magari uwe wa kielekroniki zaidi kujilinda na matishio ya kigaidi...

Ingawaje kuna mantiki katika hili lakini bado nahisi kuna mkono wa mtu kwenye kutaka kuvuna hela hapa...

Kwa nini wasiweke grace period, mathalani muda ambao mtu anatakiwa kupark gari pasipo kulipia iwe masaa mawili au matatu then anayezidi hapo ndio apewe tozo?
wajanja washaona fursa apo kutengeneza pesa
 
MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Messages
1,942
Points
1,250

MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined May 27, 2013
1,942 1,250
wajanja washaona fursa apo kutengeneza pesa
Unajua mfanyabiashara cku zote anabuni namna gani ya kuvuna pesa. Wameona hiyo ni nafasi ya kupata pesa kwa kuleta hicho kisingizio, japokuwa hata mimi kitendo cha watu kwenda kupaki pale siku nzima mtu anaendelea na mishe zake sikipendi. Ila ni watu wachache wenye tabia hiyo. Wangeweka utaratibu wa mtu kupaki bure kwa muda fulani. akizidisha hapo ndo alipie, hii tungeona kuna busara imetumika
 
Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Messages
4,381
Points
2,000

Songambele

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2007
4,381 2,000
Ni ubunifu wa kijinga na kuongeza gharama za manunuzi bila sababu ya msingi kumbukeni quality free.
Kwa nini wasiweke mfumo wa kielectronic utakaoweka kumbukumbu ya muda na gari ili anayetelekeza tu ndio alipe.
Ubunifu wa namna ndio sababu wakenya amd etal wanatukwepa eac. Sie ni kuongeza vikwazo tu kila kukicha ktk biashara
 
georgeallen

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Messages
3,759
Points
1,225

georgeallen

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2011
3,759 1,225
Ni ubunifu wa kijinga na kuongeza gharama za manunuzi bila sababu ya msingi kumbukeni quality free.
Kwa nini wasiweke mfumo wa kielectronic utakaoweka kumbukumbu ya muda na gari ili anayetelekeza tu ndio alipe.
Ubunifu wa namna ndio sababu wakenya amd etal wanatukwepa eac. Sie ni kuongeza vikwazo tu kila kukicha ktk biashara
Serikali hii ya kingese ya awamu ya nne ndiyo imetia fora kwa kuongeza kodi za kero. Na hata zile kodi za kero ambazo serikali ya Raisi Mkapa ilizoziondoa hawa mafioso wamezirudisha.
 
Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Messages
4,071
Points
1,250

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2008
4,071 1,250
duh sasa sisi tunaoenda cinema kucheki movie tutakuwa tunalazimika kulipa muda mrefu kwa vile utapaki utaingia kucheki 2 to 3 hrs ndio unatoka tutakomaje
 
wehoodie

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2011
Messages
965
Points
1,000

wehoodie

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2011
965 1,000
sijawahi kuona shopping mall unalipia parking.....watakosa wateja sana
Kama umewahi kwenda shopping mall za nairobi haswa Sarit center (westland), west gate and junction mall....zote hizi unaswipe na unalipia kutokana na muda...free ni 15 mins only....hivyo sio sahihi kusema hakuna shopping mall za kulipia
 
CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
7,385
Points
0

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
7,385 0
Kuna tabia imezuka ya watu kwenda na magari Mlimani City bila kuwa na shughuli maalum bali wao wamekuwa wanafika na kuyapaki tuu pale wanayatelekeza na wao wanaendelea na mizunguko yao jijini.

Na jioni wanapomaliza mizunguko yao wanapitia kuchukua magari na kuelekea majumbani kwao.

Na hii imegeuka tabia hasa kwa wakazi wanaotoka Mbezi, Kimara, Goba na Makongo juu na changanyikeni. watu hawa wamekuwa wakikatisha njia ya chuo au ya changanyikeni ya kwenda goba wanapita huku kukwepa foleni sasa wakishafika Mlimani City wanapaki magari yao na kuendelea na shughuli zao kama kuelekea maofisini au sehemu zao za biashara na jioni wanapitia kuchukua magari yao.

Kutokana na tabia hiyo, Mlimani City yanajengwa mageti ya kulipia amabayo ukiingia na gari yako utakuwa unalipia kutokana na mda utakaokuwa umepaki gari lako kama wanavyofanya uwanja wa ndege.

Na kwa upande wa geti la juu kama unatoka Ubungo tayari lishaanza kujengwa hivyo wadau kaeni mkao wa kujiandaa kulipia.
hii nzuri, kikubwa usalama waimarishe!
 
Atukilia

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Messages
643
Points
195

Atukilia

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2009
643 195
Shopping malls nyingi duniani unalipia. Wewe subiri hata kupita highways unapaswa kulipia. Kadiri siku zinavyokwenda hata kuzika itabidi ulipie ada ya mwaka vinginevyo wanaondoa mwili. Nani anakumbuka hapa dar kuzoa taka si ilikuwa bure gari la manispaa linapita mtaani
 
Forum statistics

Threads 1,391,023
Members 528,344
Posts 34,070,642
Top