Mnaoenda kununua vitu Zanzibar na kuleta Bara kuweni makini, kodi yake si ya kitoto

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
Habari za wakati huu wapendwa,

Naomba niende moja kwa moja kwenye point ambayo itawagusa wale wenzangu na mimi ambao wanahabari kuwa Zanzibar vitu vya electronics ni bei nafuu sana,

Jana nilikuwa niko bandarini Zanzibar baada ya kutoka matembezi, nikiwa mitaani nilipitia maduka mbali mbali kuangalia bidhaa na bei zake. Kiukweli nilivutiwa sana na bei zake sema sikuwa na mchecheto wa kununua kwa jana

Wakati nipo kwenye meli kuna jirani yangu alikuwa amenunua runinga na microwave 2, inshort ni mbara na alienda kule kwa ajili ya manunuzi ya vitu hivyo tu tukawa tunapiga story za hapa na pale mpaka tukafika bandarini

Kilichonifanya niandike uzi huu ni baada ya kumuona yule jirani yangu kwa hasira akitupa ile tv na microwave kwenye bahari baada ya kuambiwa kuwa kodi yake ni laki 4, wakati yeye alinunua kwa matumizi tu ya nyumbani

Je hili linekaaaje? maana na mimi kama ningenunua hakika yangenikuta pia
 
Habari za wakati huu wapendwa,
naomba niende moja kwa moja kwenye point,point ambayo itawagusa wale wenzangu na mimi ambao,wanahabari kuwa zanzibar vitu vya electronics ni bei nafuu sana,
jana nilikuwa niko bandarini zanzibar baada ya kutoka matembezi,nikiwa mitaani nilipitia maduka mbali mbali kuangalia bidhaa na bei zake,kiukweli nilivutiwa sana na bei zake sema sikuwa na mchecheto wa kununua kwa jana,wakati nipo kwenye meli kuna jirani yangu alikuwa amenunua tv na microwave 2,inshort ni mbara na alienda kule kwa ajili ya manunuzi ya vitu hvyo tu tukawa tunapiga story za hapa na pale mpka tukafika bandarini,kilichonifanya niandike uzi huu ni baada ya kumuona yule jirani yangu kwa hasira akitupa ile tv na microwave kwenye bahari baada ya kuambiwa kuwa kodi yake ni laki 4,wakati yeye alinunua kwa matumizi tu ya nyumbani je hili linekaaaje? maana na mm kma ningenunua hakika yangenikuta pia
Zanzibar ni nchi yakhe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo vitu vyote kwa huko Zanzibar alivinunua kwa bei gani na kwa huku bara angevipata kwa bei gani? Kama hiyo tofauti ya bei ilikuwa ni saving kubwa kwake kuzidi hiyo laki nne ya ushuru bora angelipia tu kuliko kuchukulia hasira, kutupa vitu baharini na kupata hasara kubwa hivyo. Ila pamoja na yote hilo la ushuru kwa vitu vilivyonunuliwa sehemu ya "nchi ile ile" lingeangaliwa upya.
 
KUNA DHANA INAZUNGUMZIKA KAMA KIWANGO CHA KODI KWA ZANZIBAR KIKO CHINI KULIKO TANGANYIKA KWA HIYO UKINUNUA VIFAA ZANZIBAR UKIJA BARA LAZIMA UFIDIE ILE TOFAUTI YA KODI KAMA UNGELIPIA TANGANYIKA. ILA TRA WANGETOA ELIMU JUU YA HII KADHIA YA KODI YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA MANA TUNASUMBUKA SANA KWA VITU VIDOGO TV NA MICROWAVE KODI LAKI NNE SI AFADHALI ANGENUNUA HAPA?
 
KUNA DHANA INAZUNGUMZIKA KAMA KIWANGO CHA KODI KWA ZANZIBAR KIKO CHINI KULIKO TANGANYIKA KWA HIYO UKINUNUA VIFAA ZANZIBAR UKIJA BARA LAZIMA UFIDIE ILE TOFAUTI YA KODI KAMA UNGELIPIA TANGANYIKA. ILA TRA WANGETOA ELIMU JUU YA HII KADHIA YA KODI YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA MANA TUNASUMBUKA SANA KWA VITU VIDOGO TV NA MICROWAVE KODI LAKI NNE SI AFADHALI ANGENUNUA HAPA?
Hiyo tv ni aina gani na inch ngapi kwanza tuanzie hapo..
 
Back
Top Bottom