Mnaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) naomba kuwajulisha mnavyoweza kuiba au kuibiwa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Vijana wangu najua mnakwenda vyuo lakini hamtoki na maarifa mnatoka na vyeti. Kwani nasema mnatoka na vyeti, ni kwa sababu mnashindwa kutafsiri hata mkopo mnaopewa unatolewa kwa sheria gani na una masharti gani. Leo mhitimu wa chuo kikuu unamuuliza unadaiwa kiasi gani na bodi mkopo awezi kujibu, ulikopeshwa kiasi gani awezi kukokotoa, utalipa kwa masharti gani nayo shida. Huyu mtu ambaye hajui hata kusoma na kuelewa mkataba wa mkopo wake Mwenyewe tunampa ajira sehemu nyeti Serikalini atalinda maslahi ya Taifa?

Niache kuwalaumu, naomba niwasiadie mambo ya msingi kabisa yakufanya ikiwa umenufaika na mkopo wa elimu ya juu.

1. Unapohitimu chuo make sure una taarifa za mkopo kutoka kwenye chuo ulichosoma, taarifa hizo hifadhi kwenye jalada maalumu

2. Baada ya kuhitimu, nenda benk omba statement yako kwa kipindi chote unasoma ikionyesha lini uliingiziwa kiasi gani. Hii nayo weka kwenye jalada

3. Nenda bodi watake wakupe deni lako unalodaiwa (statement ya bodi).Weka kwenye file.

4. Chukua sheria na kanuni inayosimamia mkopo iweke kwenye jalada lako.

5. Kama umeajiriwa na umeanza kukatwa lingalisha taarifa zako za mkopo uliopewa na kile kinachosomeka kwenye salary slip kuona kama kinaoana, endapo kuna utofauti waandikie bodi wakupe ufafanuzi.

6. Kama ujaajiriwa soma sheria hasa kipengele cha penalties na utafute mbinu ya kukikwepa ikiwemo kuwaandikia bodi kuwajulisha ujaajiriwa na hivyo uwezi kulipa deni hii itakusaidia huko mbeleni.

Nimeandika haya mambo kwa sababu gani, vijana wengi wanaibiwa na vyuo pamoja na bodi ya mikopo kwa fedha kutoka na kuliwa na wahasibu bila wadaiwa kujua. Madeni mengi ya wanavyuo yaliyopo chuo, bodi, benki na hazina yanatofautiana hasa kwa mikopo iliyotolewa awamu ya nne na tano. Lakini pia madeni mengi yanayosomeka kwenye makaratasi yana penalties na adhabu zisizofaaa na zisizostahili.

Natambua wanafunzi na waajiriwa wengi wa Tanzania ni mambumbumbu kwenye eneo hili ila niwaombe kupitia uzi huu tuwalazimishe watendaji wa bodi na vyuo kutenda haki. Tuwaripoti walioiba TAKUKURU na wakati mwingine wanasheria chukueni hizi kesi mzipeleke mahakamani kudai fidia. Mkiwapelekea bodi wito wa mahakama au vyuo wataanza kupitia upya madeni ya wanufaika na kuachana na business as ussual
 
Wakati unasoma uliambiwa utakatwa 8% kila mwezi lakini anatokea kichaa mmoja anasema 15% hivyo hata ukijua haisaidii kitu uanaacha wakate mpaka wachoke.
 
Naomba ushaur nataka kuacha chuo kikuu niende diploma kwani garama zimekuwa kubwa na mkopo nimeopewa na bodi ni mdogo sana naomben ushaur wakuu
 
Ni kweli kabisa Kuna wizi unafanywa na wahasibu. Mimi sikuwahi kuchukua mkopo niliomba nilipoona haukidhi mahitaji sikuchukua hata senti moja. Mwezi wa 10 nilikuta deni katika mshahara la New Heslb
 
Back
Top Bottom