Mnaochochea migogoro chadema poleni sana na someni hii habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaochochea migogoro chadema poleni sana na someni hii habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 2, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  MKOA WA TABORA: Ngome mpya ya CHADEMA
  [​IMG]


  Joseph Senga


  MKOA wa Tabora ni moja ya mikoa ambayo ina historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanzania ambao pia umetoa vipaji vya nyanja mbalimbali.
  Lakini cha kushangaza leo hii ndio mkoa ambao umedumaa kwa kila nyanja ikiwemo kisiasa na kiuchumi; Mabadiliko ndio kwanza yanaanza kuwaingia wakazi wa mkoa huo.
  Kisiasa Tabora imekuwa ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kipindi kirefu sasa, kabla ya Chama cha Wananchi (CUF), kujaribu bila mafanikio kutaka kuiteka ngome hiyo kidogokidogo. Tabora ni mkoa ambao umetoa viongozi wengi kwa maana ya kuwa na mawaziri mahiri katika awamu zote.
  Tabora ndio viongozi wengi wamesoma akiwemo Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na wengine wengi. Unasifa kemkemu, lakini mabadiliko yalishindikana au wanasiasa wamewacheleshwa kuwapelekea ujumbe wa mabadiliko ya kisiasa ambayo yanazaa mabadiliko ya kiuchumi.
  Wanasiasa waliopita katika uongozi wa mkoa ule, iwe kupitia uteule wa serikalini au kuchaguliwa na wanachi wake, wameendelea kuwa na mazoea yale yale ya kuwaongoza wananchi ambao huenda na wao pia walizoea kuongozwa hivyo.
  Naamini wana Tabora walicheleweshewa kupelekewa ujumbe wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi. Kwa sababu ya mazoea ya wanasiasa, hata wale walioonekana kujaribu kuingiza ujumbe wa mabadiliko mkoani humo kama kina Profesa Ibrahim Lipumba na chama chake, bado waliona kama hakuhitajiki mabadiliko ya kweli kwa sababu ujumbe uliopelekwa ulikuwa ni vipande vipande haukuweza kufika kama inavyopasa.
  Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alifanya ziara ya siku saba ya kisiasa mkoani Tabora, ambako hata yeye alielezea kuwa aliwahi kusoma katika seminari ya Itaga.
  Ziara hiyo ilitoa picha kama wananchi wa mkoa huo walicheleweshwa kupelekewa ujumbe mahsusi wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.
  Kama uliamini kuwa Tabora bado ni ngome ya CCM kama zamani utakuwa unapotoka, huelewi. Wanatabora wamebadilika, wanahitaji mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kiuchumi.
  Ukitajiwa majina makubwa ya watu waliobobea kisiasa na kiuchumi ambao wamewahi kuwa viongozi wa mkoa huo na hata wanaoendelea kuwa viongozi wa sasa, unaweza kukata tamaa ya kuwasogelea wananchi wa mkoa huo kuwapa ujumbe wa mabadiliko; Bado ungeogopa majina ya wakubwa hao. CHADEMA, chama ambacho kimejizolea sifa na umaarufu miaka ya hivi karibuni, kupitia Katibu Mkuu wake, Dk. Slaa kimejaribu kupenyeza ujumbe wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika mkoa huo. Nilishuhudia. Wanatabora wameitikia, wamekipokea na kukiamini kuwa ndicho chama kinachoweza kurejesha hadhi ya mkoa huo.

  Dk. Slaa naye alijua ujumbe gani aupeleke kwao ili hatimaye wafanye maamuzi. Alizungumzia kero zinazowakabili wananchi wa Tabora licha ya kujaliwa neema na Mwenyezi mungu ya kuwa na raslimali lukuki ikiwemo ardhi nzuri.
  Hakuishia kuzungumzia tu kero hizo, bali pia alizitolea sababu nyingi zilizosababisha kuwepo kwa kero hizo; Kwamba mfumo mbaya wa uongozi wa CCM, uliodumu kwa miaka hamsini sasa ndio sababu kuu.
  Dk. Slaa na timu yake katika ziara hiyo walifumbua macho hata wale waliokuwa wamezoea kutawala kwa staili ileile, wameanza kunung’unika kuwa wamechokozwa kwenye kambi zao, hawajajua kuwa wananchi wa mkoa wa Tabora walikuwa tayari. Walikosa mtu wa kuwapelekea ujumbe murua ili kufikia mabadiliko yanayotakikana mapema.
  Leo hii ukiwauliza wananchi wa mkoa wa Tabora kuwa wanjivunia nini katika miaka takriban 50 ya uhuru wa nchi yao, licha ya kuwa kitovu cha kuzalisha viongozi, wanamichezo hodari na kutoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru, watakwambia neno moja tu, ‘tumekwama’. Wanataka kukwamuliwa, hawajui mpaka leo bei ya tumbaku yao wakati wanaivuna.
  Kisiasa hawana cha kujivunia licha ya kuwa na viongozi lukuki waliokalia madaraka kwa mika mingi wakiwemo akina marehemu Chifu Said Fundikira, Said Maswanya, marehemu Charles Kabeho na wengineo waliowahi kuwa mawaziri na sasa kina Profesa Juma Kapuya na Samwel Sitta.
  Hawana barabara hata moja ya lami inayoingia au kutoka makao makuu ya mkoa wa Tabota (mji wa Tabora). Hawana maji ya kutosha katika mji na vitongoji vyake.
  Dk. Slaa na timu yake waliyaeleza hayo na sababu zilizosababisha kuwepo kwa matatizo hayo wakati nchi inaelekea kusherehekea miaka 50 ya uhuru. Wananchi walielewa na sasa Tabora si ile ya juzi wala ya jana, wananchi wanataka mabadiliko na wamebadilika.
  Ni ukweli usiopingika kuwa, wingi wa watu wanaokusanyika kwenye mikutano ya hadhara ya Dk. Slaa na timu yake, ni dalili za kukiunga mkono chama hicho na kukubaliana nacho kwa kila jambo. Walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa ufasaha. Hawakujaa tu katika mikutano, pia walinunua kadi nyingi za CHADEMA hasa katika wilaya za Nzega, Igunga, Tabora na Urambo.
  Ziara ya Dk. Slaa na ujumbe wake uliowashirikisha vinara wakuu wa siasa nchini, akiwamo Mabere Marando, Profesa Abdallah Safari, Fred Mpendazoe na wakurugenzi mbali mbali wa chama hicho ilichukua siku saba katika wilaya za mkoa huo. Ziara hiyo ilihitimishwa katika Wilaya ya Igunga, jimbo la kada na mfanyabiashara maarufu wa CCM, Rostam Aziz.
  Ukisikia au kuambiwa kuwa hapa ni eneo linaloongozwa Rostam Aziz, Profesa Kapuya na Samwel Sitta, kama si mwanasiasa mahiri unaweza kukata tamaa kupeleka ujumbe wa kisiasa kabla hujafika katika eneo lenyewe. Kwani viongozi wa majimbo hayo ni watu maarufu sana kisiasa na wana uwezo mkubwa kiuchumi.
  Dk. Slaa na ujumbe wake ulilijua hilo, alitoa ujumbe wake kwa ustadi mkubwa na hatimaye aliweza kuwabadilisha wana wa Tabora; wengi wakawa wana CHADEMA, wakaahidi kumuunga mkono na kwamba hawatarudi nyuma tena.
  Ukiwa nje ya mkoa wa Tabora ni rahisi kufikiri kuwa wananchi wa mkoa huo hawamjui na pengine hawawezi hata kutamka neno Dk. Slaa. Hapana hali ilikuwa tofauti kabisa, wengi wanamjua Dk. Slaa na wanaijua CHADEMA. Walichokifanya ni kujiunga nayo rasmi baada ya CHADEMA kuwafikia moja kwa moja.
  Sehemu zote alizopita na ujumbe wake, wana wa Tabora walitaka kwa shauku kubwa kumuona na kumsikia; Waliziba njia kuzuia msafara wake ili azungumze japo kidogo.
  Maneno kama, “Yako wapi matendo mema ya CCM kwa wananchi”, yaliyotamkwa na Fred Mpendazoe wakati wa mikutano yaliwatia hamasa wananchi wa Tabora ya kuelewa nini maana ya mabadiliko.
  Licha ya kulalamikia sana kudidimia kwa uchumi wa mkoa huo ikiwemo kufa kwa reli ya kati, pia wana wa Tabora wanatakiwa wakumbuke kuwa, kuchagua viongozi kwa mazoea kunaweza kukawarudisha nyuma tena. Wakiyatupa waliyopewa na akina Dk. Slaa watajuta. Wajue haki haiji kwa kuletewa katika sahani, bali daima hupiganiwa. Tabora sasa naitazama kuwa ni ngome mpya ya CHADEMA, matokeo tutayaona.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Sikonge uko wapi?

  Habari njema sana kwa ile Kampeni yako ya Makao Makuu ya CDM kuwa Tabora.....Hii ni hatua ya kwanza kuchochea kampeni yako...

  Well bandugu ba Tabora, keep it rolling
   
 3. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila wazo linalotolewa na binadamu ni muhimu kutafakari na kulifanyia kazi.
   
 4. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  tupo pamoja sana wa TBR!Baada ya kikosi cha uhamasishaji, nyyuma yao kiwepo kikosi kwa ajili ya kutoa mafunzo juu ya falsafa, malengo na madhumuni ya chama.
   
Loading...