Mnaoamini Mungu, kwenye vichwa vyenu mna "imagine" sawa jinsi alivyo?

Nyie mnao amini uwepo wa Mungu, Wakristo na waislam, na madhehebu mengine Je kila mmoja wenu mnamaanisha Mungu Mmoja?

Yani unavyomfikiria wewe na mwezio ni hivyohivyo? Je unauhakika Kiongozi wako wa dini, Rafiki yako, na yeyote yule Jinsi anavyomuwaza huyu Mungu alivyo ndivyo unavyomuwaza wewe? Yani picha uliyojijengea kichwani mwako Jinsi alivyo, tabia zake ndivyo wenzio wanavyomuwaza hivyo? Kama mnatofautiana hatima yake nini?

Je huyu Mungu wenu alivyokusudia mumuwaze alivyo ndivyo ilivyo?
Je mpaka sasa unauhakika na dini yako ndio sahihi kumweleza huyo Mungu? Au tangu upokee kutoka kwa wazazi wako dini hiyo ndio umejidhihirisha wazi kwamba upo sahihi?

Je umejifunza dini nyingine kujihakikishia upo sahihi mpaka sasa kwamba Mungu anaikubali dini yako? na upo sahihi?

Je Ni biblia na quran ndio references kuthibitisha Mungu yupo, na jinsi alivyo?
Unajidhihirishaje kwamba vitabu hivyo si maandiko ya watu kwa utashi wao?

Je Maswali yangu hapo Unaweza kuyajibu????
kuna Mungu na mungu
 
Mm kabla sijapoteza muda na nguvu zangu kukujibu nahitaji kujua lengo ya kuuliza maswali hayo ni lipi??????
Maswali ulouliza hapo ni ya kawaida na haujaanza ww wapo waliokuwa kabla yako pia waliuliza na majibu pia hapo pamoja na dalili tosha kwa wenye akili.

Ila nikitambua lengo la muulizaji najua jibu lipi linamfaa kwa makusudio yake
 
Nadhani sihitaji kukupa tafsiri ya neno potofu kwamaana kwa umri wako nadhani wajua maana, kuhusu imani yangu ninauhakika sio potofu ila inamapungufu, kuhusu kujiridhisha sijui kujidhihirisha hilo ni la kiimani zaidi na kwa kuwa imani yangu haikuhusu hilo huna haja ya kulijua, kuhusu mimi kupotoka au la nishakujibu, sijapotoka kwamaana imani yangu sio potofu.
Kumbe waamini kwamba imani yako sio potofu, unajidhihirishaje ambae atajifunza imani nyingine kwamba atapotoka?
Kwanini isiwe anaujua ukweli au kupata iman nyingine kamili?

Pamoja na kwamba unaiamini imani yako, bado hujaweka sababu kwanini iwe hiyo isiwe ingine, kwa sababu zip
 
Uthibitisho wa kwanza kwamba Mungu yupo ni uwepo wako na uwezo wa kuhoji kwamba Mungu yupo au la. fikiria nguo iulize kama wapo washonaji au gari ya NISSAN iulize kama kampuni ya NISSAN ipo au la. Unatakiwa kijiangalia mwenyewe: ulitoka wapi, unaweza kujijua mwenyewe asilimia 100, unaweza tatua matatizo yote yanayokuja mbele zako?

Tafakari na mimi kitu kidogo: ulishawahi jiuliza kuhusu vyakula unavyokula, vilitoka wapi, kwa nini ukivila havikupi shida. Turudi kwa gari; gari inaenda kwa mafuta au gas au umeme, gari iliyotengenezwa iende kwa mafuta haiwezi kwenda kwa umeme. inamaana aliyebunu na kutengeneza gari alifanya hivyo akijua itaenda kwa kutumia nini tena bila shida.

Rafiki yangu na ndugu yangu kwako wewe ukila maharage ukashiba hushangai: nani alinibuni, akanitengeneza - haiyumkuni ndiye aliye buni na kutengeneza maharage. Sidhani kama UNAAMINI wewe na maharage mlikuja kwa bahati (chance) na kama ndivyo hiyo nayo ni DINI maana msingi wake ni imani tuu, nini tofauti na dini basi?
Hayo maswali yako ndio yanathibitisha mungu yupo?
Tatizo unaogopeshwa kiasi cha kujindwa ku-reasoning..
Kama mungu angekuwepo kusibgekuuwa na maswali
 
Binafsi naamini Mungu yupo, nami ni Mkristo Mkatoliki, Naamini hivyo kutokana na mambo mengi ambayo amenitendea na anazidi kunitendea. Kuhusu Imani zingine jinsi wanavyo imagine nadhani tunatofautiana, Mathalani Waislamu Wanaamini uwepo wa Mungu mmoja wakati Wakristo tunaamini ktk UTATU MTAKATIFU. Ndani ya Kanisa langu RC Naamini sote tuna mtazamo mmoja, japo siwezi Kuwa na uhakika wa asilimia mia.
Mambo gani umetendewa kiasi cha kuuamini mungu yupo?
 
'Science without religion is Lame and Religion without science is Blind'

Mkuu ukituacha sisi tunao amini katika Mungu, wewe una amini katika nini?
Siamini ktk chochote ambacho kinaitwa Mungu au shetan.
Naamini Mungu na shetan ni fikra zilizotengenezwa na binadam.
 
Kuna mambo ya kufanyia mzaha lakini si Mungu. Naomba mwenye enzi Mungu akurehemu. Mungu si wa size yetu, yuko kwenye level nyingine, malumbano kuhusu Mungu yupo au hayupo sidhani kama ni sahii sana. Wote tutakufa alafu tutajua kama yupo au hayupo, usiwe na haraka.
Mbona unapenda kunitisha?
Unajua km Mungu yupo hupaswi kunitisha, kwani mwisho wa siku si wewe wala mimi tutakufa, tena waweza tangulia ww
 
5adb806635b44afffe9d7d8c984dc554.jpg
Hayo ni maandishi, huwezi thibitisha ni ya Mungu!!
 
Mimi ninaamini katika Mungu, na Image yake ambayo naiweka Kichwani pale linapotajwa Jina la Mungu basi ninayo mimi mwenyewe.

Sasa basi so long as hii image ya Mungu iliyoko Kichwani sijawahi kumtajia binadamu yeyote yule awaye hivyo sina uhakika kama na yeye anafikiria Image kama mimi au nae ana Image yake, kwanza awali ya yote Image anayofikiria yeye huyo mwengine is none of my business.
 
Mm kabla sijapoteza muda na nguvu zangu kukujibu nahitaji kujua lengo ya kuuliza maswali hayo ni lipi??????
Maswali ulouliza hapo ni ya kawaida na haujaanza ww wapo waliokuwa kabla yako pia waliuliza na majibu pia hapo pamoja na dalili tosha kwa wenye akili
Ila nikitambua lengo la muulizaji najua jibu lipi linamfaa kwa makusudio yake
Lengo la maswali hayo ni kupata majibu.
Unasemaje?
 
Jibu maswali hapo juu, acha blaa blaa
Maswali ambayo hayana msingi halafu unataka tu ujibiwe.

Nimesema hapo kuwa wewe unauliza kama watu wote wanafikiria sawa juu ya kitu ambacho hawajawahi kukiona na wala hawana mfanano wake.

Sijui ulifikiria nini kabla ya kuuliza hili swali? na ndiyo maana nasema nyie watu mna stress.
 
Siamini ktk chochote ambacho kinaitwa Mungu au shetan.
Naamini Mungu na shetan ni fikra zilizotengenezwa na binadam.
Sasa mkuu kama unaamini kuwa Mungu na shetani ni fikra zilizotengenezwa unatakaje kujua kuwa tunao amini uwezo wa Mungu jinsi tunavyo mfikiria Mungu wote tunajenga picha moja?

Ulivyo kuwa mdogo uliwahi kucheza mchezo uliokuwa unahitaji kufikiria namba ukiwa na wenzako Kisha unaambiwa 'izidishe' 'itoe' 'ijumlishe' na namba fulani Kisha unapewa jibu?

Kama jibu ndiyo je wote mlikuwa mnafikiria jibu moja?
 
Maswali ambayo hayana msingi halafu unataka tu ujibiwe.

Nimesema hapo kuwa wewe unauliza kama watu wote wanafikiria sawa juu ya kitu ambacho hawajawahi kukiona na wala hawana mfanano wake.

Sijui ulifikiria nini kabla ya kuuliza hili swali? na ndiyo maana nasema nyie watu mna stress.
Kama hamjawahi kumwona na hamjui mfanano wake, vichwa vyenu v8namuwaza sawa? yeye anajua mnatofautiana kumuwaza?
 
Back
Top Bottom