Mnamkumbuka huyu mtoto wa jabu?

nhassall

Senior Member
Dec 17, 2010
195
41
Stori: Mwandishi Wetu, Songea

MTOTO wa ajabu aliyezaliwa hivi karibuni katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, amewasikitisha wengi huku baadhi wakisema hilo ni fundisho kwa wanawake wajawazito.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa, baadhi ya wananchi waliomshuhudia mtoto huyo ambaye sehemu zake za siri ziko kichwani walisema ni tukio la kusikitisha kuwahi kutokea lakini pia iwe ni somo kwa wanawake wajawazito kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mimi mwenyewe amenisikitisha sana huyu mtoto lakini kwa maelezo kuwa inaweza kuwa imesababishwa na mama yake kunywa dawa zisizostahili kabla ya mimba kutimiza miezi mitatu, basi iwe fundisho kwa wengine la sivyo matukio kama hata yataendeelea kutokea katika jamii zetu.

Pia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iangalie namna inavyoweza kumsaidia mtoto huyu kwani anateseka, alisema Mama Zuhura wa Songea mjini.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Mathayo Chanangula alisema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa na kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na uzito wa kilo 2.5.

Mtoto huyo kila anaponyonya, sehemu yake ya siri ya jinsi ya kiume iliyo kichwani kwake inasimama kama vile anataka kujisaidia haja ndogo.
Gazeti hili linamuombea kwa Mungu mtoto huyo afanyiwe linalowezekana ili arudi kwenye hali ya kawaida.
 

Attachments

  • MTOTO WA AJABU.JPG
    MTOTO WA AJABU.JPG
    19.5 KB · Views: 120
Mmhh duniani kuna mambo ya kusikitisha sana, vipi wataalamu wamesema hiiyoimesababishwa na nini? au nao hawajui?
 
Mmhh duniani kuna mambo ya kusikitisha sana, vipi wataalamu wamesema hiiyoimesababishwa na nini? au nao hawajui?

Mama yake inasadikika alikunywa dawa ambazo hakutakiwa kunywa wakati mimba ikiwa changa, na pia unywaji wa pombe na utumiaji wa madawa ya kuevya kupita kiasi wakati mimba ikiwa changa inaweza kusababbisha yote haya. Inategemea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom