zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,835
Habari wana Jamvi. Wataalamu wa vitabu vya dini wanasema mwanamke alitokea kwenye ubavu wa kushoto wa mwanaume katika uumbaji.
Ila tuachane na hayo kwanza walezi wakuu wa familia tunatambua kuwa ni wanawake na viongozi wakuu wa familia huwa ni wanaume hasa katika jamii zetu za Kiafrika.Lakini hili linatambulika na Dunia kwa ujumla.
Ila kwa siku za hivi karibuni wanawake wamekuwa wakipaza sauti na kudai uwepo wa haki sawa kati ya wanaume na wanawake(Gender Equality).Hii inamanisha haki sawa katika ugawaji wa kazi,fursa na ajira.
Kwa mfano siku chache zilizopita wanawake nchini Kenya wameibuka na kudai Kuwepo na idadi sawa ya wabunge bungeni yani nusu ya wabunge wawe wa kiume na nusu iliyobakia wawe wanawake(Gender Balance).
Takwimu zinaonesha kuna idadi(population) kubwa ya wanawake duniani kote ukilinganisha na idadi ya wanaume.
Ila kilio cha haki sawa hakijawahi kuisha kabisa licha ya idadi hiyo kubwa ya wanawake.
Wengine wamekuwa wakitoa mitazamo yao kuwa haiwezekani kabisa kuwepo kwa usawa(Gender Equality) kwa sababu ya mfumo dume wa nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania unaowafanya wanaume kuwa Superior zaidi ya Wanawake.
Wengine wamediriki kusema haiwezekani kwasababu ni asili ndio iko hivyo kuwa mwanamke siku zote atakuwa kiumbe dhaifu na atakuwa inferior kwa mwanaume.
Wengine wameamini kuwa hata maandiko yanalitambua hilo kuwa mwanamke atakuwa mtu wa kutii na atakuwa chini ya mume wake kwasababu ametoka katika ubavu wake wa kushoto.
Wanawake wanatumia nguvu kubwa kudai haki na usawa katika nyanja zote.Wakati jamii imeshindwa kuelewa tatizo liko wapi?
Mada hii ni pana sana Ila kwa kifupi tuanzie hapa
Kwanini wadai haki na usawa?
Je Hakuna haki na usawa Tanzania na Afrika Kwa ujumla?
Ni upi ushauri na mtazamo wako juu ya hili suala?