Nimekuwa nikifuatilia mechi nyingi hapa TZ hasa zile zinazoingiza mapato makubwa, hawa jamaa wamekuwa kero kabisa. Mara nyingi wamekuwa wakichelewa kutoa mapato ya mechi kwa madai kuwa ni pesa ilikuwa nyingi hivyo kuhesabu imechukua muda mrefu. Pili, majuzi wameitunishia misuli kamati ya kusimamia uwanja wa taifa eti wakitaka 50-50% mgao wa mechi dhidi ya indomitable lions. Jamaa hawa hawawezi kuwa na vyanzo vyao vya mapato? Mbona hatuisikii FA ya UK wakilalama ktk vyombo vya habari eti wamepata hasara kuendesha timu ya taifa? Wadau wa soka mnasemaje?