Mnalionaje hili la TFF kogombea mapato? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnalionaje hili la TFF kogombea mapato?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Orkesumet, Jun 28, 2008.

 1. O

  Orkesumet Member

  #1
  Jun 28, 2008
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nimekuwa nikifuatilia mechi nyingi hapa TZ hasa zile zinazoingiza mapato makubwa, hawa jamaa wamekuwa kero kabisa. Mara nyingi wamekuwa wakichelewa kutoa mapato ya mechi kwa madai kuwa ni pesa ilikuwa nyingi hivyo kuhesabu imechukua muda mrefu. Pili, majuzi wameitunishia misuli kamati ya kusimamia uwanja wa taifa eti wakitaka 50-50% mgao wa mechi dhidi ya indomitable lions. Jamaa hawa hawawezi kuwa na vyanzo vyao vya mapato? Mbona hatuisikii FA ya UK wakilalama ktk vyombo vya habari eti wamepata hasara kuendesha timu ya taifa? Wadau wa soka mnasemaje?
   
 2. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2008
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hasara ya kuendesha timu ya taifa inatoka wapi???Kwani zile pesa zinazotolewa na Serengeti pamoja NMB zinatumika vipi mbona udhamini ni mkubwa hiyo hasara inatoka wapi?? Hatuna viongozi wabunifu pale TFF
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  TFF inatia aibu kwa kweli sio tu kwa kugombania mapato hata kuwakata posho wachezaji kisa wamebadilishana jezi after mechi kuisha hili limenisikitisha sana
  Leo kwenye moja ya magazeti ya michezo nimeona wameandika "TFF - CANAVARO TURUDISHIE JEZI YETU ULIOMPA ETO'O hivi huu ni wakati wa kudaina jezi ya thamani ya pesa za kitanznia 15000/- kweli? wakati wafadhili kila mechi wanatoa MAMILION ya pesa hizo pesa za wafadhili zinafanya shughuli gani?
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  nahisi kuna mchezo mchafu wa pesa ndani ya TFF inabidi wachunguzwe....!!!, pesa za MAJI MASAFI,SERENGETI na NMB ambazo ni mabilioni zinafanya shughuli gani hadi waseme wanapata hasara bado kuna wadau wengine ambao huwa wanatoa michango yao midogomidogo timu iwapo kambini.
  Nahisi yule mdudu FISADI ameingia TFF
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mbona tunajua wanapiga panga sana hawa jamaa wa TFF akina Tenga,MWakalebela,Kaijage.
  Angalia mechi ya juzi na Cameroun eti wanasema zimeingia milioni 500 tu mmh kwa kweri haingii akilini wakitishiwa kuwa kutakuwa na TAKUKURU mapato yanaongezeka hawa jamaa wezi sana.Wamekula pesa kibao mechi ya juzi na Cameroun.
  Angali sasa wanalia na jezi aliyo pewa Etoo na beki wa Stars hii ni aibu jamani tena aibu sana tu.KUmbe jezi ipo moja tu ndo maana wanaililia.
  TFF wamejaa mafisadi tu ndo maana mpira wetu hauendelei kila mwaka kichwa cha mwendawazimu watu wanajaza matumbo yao tu mpaka utaifa wanauweka pembeni ili washibe wao.
   
 6. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2008
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Beki Nadir Haroub amekatwa posho ya shilingi 40,000 Zza kibongo kwa kitendo cha kumpa jezi Samwel Etoo,ambapo kitendo hicho ni kitendo cha mchezaji kutimiza kanuni za fair play za FIFA
  SHAME ON YOU TFF
   
 7. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ..TFF ya sasa bora hata FAT ya akina Ndoranga....sponsorship wanayopata sasa kwa timu ya taifa haijawahi kutokea katika historia ya soka Tanzania lakini kila siku wanatangaza njaa sijui wana matatizo gani?? Bora hata akina Ndoranga walikuwa wanahudumia taifa stars kimkandamkanda ilikuwa inaeleweka wako peke yao....Mapato wanapata makubwa lakini ndio hivyo tena migao imekuwa mingi sana...

  Na hili la kuwakata posho wachezaji eti kama amepoteza au amebadirishana jezi na mchezaji wa timu nyingine inaonesha ni jinsi gani TFF walivyo na maono finyo katika karne hii hilo ni jambo la kawaida tatizo wanaona jezi zikipungua watapa hasara....useless kabisa
   
 8. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  JAMANI Tshirt inauzwa 15000/- wanamkata elfu 40?? kweli huu ni uwonevu wa hali ya juu. Hii sio haki kabisa.

  Naomba ufafanuzi "Hivi jezi za Taifa stars nani ananunua ni TFF ama wadhamini?
  Kama ni TFF tangu timu ianze kuingia kambini hadi leo wanamenunua jezi pear 1? na kwanini waazimane jezi karne hii inamaana daktari wa timu hajui kama kuna magonjwa ya ngozi? kwanini nasema hivi kwenye gazeti wazedai kuwa jezi hiyo hutumiwa na mchezaji mwingine ambaye alikuwa yuko benchi siku ya mechi, NADHANI KUNA HAJA SASA JEZI ZETU ZIWE KAMA ZA MATAIFA MENGINE TIMU YA TAIFA KILA MCHEZAJI JEZI ATAKAYO VAA IWE NA JINA LAKE hii itasaidia kupunguza huu uwazimishanaji nguo
  yaani wanaishushia hadhi timu yetu ya taifa na kuiweka sawa na zile timu za mchangani maana wale wana jezi moja na baada ya mechi zinarudishwa na kupewa dobi afue.

  Nadhani kuna haya ya kuwachunguza personal account zao ili tuangalie tangu waingie madarakani ni hela kiasi gani zimeingia kwenye account zao na kutoka na tuangalie mshahara wao kwa mwezi je viwango tutakavyo vikuta kama haviendani na mshahara wake inabidi awajibishwe kwa kufukuzwa kazi na sheria ifuatwe.
  Hatuwezi kuvumilia ujinga huu wa watu wa chache wasiokuwa na uchungu na nchi yao.

  Tenga na kundi lake lote la TFF inabidi wawajibishwe
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  UWANJA WA TAIFA UNAINGIA WATU 60 ELFU.

  TUGAWE VIP 700@ 50000 = 35,000,000
  VIP (B) 800 @ 40000 = 32,000,000
  VITI VYA JUU KABISA 20000 @ 5000= 100,000,000
  VITI VINAVYOFUATIA 10000 @ 7000 = 70,000,000
  GOLI NA GOLI 10000 @ 10000= 100,000,000
  ORANGE 18500 @ 20000= 370,000,000

  HUU NI MFANO TU WA VIINGILIO VYA MECHI YA CAMERUNI SASA JUMLISHA MWENYEWE UONE MAPATO YALIO INGIA THEN TFF WANASEMA "ETI WANAPATA HASARA" HAYO NI MAPATO YA MECHI MOJA TU

  ie: green color ni idadi ya watu
  brown ni kiingilio
   
 10. c

  capuchino Member

  #10
  Jun 28, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakale Selo?????????????????????
   
Loading...