Mnalifahamu hili la maasai girls high school? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnalifahamu hili la maasai girls high school?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sipo, May 4, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nani anafahamu lolote kuhusu hii shule au ni uzushi tu wa mitaani wa kuharibiana sifa na kazi za wengine?
   
 2. K

  KASRI Member

  #2
  May 4, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh. Hii ndo TZ
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  1. Upendeleo na Ufisadi ndani ya kanisa ndugu yangu! Lol!

  2. Je yawezekana watoto wa Kimaasai hawataki kusoma hivyo Dayosisi ikaona nafasi hizi zisipotee bure?
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tungepewa majina ya wachache hawa wanaodhulumu sadaka ya Wamerkani.
  Quite sacrilegious!!!!!!!!!!!!!
   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bwana Mzalendo sio kweli kuwa WAMAASAI hawataki kusoma, ukumbuke kuwa hii ni jamii ambayo elimu kwa mtoto wa kike ni ya kulazimisha hasa kwa kipindi cha hapo nyuma, ukisema tu wanakataa wakati hujafanya capacity building yoyote ni sawa na kusema kwa sababu Watanzania wamekataa kuvaa CONDOMS basi tuwaache Wakenya na Waganda wavae peke yao. They were required to conduct the CAPACITY BUILDING kuwaonyesha akina BABA wakimaasai umuhimu wa elimu kwa MABINTI zao na sio kuwapa watu wenye uwezo wa kipesa nafasi hizo, angalau basi wangewapa wenye uwezo wa kiakili na sio kwenda kutuletea AIBU uko umangani kuwa watanzania ni VILAZA!!!
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwana Kijiji,

  Tafadhali hebu kapeleke ka-inzi kafuatilie na ikibidi kuwaambia hao watoa pesa kuwa huku mambo yamekaa kifisadi na ikibidi basi waje wafanye ufuatiliaji na kujua kulikoni.

  Shemeji yangu mmoja aliniambia kuwa kule Kilimanjaro, dada mmoja alikuwa ame-adopt mtoto masikini. Alikuwa akijinyima ili kumsaidia binti na akatafuta nauli kuja kumuona. Alipofika akakuta kumbe binti ni MTOTO WA MKURUGENZI na wanaishi mzinga wa jumba na maisha ya juu kuliko hata yeye anayoishi. Nasikia dada wa Kizungu alilia sana kujua kuwa ameingizwa mjini. Alikuwa akiishi kwa kujinyima ili kusaidia mtoto wa KIZITO.

  Huu ufisadi uko mwingi na kuna haja nao kuufichua. Naomba wenye magazeti na waandishi wa habari wafuatilie hili swala na kuwalima wote hata kama Maaskofu nao wanahusika basi walimwe.
   
 7. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Sehemu nzuri na rahisi kufanya kama kupitia ktk dini. Kuna tuhuma kuwa askofu wa kkkt dayosisi moja ya nyanda za juu kusini ili upate udhamini wa dini anayoiongoza ni lazima uwe na uke na ufanye naye balaa.

  Pamoja na hayo hii ndio BONGOLAND; Akili mukichwa
   
 8. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2009
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimelazimika kuchangia kidogo kutokana na kwamba hizi ni serious allegations na hilo la Concordia College naomba mleta mada uka research upya sources zako kwani hazina ukweli hata kidogo. Sio kweli Concordia College ndio mdhamini wa Maasae Girls Schools. Na kuhusu uongozi wa shule I can go back to when mke wa Bishop Laizer (Mary) akiwa mkuu wa shule hiyo. Hata hivyo alishinikizwa ku step down na wafadhili ambao ni makanisa ya kilutheri hapa Marekani kwa kutimia organization yao ya Operations Bootstrap inayoongozwa na mchungaji mstaafu Wayne Tellekson.
  Ni kweli kwamba kuna baadhi ya watoto waliokuwa wanasoma pale, sielewi kwa sasa hivi kwa sababu sipo nchini watoto ambao hawakutakiwa kuwepo pale kwani lengo la shule ya Maasae Girls lilikuwa kumkomboa msichana wa kutoka kwenye jamii ya/za ufugaji kwa kumpatia elimu kutokana na ukosefu wa resources kwenye mazingira aliyokulia.
  Sasa basi naomba nirudie swala la Concordia College Scholarships. Hiki chuo kilichopo Moorhead, Minnesota huwa kina provide two scholarships every year kwa best students. Concordia College hawana major ya u-daktari. Hiki ni chuo cha undergraduate. Ukitaka kusoma udktari ni lazima usome masomo ya Science na ufanye vizuri then u pass MCAT (Medical College Admission Test), halafu ndio uwe admitted kwenda Medical School.
  Medical school Marekani ni miaka depends on specialty ni wastani wa miaka 3, bado hujafanya residency ambayo ni miaka mingine 3 depends again on specialty. Kwa mfano ukisoma kuwa pediatrician ni miaka 3 na residency ni miaka 3. Ukiamua ku focus na kuwa neonatologist kuna mwaka mwingine wa residency hivyo kufanya miaka ya elimu ya udaktari kuwa 7.
  Sasa basi ukiweka na miaka ya undegradute on top of those 6 or seven years of medical school ni miaka 10, na almost $300,000 investment. Kwa nini Concordia College watumie kiasi hiki kikubwa kumsomesha mwanafunzi mmoja wakati wanaweza kuwasomesha wanafunzi 3 kwa miaka 4 ya elimu yao ya undergrad?

  Narudia tena Concordia hawana medical school. Na hawana mpango wa kusomesha au kusponsor watoto wanaokuja huku kwa hizi special scholarship zaidi ya undergraduate level. Wanafunzi wanao chose kuendelea either wanatafuta sponsors wao binafsi ama wanatafuta watu wa ku sign loans (co-signers) ili waweze kukopa kwenda shule.

  Vile vile ninawajua wasichana wote waliokuja kwa hizo scholarship. Sio kweli kwamba "wote" ni watoto wa vigogo. Watoto wa unaosema ni wa vigogo walikuwa wachache sana compared na watoto wanaotoka familia za kawaida. Kama ungetaka kuwa objective usingetumia neno "wengi" ungetumia neno "baadhi". Watoto 2 kati ya 10 haifanyi kuwa wengi. Umetumia wengi ili kui pamba story yako.
  Swali la maana hapa ni je kuna ufisadi Dayosis ya mkoa wa Arusha? No doubt. Kuna kiwingu kizito pale, lakini tunapotoa shutuma at least tuwe fair na sio biased.
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Capitol Hill,

  Unaonekana unatetea upendeleo ndugu yangu? hata akiwa mtoto mmoja tu wa kigogo wa dini: sii sahihi!

  Ufisadi ni ufisadi tu: hakuna cha unafuu!

  Hebu wawekwe majina yao hapa hao watoto wanaopendelewa!
   
 10. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2009
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapana, sitetei ufisadi. Ndio maana nikasema kwenye paragraph yangu mwishoni kabisa kuwa I have no doubt kwamba kuna ufisadi kwenye hii dayosisi, lakini pia nikaomba mkuu wetu aliyeleta hii habari aje na habari zenye uhakika zaidi ili tuwatendee haki watu wote.
  Mzalendohalisi, katika wasichana waliokuja na schorlaships za Concordia College ni binti mmoja tu aliyekuwa anasoma masomo ya Science na aliyekuwa na ndoto za ku persue udaktari hapa Marekani. Huyu amerudi nyumbani na alikwenda kufanya kazi Selian Hospital, right after alivyofika nchini.
  Ieleweke kwamba hakufeli, kwa sababu ali graduate na Bachelors yake May 2007, na hakurudishwa kama inavyodaiwa hapo mwanzoni. Alirudi kwa hiari yake mwenyewe.
  Na kama huyu binti ndio mkuu wetu aliyeleta hii mada anamzungumzia, basi ngoja ni m correct kidogo. Huyu binti si mtoto wa rafiki wa Bishop wa Arusha ila ni ndugu wa Bishop upande wa mke.
   
 11. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe. Capitoll Hill kwanza nianze kwa kukupongeza kuwa unafahamu mambo mengi sana kuhusiana na suala hili nililoliweka hapa mezani lijadiliwe. Lakini pia nikusahihishe kuwa sikuandika kuwa Concordia College ndio main sponsor wa Maasae Girls ila niliandika kuwa wanaprovide scholarships. Naomba nieleweke kwa hilo. Lakini kama ilivyo kwako kwa sasa siko nchini lakini nimetoa picha ya jumla ya nilichokifahamu kuhusiana na shule hii kwahiyo kama kuna mabadiliko basi hayana muda mrefu lakini ndio ninachokililia hapa ili wanaostahili wapate walicholetewa na wafadhili wao. Lakini pia niseme wewe umeanzisha mjadala mpya ndani ya mada yangu kuhusiana na ufisadi ndani ya dayosisi, mimi sijasema kuna ufisadi ila kama wewe unajua kuhusiana na hilo ulianzishie mada nyingine ila kwa sasa tujadili hili la MABINTI MSIKINI WA KIMAASAI WANAOKOSA NAFASI ZA MASOMO AMBAZO ZILIKUWA NI HAKI YAO YA KIMSINGI!!
   
 12. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli wapo baadhi ya watoto wa vigogo katika hii shule. lengo la awali lililotoa mwanya wa vigogo kuingiza watoto wao ni huu. Kwanza watoto walengwa wa jamii ya Maasai walikuwa wanatoka katika mazingira magumu mno, na waliruhusu wachache "waliostarabika" toka jamii ya Wamaasai waruhusiwe kujiunga hapo ili kuwasaidia kuwa-socialize hao wenzao. Nitoe mfano, maliwato zilizoko pale shule ni za kutumia maji, sasa unamtoa binti huko kwao hana habari hata ya choo cha shimo, unadhani inakuwaje? n.k, n.k. LENGO LILIKUWA ZURI, LKN MMBWA MWITU KATI YA KONDOO WAKATUMIA MWANYA HUO HUO.
   
 13. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mr. Capitol Hill, Taasisi ya Operation Bootstrap Africa (OBA) iliyopo Minnesota-siyo la dhehebu la Kilutheri bali ni interdenominational kwa ajili ya misaada ya kuwezesha mipango ya elimu katika Afrika.

  Pia ninavyofahamu Shule ya Maasae Girls huwa ina asilimia fulani ya watoto ambao sio wa wafugaji. Na ni gharama kuwapata watoto wa wafugaji ama wawindaji wenye nia ya kupenda kusoma.

  Pia katika hizi tuhuma tungepewa shule ina wasichana wangapi ambao wametoka katika familia zenye nafasi.
   
 14. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2009
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu unajua ni nani aliianzisha OBA? Ni yule babu Mchungaji David Simonson aliyekuja Tanzania kama Lutheran missionary volunteer miaka ya nyuma kabisa. Sikatai kwamba OBA ni interdenomination lakini nafikiri wanasema hivi ili wapate watoaji ambao sometimes ni non Lutherans.
  Obviously, una knowledge kubwa kuhusu hili suala na vile vile unaielewa OBA. Kwa mfano, ukiangalia board ya trustee ya OBA kuna Lutherans kibao. I know 3/4 of these people. Angalia mfano wa Tanzania. Ni shule au taasisi ngapi zinapewa misaada through OBA? Ngoja nikuhesabie. Kuna 1. Moringe Sokoine (Shule ya Kilutheri), 2. Maasae Girls (Lutheran) 3. Enaboishu Secondary (Lutheran), pia kuna Selian Hospital (Lutheran). Labda wewe mkuu unaweza kuwa na mfano wa shule inayopewa msaada ambayo haina ties na Lutheran Church. Kama ipo nitafurahi kujifunza.
  Angalia ni nani huku Marekani anachangia OBA either hela, equipment au supplies za mashuleni...ukiangalia utakuta ni makanisa ya kilutheri ya huku ndiyo yanayotoa hiyo misaada.

  Tukirudi kwenye debate yetu...umeongea point nzuri sana kuhusu hawa ma binti wanaotoka kwenye jamii za wafugaji. I remember back in the days, wale waalimu wa mwanzoni (Abby na Jane Tellekson) walikuwa wakienda Umasaini ku recruit wasichana wa kuwaleta shuleni lakini ilikuwa ngumu sana. Kuna baadhi ya situation ilibidi nguvu ya Serikali itumike kuwa force wazazi wawache watoto wao wa kike waje shuleni. Some of these girls wakati wa likizo had to stay in school kwa sababu wangerudi nyumbani wange olewa kwani some of them mahari ilikuwa imeshatolewa. Na wengine hated the place, hated the school kwa hiyo they would go home for likizo and come back pregnant. Kwa hiyo hizo ndizo challenges kwa haraka haraka walizopata wale early pioneers wa hii program katika kumuendeleza mtoto wa kike wa jamii ya kifugaji.
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe. Capitol nashukuru kwa mchango wako wa hali na mali, lakini sijui kwanini point ya msingi hapa unaikimbia kuwa hii shule imepambwa na watoto wa vigogo kwa asilimia kubwa kuliko wale waliolengwa na msaada wenyewe. Na pia kama lengo lilikuwa ni kuchukuwa baadhi ya waliostaarabika kama mwenyewe unavyosema, kwanini hao baadhi wakazidi wakawa wengi hata kuliko wale waliokusudiwa. Ingekuwa lengo langu ni kumchafua mtu ningetoa list ya vigogo ambao watoto wao walisoma pale au bado wanasoma pale. Lakini kwakuwa lengo langu ni kucorrect the situation ndio maana nataka tujadiliane ili wahusika wapunguze hali hii na walengwa wafaidike wa kiwango cha juu zaidi.
   
 16. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2009
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu sikimbii hoja yako, lakini naomba turudi kule kwenye tundiko langu la mwanzoni kwamba ili tuwe objective tunapotuhumu kuhusu ufisadi tuwe na FACTS na tusitumie "emotions" au maneno ya kusikia. Hii ni muhimu sana ili tuweze kuwatenda haki watu wote.
  Kama utasoma tundiko lako la kwanza ndugu yangu..umesema nakunukuu "kimsingi wasichana wanaosoma pale asilimia 75 sio watoto wa jamii ya KIMAASAI ambao wazazi au walezi wao hawana uwezo au hawana mwamko na suala zima la elimu kwa mtoto wa kike. Kimsingi watoto wengi wanaosoma pale ni watoto wa MATAJIRI wa mkoani Arusha na mikoa mingine ambao wana uwezo wa kuwasomesha watoto wao toka nursery hadi chuo kikuu kwenye private institutions."
  Haya maelezo yako mkuu wangu yana utata. Sikatai kwamba kuna watoto wanaosoma pale ambao hawakutakiwa ama hawatakiwi kusoma pale according to the mission ya shule. Lakini sio ukweli hata chembe kwamba 75% ni watoto wanaosoma pale au waliosoma pale at any given point tangia shule ilipoanza mwaka 1995 (the very first pre form one) hawakuwa "walengwa".
  Je kumekuwa na watoto wanaotoka familia zinazojiweza ambazo wazazi wao wangeweza kuwapeleka kwenye institutions nyingine na kuwalipia...No doubt. Pia sio kweli kwamba watoto wengi wanaosoma Maasae Girls ni wa matajiri. Swali ni hili what is wengi? Kama ni watoto 5 au 10 out of 200 je ni wengi?
  Ndio maana ukirudia post yangu ya mwanzoni nimesema tusilete data ambazo hazina ukweli ku support allegations zetu. What is wrong kuwa fair? Mimi nimekubali kuwa kuna mazingira ya ufisadi, na si i tetei Dayosisi, lakini kwa sababu ninaielewa program nzima na ninawajua stakeholders wake wengi, napinga baadhi ya vidhibiti vyako.
   
 17. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  Mhe. Capitol Hill mimi ni mtu ambaye napenda kusahihishwa sana hasa pale ninapoeleweshwa kwa undani na mtu ambaye ana uhakika na kile ambacho anakiongea. Kimsingi nakubaliana na hoja yako ya kuwa fair, something which is good anyway. Lakini nafikiri ni wakati wa kuungana pamoja na kupinga huu udhalimu unaofanywa na wenzetu tuliowaamini na kuwakabidhi majukumu ya kutuongoza sio serikalini tu bali pia kwenye taasisi za kibinasfi (NGOs) na hizi za kidini pia. Kwangu huu ni mwanzo tu wa kufichua jinsi misaada inavyotumika vibaya kwa kutokuwafikia walengwa. Na kwaa kutumia review mechanisims mbalimbali kama mtafiti kwenye maeneo mbalimbali nitakuwa nawaletea yale maeneo ambayo yatakuwa yanakera zaidi na kuwanyima watu wengi HAKI zao za kimsingi kama ilivyokusudiwa.
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Sipo

  safi ndugu: that is a good spirit we need in Tz today!

  Keep the spirit up!
   
 19. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Thanks my Senior!!
  Let us join together, together we can accomplish the task!!
   
 20. T

  Tsidekenu Senior Member

  #20
  May 7, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  yani hapo ndo ufisadi wenyewe kabisaaa. nilivyomuelewa mtoa mada ni kuwa hizo scholarship za first degree ndo haziwafikii walengwa wote. hata kama nafasi iliyoibwa akapewa mtoto wa kigogo tayari imedeny maskini mwingine kupata elimu ya chuo kikuu. halafu hvi mnadhani hawa mafisadi papa na nyangumi sijui na mafisadi tembo walianzanje????? leo nafasi moja kwa ndugu wa bishop, kesho katibu mkuu naye anataka housegirl wake apewe nafasi, mtondogoo parish worker nae anampigia pande nduguye, mwisho wa siku mlengwa hata mmoja hapati.
   
Loading...