Mnakumbuka Tendwa alisema hivi majuzi kwamba baada ya uchaguzi rallies za kisiasa hazina maana?

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Ndugu zangu hivi majuzi baada ya matukio mengi ya polisi kuzuia mikutano ya chadema na kusababaisha vurugu, tendwa aliibuka na kudai wanataka kuangalia upya sheria ya vyama vya siasa na mikutano ya hadhara hasa baada ya uchaguzi kwamba nini lengo la kufanya mikutano ya kisiasa baadaya uchaguzi. Kwamba uchaguzi ukiisha watu wasubirie uchaguzi mwingine ndio waanze kampeni za kujiimarisha.

Swali, je hii statement aliitoa tu kwa madhumuni ya kukandamiza vyama vya upinzani (chadema) au alikuwa anamaanisha? Je alikuwa anajua pia kwamba CCM itahitaji kufanya mikutano ya kuwaambia watu kwamba wanafanya vizuri kana kwamba watu wenyewe hawawezi kuona yanayofanywa kwa maana ya kupungua kwa ukali wao wa maisha?
 
Back
Top Bottom