Mnakumbuka filamu hizi za kihindi!!

Hebrew

JF-Expert Member
Jul 3, 2008
559
167
Mimi nilikuwa mpenzi sana wa picha za kihindi miaka ile ya 1980s.
Nakumbuka sana Majumba ya sinema ya Chox, Cameo, Avalon, Empire, Empress na Starlight ..wakati ule unalanguliwa ticketi kuona sinema kwenye haya maukumbi. Nawakilisha picha ninazokumbuka;

Naseeb ya Amitabh Bachchan
[ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Hum_Kisi_Se_Kum_Nahin"]Hum Kisi Se Kum[/ame] Nahin ya Rishi Kapoor
Qurbani ya Zenaat Aman na Feroz Khan
Disco Dancer ya Mithun Chakraborty
Nishaan ya Rekha na Jeetendra
Hum Se Hai Zamana ya Ranjeet

Nawakumbuka wengine kama kina Rekha, Amjad Khan (RIP), Ranjeet, Rishi na Rajiv Kapoor.
 
thannks Hebrew mie hizi picha nimekuja kuziona juzi juzi tu ila ni ndefu sana (nzuri )
 
Andha Khanoon...i dont remeber whor starred...by the way watu wanasema stering,stelingi sijui... badala ya starring..lugha bwana
 
Andha Khanoon...i dont remeber whor starred...by the way watu wanasema stering,stelingi sijui... badala ya starring..lugha bwana

Hii picha ya Amitabh na Amrish Puri niliiona kipindi sana..nakumbuka ilikuwa Cameo..
Si unajua Bongo miaka hiyo kila mtu anasema stelingi..Maluninga hayakuwepo mengi na watu waliokuwa wanasoma Daily News na Sunday news walikuwa wachache!! Watu tulikuwa tunangojea jumamosi tukapiganie magazeti ya Mfanyakazi!!
 
Love in Goa...I like the soundtrack.....lakini ile langua ya pale Empire ilikua balaa hasa siku za IDD
 
Love in Goa...I like the soundtrack.....lakini ile langua ya pale Empire ilikua balaa hasa siku za IDD

Hii nayo ilikuwa classic. Sikukuu na wikiendi ilikuwa lazima ulanguliwe tiketi...ndio ilikuwa ulaji wa watu wengine miaka ile
 
Love in Goa...I like the soundtrack.....lakini ile langua ya pale Empire ilikua balaa hasa siku za IDD

Juzi juzi tu nilikuwa naangalia hizi Video.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=uhozOgO1eiI[/ame]

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=z6RrbsjY6YY[/ame]
 
Hizi picha zilikuwa na stori nzuri sana ila kwa bahati mbaya tulikuwa hatujui kihindi
 
Mimi nilikuwa mpenzi sana wa picha za kihindi miaka ile ya 1980s.
Nakumbuka sana Majumba ya sinema ya Chox, Cameo, Avalon, Empire, Empress na Starlight ..wakati ule unalanguliwa ticketi kuona sinema kwenye haya maukumbi. Nawakilisha picha ninazokumbuka;

Naseeb ya Amitabh Bachchan
Hum Kisi Se Kum Nahin ya Rishi Kapoor
Qurbani ya Zenaat Aman na Feroz Khan
Disco Dancer ya Mithun Chakraborty
Nishaan ya Rekha na Jeetendra
Hum Se Hai Zamana ya Ranjeet

Nawakumbuka wengine kama kina Rekha, Amjad Khan (RIP), Ranjeet, Rishi na Rajiv Kapoor.

Nakumbuka darasa la pili jamaa alikuja toka Zoo (Mwanza) wakaingia kijijini sasa kila siku anatukusanya anatusimulia hizi movies hadi tunachelewa nyumbani - tulikuwa tunamwona kama star hivi wa hollywood
 
Cameo walikuwa wanaonyesha Sholay kila sunday i think more then five years.
Movie ilikuwa nzuri sana ile....mpaka leo naweza kuitazama tema....
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom