Mnakumbuka East African Airways? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnakumbuka East African Airways?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Boflo, Jun 20, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]

  Wadau hapo zamani za kale kulikuwa na shirika la ndege East African Airlines. Ilikuwa sehemu ya East African Community. Waliokuwa wanakmiliki ni Tanzania, Kenya na Uganda.

  Mwaka 1971, familia tulisafiri Mbeya hadi Dar na ndege ya East African Airways. Ilikuwa Prop Job kama ile kwenye picha ya kati kati. Tulikuwa tunatoka kijijini Manda kwa ndugu wa baba. Mkikaa kwenye kiti kama vile mnatazama hewani, halafu ilisha ruka ndo mnakuwa sawa. Ingawa nilikuwa na miaka saba nakumbuka waliwapa aibiria lunch box. Mwaka 1976 tulisafiri na ndege 727 Nairobi -Dar. Haikuwa mbaya. Pia tulisafiri na treni, lakini jamani zilikuwa safi na wenye wahudumu waliopenda kazi yao.

  Nakumbuka nikiwa Form One mwaka 1977, ghafla shirika hiyo ilivunjwa. Waliokuwa na mali (treni, ndege, mabasi) kwenye nchi yao ndo ilikuwa mali yao. Wakati ule damu ulikuwa mbaya kweli kati ya WaTanzania na WaKenya.

  Mwalimu shuleni alitusimulia hivi, waKenya walivizia siku ambayo ndege kubwa na nzuri zitakuwa zimetua pale Embakasi airport Nairobi, ndo wakazizoa na kuita Kenya Airways! Tanzania tuliambulia zile Fokker Friendships na ndege nyingine 737 ikawa Air Tanzania, halafu Uganda walikuwa wazembe eti walipata ndege moja tu! Ikawa Uganda Airways.

  Lakini jamani nakumbuka watu walikuwa na huzuni kubwa mno jumuiya ilivyovunjika. Mbaya zaidi watu wakawa wanyama. WaTanzania walifukuzwa Kenya kama mbwa. Hasa hao waliokuwa wanafanya kazi na East African community. Wengine walirudi Tanzania kwa mguu na begi moja!
  Wenye stori za wakati ule hebu mtupashe.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mimi nina kumbukumbu sana kuhusu hili ndiyo maana hii harufu ya EAC mpya na msukumo unaotolewa na Kenya unanikera sana. Yaani viongozi wetu hawajifunzi kutokana na historia kabisa, ndio ubaya wa kuwa ni viongozi myopic. Kuna wafanyakzi wa EAC waliohangaishwa na serikali yetu kuhusu mafao yao muda wote huo hadi mwaka jana; nina imani kuna waliokufa bila kupata mafao yao.
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ..Thank You for the Memory! Hizo Ndege zinayoangalia hewani kabla ya kuruka zilikuwa Dakota 9 na yalikuwa so rugged, mandege ya kazi kiasi cha kuweza kutua hata kwenye uwanja wa mpira! I dont think they are producing them anymore. halafu angalia kichekesho. Miaka mingi iliyopita kama anavyosema mkuu kulikuwa na schedule flights kwenda Mbeya moja ya miko muhimu sana kiuchumi, saa hizi kumekuchwa ndio tunaaza kukumbuka kujenga kiwanja cha ndege ambacho hata maendeleo yake hatuambiwi! Mungu Ibariki Tanzania.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa taarifa nilizo nazo kwenye deski langu Kiwanja cha Ndege cha Mbeya kinafunguliwa rasmi mwezi wa 11 mwaka huu, na kazi za finalization zimepamba moto sana huko sasa....Kwa ujumla mambo mengi ya kimaendeleo ya jamii na huduma yamekuwa na tendency ya kurudi nyuma ukilinganisha na miaka ya zamani!....Fikiria treni linakwama kwa miezi 6, huku wananchi wa huko wakikwama kabisa kimaendeleo, ambapo timu ya Brazil inapokelewa kwa gharama ya 3bn!...do we have people or the likes?
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Miaka hiyo hata sikumbuki maana hata kunusa aridhi ya dunia hii nilikuwa bado..ila hii habari imeniingia mpaka kwenye damu. PJ wewe unazifahamu habari hizi??
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  kwa habari hii kimaendeleo tumerudi nyuma....maana kama miaka ya 1970 kulikuwa na schedule za ndege kwenda mbeya na 2010 hakuna schedule basi maana yake ni kurudi nyuma.
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,485
  Trophy Points: 280
  Lakini sasa tumeanza kwenda mbele ila kuna matapeli wa kisiasa wanaumia roho sana.
   
 8. robert sendabishaka

  robert sendabishaka JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2017
  Joined: Dec 11, 2015
  Messages: 1,260
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  mjomba wangu zee #Buchanimanza pita hapa utuwekee mambo sawa. maana wewe ulikuwa kiongozi wa routes hizi kabla hujajiuzulu kuitikia wito wa kumtumikia Mungu.

  cc. #jessejohn
   
 9. stickvibration

  stickvibration JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2017
  Joined: Feb 7, 2017
  Messages: 1,744
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Kweli ukiwa mwongo usiwe msahaulifu... hapajawahi tokea mkoa wa Mbeya kukawa na airport miaka hio
  Na hata baada ya hilo shirika kuvunjika EAA lkn bado mkoa wa mbeya palikua hapana airport ya kutua ndege aina ya FOKER yenye kubeba abiria 20 hadi 30
  Palikua na small airport tu ya kutua vi ndege vidogo
   
 10. muhomakilo jr

  muhomakilo jr JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2017
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 10,128
  Likes Received: 3,230
  Trophy Points: 280
  Captain Mazula..aliiba ndege moja, kutoka huko Kenya na kuileta Tanzania.....R.I.P..Legends Mazula...
   
 11. g

  golden pride JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2017
  Joined: Oct 24, 2014
  Messages: 721
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 80
  Duh
   
 12. Omary Ndama

  Omary Ndama JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2017
  Joined: Apr 16, 2017
  Messages: 1,008
  Likes Received: 593
  Trophy Points: 280
  Tatizo lenu mbaya MTU anayewaelekeza njia nzuri zaidi ya kupita ili usije potea njia kama awali...kubalini kuelekezwa sio kila njia mpitayo ni sahihi nyny sio malaika...kama mnaakili mbona uchumi unaoza kila siku mngewasikiliza kina zitto dangote tungefika huku na bado tunazidi kudidimia kwa ubinafsi wenu...wahini kukubali kukosolewa msije kukubali tukiwa marehemu tayari
   
 13. mzado

  mzado JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2017
  Joined: Jan 12, 2014
  Messages: 807
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 180
  Heshima yako mkuu, inaonyesha ulikua wakishua haswa hahaha btw asante kwa kushare kumbukumbu nzuri kiukweli nmejifunza kitu kikubwa kuhusu EAC, pia imeniacha namaswali mengi
   
 14. M

  Mpemba Mimi JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2017
  Joined: Jul 6, 2013
  Messages: 317
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Ni kweli - Kenya walichukua ndege nyingi. Actually moja ya ndege - DC 9 - bado inafanya kazi mpaka sasa. Inamilikiwa na moja ya Kampuni binafsi ya ndege ya Kenya. Mimi niliipanda hiyo ndege miaka hiyo nikiwa mdogo; na nimeipanda tena sasa hivi - miaka hii kuanzia 2013 Mpaka 2016. Mpaka sasa iko inapiga kazi.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2017
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hivi Boflo alienda wapi?
   
 16. swahiba92

  swahiba92 JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2017
  Joined: Nov 12, 2016
  Messages: 1,485
  Likes Received: 1,493
  Trophy Points: 280
  mkuu hebu nipe kiundani ilikuwaje?
   
 17. Cloud Computing

  Cloud Computing JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2017
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Acha urongo wewe, kafanye utafiti vizuri.
   
 18. A

  Abel Mtambuki Member

  #18
  Oct 21, 2017
  Joined: Oct 7, 2017
  Messages: 19
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Tumebaki pia na AICC Arusha
   
Loading...