Mnakomaa kupata Tume Huru ya Uchaguzi, mnadhani itawaweka madarakani?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwa mujibu wa ibara ya 190 ya rasimu ya Katiba ya JMT iliyoundwa na tume ya Jaji warioba ni kuwa kutakuwa na tume huru.

Mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe saba wa tume watakuwa wanateuliwa na rais. Kama mwenyekiti akitoka bara,makamu atatoka Zanzibar vivyo hivyo makamu akitoka Zanzibar mwenyekiti atatoka bara.

Pia ibara ya 191 imeanisha kuwa kutakuwa na kamati ya uteuzi. Ambayo itachambua majina ya waliomba kisha kumpelekea rais na yeye atateua jina walilopitisha. Na kisha jina kurudishwa bungeni na kisha kuthibitishwa na bunge.

Je, hao wajumbe wa kamati ya uteuzi mnajua wanapatikana vipi? Hata kama nafasi za Ujaji zitakuwa ni za kuomba kisha kuteuliwa na rais mnajua watakuwa na mamlaka gani? Hawatakuwa na nasaba za kisiasa?

Hao wataoomba nafasi za kuingia tume huru ya uchaguzi mtakuwa na uhakika hawana nasaba za kisiasa?

My take; Kama mnataka kuingia madarakani ni bora mkajenga imani kwa wananchi kuwa nyie ni wanansiasa mnaofaa kwa kila namna. Maana hata ikipatikana hiyo mnayoita tume huru mtapigwa tu.
 
Kama upinzani ungekuwa hauna imani kwa wananchi msingehangaika kuharibu uchaguzi mkuu uliopita, mngeacha wananchi wajichagulie viongozi wanaowataka, hapo ndio mngejua CCM sio chama cha siasa tena, ni chama dola tu.
 
Huna hoja bwege wewe! Utadhani hauishi tanzania! Endelea tu kula maisha, siku wakikugeuka akili zitekuingia
Huja haja ya kutukana, jibu swali kisha toa ushahidi. Au zile picha za Kawe ndio ushahidi wako? Mpaka leo mwezi wa nne hujaenda mahakani?

Pia kumbuka mada ni tume huru,je utakutoa?
 
Watanzania kwa sasa tunataka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi! Tatizo liko wapi ikiendelea kushinda CCM katika mazingira ya uchaguzi huru na wa haki? Nyinyi kubalini tu uwepo wa hiyo Tume, lakini pia kuurejesha mchakato wa Katiba Mpya. Nyinyi si mnapendwa! Mmenunua ndege, mmeifanya nchi kuwa uchumi wa kati! Sasa hofu iko wapi?

Kinachotukera Watanzania wengi kiasi cha kutufanya kususia zoezi la upigaji wa kura, ni uwepo wa hiyo tume hovyo ya uchaguzi, mamlaka makubwa ya Rais kuingilia huo mchakato mzima wa uchaguzi, na uwepo wa wale nyau policcm wanao tumika kuwatisha wagombea wa upinzani, mawakala na pia wapiga kura.
 
Tume huru itakuwa msaada wa kupata madaraka kama mnavyokomaa?
 
Kwa mujibu wa ibara ya 190 ya rasimu ya katiba ya JMT iliyoundwa na tume ya Jaji warioba ni kuwa kutakuwa na tume huru.

Mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe saba wa tume watakuwa wanateuliwa na rais. Kama mwenyekiti akitoka bara,makamu atatoka Zanzibar vivyo hivyo makamu akitoka Zanzibar mwenyekiti atatoka bara.

Pia ibara ya 191 imeanisha kuwa kutakuwa na kamati ya uteuzi. Ambayo itachambua majina ya waliomba kisha kumpelekea rais na yeye atateua jina walilopitisha. Na kisha jina kurudishwa bungeni na kisha kuthibitishwa na bunge.

Je hao wajumbe wa kamati ya uteuzi mnajua wanapatikana vipi? Hata kama nafasi za Ujaji zitakuwa ni za kuomba kisha kuteuliwa na rais mnajua watakuwa na mamlaka gani? Hawatakuwa na nasaba za kisiasa?

Hao wataoomba nafasi za kuingia tume huru ya uchaguzi mtakuwa na uhakika hawana nasaba za kisiasa?

My take; Kama mnataka kuingia madarakani ni bora mkajenga imani kwa wananchi kuwa nyie ni wanansiasa mnaofaa kwa kila namna. Maana hata ikipatikana hiyo mnayoita tume huru mtapigwa tu.
Huna akili
 
Tume huru itakuwa msaada wa kupata madaraka kama mnavyokomaa?
Sasa mbona kama huelewi hivi! Tume Huru na Katiba Mpya havidaiwi na Chadema kwa ajili ya hayo madaraka mnayo yapigania nyinyi maccm kwa gharama yoyote ile! Hivi vitu viwili vinadaiwa na Watanzania.

Na lengo ni kutaka kuwepo na haki, uhuru na usawa katika Uhaguzi! Au unadhani Watanzania hawana akili kama mnavyodhani? Wana akili nyingi tu tena kuwazidi nyinyi na hayo matakataka yenu mnayo yaita Ma PhD!! Na wanajua fika hata upuuzi wenu wote mlio ufanya kwenye uchaguzi uliopita.

By the way, mimi ni Mtanzania tu Mpenda Haki na Mabadiliko ya kweli. Si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa. Ingawa siku zote siwezi kusema uongo ya kwamba SIIPENDI CCM kutoka moyoni.
 
Mkuu ukitaka kumjua ni wa aina gani angalia kwanza I'D yake ndiyo utaelewa anatoka wapi na kwanini anarohoja upuuzi kama huu
Jikite kwenye mada boss. Wewe mwenyewe Id yako inanuka harufu ya wala panya na watu.
 
Sasa mbona kama huelewi hivi! Tume Huru na Katiba Mpya havidaiwi na Chadema kwa ajili ya hayo madaraka mnayo yapigania nyinyi maccm kwa gharama yoyote ile! Hivi vitu viwili vinadaiwa na Watanzania.

Na lengo ni kutaka kuwepo na haki, uhuru na usawa katika Uhaguzi! Au unadhani Watanzania hawana akili kama mnavyodhani? Wana akili nyingi tu tena kuwazidi nyinyi na hayo matakataka yenu mnayo yaita Ma PhD!! Na wanajua fika hata upuuzi wenu wote mlio ufanya kwenye uchaguzi uliopita.

By the way, mimi ni Mtanzania tu Mpenda Haki na Mabadiliko ya kweli. Si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa. Ingawa siku zote siwezi kusema uongo ya kwamba SIIPENDI CCM kutoka moyoni.
Kwani mimi ni mwanaCcm? Mimi nashangaa kwa nini wewe na wanaCdm hoja yenu ya katiba mpya na tume mpya mnaikomalia huku mkidai kuwa matokeo mabaya uchaguzi 2020 ndio sababu ya kudai tume huru na katiba mpya. Je itawafikisha?
 
Back
Top Bottom