Mnajua Hoseah hakupiga kura kumchagua Rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnajua Hoseah hakupiga kura kumchagua Rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gamaya, Jan 10, 2011.

 1. g

  gamaya Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa za siri kutoka ndani ya TAKUKURU zinasema kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Edward gamaya Hoseah aliondoka nchini Tanzania tarehe 29 Oktoba 2010 kuelekea nchini CHINA kwa mapumziko binafsi ya wiki mmoja huku akijua kuwa tarehe 31 Oktoba 2010 ni siku ya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

  Hii inamaanisha kwamba Hoseah hakushiriki kumpigia kura ya urais bosi wake JK kwa ajili tuu ya kwenda mapumzikoni. Vilevile kwa kiongozi wa ngazi kama yake na wa chombo kama TAKUKURU ambacho kwenye uchaguzi huu uliopita kilikuwa ni mmojawapo ya mihimili iliyotakiwa kuwa macho wakati wote ili uchaguzi uwe huru na wa haki kukimbia nchi na kwenda mapumzikoni nje ya nchi, inatoa picha kwamba haiwezi kazi yake na hamuheshimu bosi wake JK.

  Ina maana kwake mapumziko ni zaidi ya uchaguzi wa Rais ambaye ni bosi wake?

  Ndugu waandishi wa habari mliopo humu jamvini twawaomba nendeni pale Upange PCCB house mkathibishe habari hii.
   
 2. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  alipiga kabla hajaondoka, si wapiga kura wote walipigia kwa ballot box kwi kwi kwi kwi kwi ...
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Msisahau ya kuwa Hosea nae ni binadamu wa kawaida kama alivyo mwingine yeyote, Watanzania wangapi hawakupiga kura?? why Hosea??? mi naomba tusiliweke suala hili kisiasa au kichonganishi. Tuna mambo mengi sana ya kujadili kwa manufaa ya Taifa hili changa.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,225
  Trophy Points: 280
  gamaya, kwanza karibu jf nimeona ndi post number 2.
  pili, kwa mtu kama Hosea, kusafiri sio jambo la siri mpaka uiite ni taarifa ya siri kuwa alikwenda mapumzikoni China. Yeye ni mtu wa juu mno mpka mapumsiko yake ni kama ya Obama, hivi kwa akili ya kawaida, Hosea akapumzikie China, aache kujipumzikia zake Marekani kwa mkewe na wanawe?, unless familia nzima ndio ilihamia China!. Wakuu wa ki-hosea hosea, hata wakienda mapumzikoni China, wako huko kwa kazi maalum, kama mkulu anavyopita ile njia yetu kwenda kujipumzikia mligotini kila wiki, mateso wanayoyapata wale polisi wetu, na usumbufu kwa watumiaji wa barabara husika, ni kazi maalum tosha, ukiachilia misusuru ya wale wanaokwenda kumshika mkono mapumzikoni ni kazi tosha na ndio mapumziko yenyewe.

  na mwisho, kutokupiga kura, sio kosa kisheria, wala kosa kiutendaji, hivyo hajafanya kosa lolote, haswa kwa kuzingatia anapanga kuikimbia nchi, hivyo ametumia muda huo kufanya utafiti makao yake ya ukimbizi yawe wapi kama ni Marekani kwenye familia au China kwenye cheap life. Kupiga kura ama kutokupiga, ni masuala binafsi ya mtu usiyageuze issue!.

  Mkuu Hosea, tunajua huwa unapita humu au vijana wako wanakuwekea mezani, usivijali hivi vimaneno vidogo vidogo vya uchonganishi kwenye blogs na magazeti mbalimbali, wewe endelea kuchapa kazi nzuri kama unavyochapa, mfano mzuri ni jinsi ulivyoitimiza ile ahadi yako ya kuishughulikia rushwa ya uchaguzi wa CCM, kwa hata baada ya kuwakamata baadhi ya watuhumiwa red handed na ushahidi unao, uchunguzi unaendelea na wengine wameshachaguliwa, huku waliohisiwa tuu kama kina Bashe walienguliwa!.

  Pia nichukue fursa hii kukupongeza, ile deal ya Richmond, uliosema kwa kamati ya Mwakiembe kuwa haina rushwa, was a clean deal, tumeithibitisha, its really a clean deal na waliotaka kuichafua na kuilazimisha serikali yetu kuvunja mikataba, ndio sasa inabidi washitakiwe kwa kuitia serikali yetu hasara.

  Heri ya Mwaka Mpya!.
   
 5. T

  The Future. Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mimi sikupiga, kwa sababu sikuwepo nyumbani
   
 6. m

  mzambia JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mhhh hii nayo kali ya kufungulia mwaka.
   
 7. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo wandugu mnamtetea au? ni sawa kabisa yeye kuwa nje ya nchi wakati wa kupiga kura? yaani kama mnaamini hivyo, basi kazi ipo.
   
 8. t

  tufikiri Senior Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Yaani kweli umekosa mabo ya msingi ya kuandika yanyohusu maslahi ya umma, unajadili taarifa ya Hosea kutompigia kura Kikwete. Hivi Hosea ni nani?na kura yake inatofauti gani na zile kura zadi ya mil.9 ambao hawakupiga?Jaribu kujadili mambo ya msingi.
   
 9. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kutopiga kura si kosa, isipokuwa aliyekupa ugali usipompigia kura nani mwingine utamthamini. Lakini si hosea tu aliyekuwa nje ya nchi ndio hakumpigia kikwete, yule diwani wa Arusha wa ccm si amesema hakumpigia kikwete. Wengi hata baadhi ya mawaziri wake hawakumchagua, kwani hilo hamlijui?
   
 10. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mi mwenyewe sikupiga kura, nliona itaibiwa nikaona ngoja nikae nayo tu! hahahahahaha! issue hapa kwa bwana mkubwa nnayo iona mimi ni kuwa absent wakati a big issue like election is going down, issue ambayo inaihusu sana ofisi yake, and yeye ni mtendaji mkuu. Anyway because dunia ni kijiji, maybe while on leave alikuwa reachable through net and cell phone incase of urgent matters ambazo they needed his attention. Vile vile kama sub-ordinates wake walijipanga vizuri, ilikuwa poa tu kwa yeye kusafiri.

  Mbona babake Riz1 anasafiri daily na jahazi linasonga tu? japo kiuchakachuaji?
   
Loading...