Mnaikumbuka Salamu hii shuleni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaikumbuka Salamu hii shuleni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Dec 6, 2008.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Je mnakumbuka vijana tulivyojengwa kimaadili kupitia salamu za darasani wakati mwalimu akiingia:

  " Siasa ya Ubaguzi wa Rangi ni Unyama...Shikamoo mwalimu". Je kuna haja ya kuja na salamu mpya hili kuelemisha kizazi hiki kuhusu mmomonyoko wa maadili Tanzania?

  Mfano kuna haja ya kurudisha hiyo salamu kwa kuibadilisha kidogo mfano:" siasa ya kunyanyapaa kikabila ni Unyama......."

  Naomba kuwakilisha Hoja.

  Shadow.
   
 2. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kulikuwepo na hii "ili tuendeleee tunahitaji vitu vinne watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora shikaaa mooo mwaaalimu"
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Lusajo, hiyo ilikuwa safi, tatizo ni kipi tulichokosa kati ya hivyo vitu vinne mpaka sasa miaka 44 bila maendeleo ya msingi kwa mfano hakuna maji safi, hospitali duni, umeme wenye kwikwi nyingi tu za kirichmond na Zimwi liitwalo Independent power supply? je ni uongozi mbovu? au tatizo liko kwetu wananchi?
   
 4. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yap ni hii hapa kaka UONGOZI MBOVI, kwa sababu watu wapoo, ardhi ipoo, ila viwili hakuna, siasa safi hakuna na uongozi bora hakuna na hivi viwili vinakwenda pamoja, yaani siasa ikiwa safi na uongozi utakuwa bora. I hope next Generation watamaliza hayo matatizo mawili.
   
 5. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Lusajo,

  Hiki kizazi kipya mbona ndo kinakuja na mambo ya ajabu ajabu kama vile arrogance na kujikweza na kulewa madaraka umeyaona kama ya kina mengi na waziri kijana. Badala ya hiyo damu changa na mpya kuleta faraja inakuja kuleta karaha. Si unaona kizazi kipya kimetoka na EPA na madudu mengine ya ajabu ajabu. Tuombe sana tupate viongozi patrotic kama Patrice Lumumba, Nyerere, au hata Mandela. Siasa za sasa bila kujali umri ni zile tunaita "Cosmetic Politics" hawana jipya hata ukiwapima kwenye mzani...jaribu kuchunguza pande zote.
   
 6. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna na hii nayo tulikuwa nayo sisi:
  Imaani ya Chama Yasema, Kila mtu Astahili Heshima, Shikamoo mwalimu...
   
 7. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2008
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kuna hii hapa ambayo tuliitumia;

  "NITASEMA KWELI DAIMA,
  FITINA KWANGU NI MWIKO,
  SHIKAMOO NDUGU MWALIMU"

  Hawa mafisadi hayo yote wameyasau ndio maana wana fitina katika kuhujumu uchumi wetu wananchi.
   
 8. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Unajua mafisadi walikuja na kuua MIIKO ya Uongozi. Si mnakumbuka ahadi za mwanatanu enzi hizo. Hafu hao mafisadi utafikiri awakuimba zile nyimbo za kuonyeshe allegency kwa nchi yetu na Bendera ya taifa? Si huwa wanaimba Mungu Ibariki. Kazi Kubeba misaafu na Kuapa kwa Imani za dini wakati ndani ya mioyo yao hawana hata chembe ya hofu ya Mungu.Bini yao ni matumbo yao, familia zao, wapambe wao, nyumba ndogo zao etc. Hivi tukiwaita hawa jamaa kwamba "hawana Dini" nao watapiga kelele? Vile viapo wanavyoapa huwa ni maigizo au just by default lazima wabebe vitabu vitakatifu?

  Naona kuna haja kumleta Ombudsman wa China alete hile adhabu ya wara rushwa....Mtanisamehe Human Rights Activists...Wabunge mnaubavu wa kuimport ile adhabu ya kichina?

  "Cosmetic politics" kule Dodomya hawawezi wale kuleta mabadiliko nchi hii
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Dec 7, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ...KILA SIKU ASUBUHI MASHULE YOTE TLIPANDISHA BENDERA YA TAIFA NA YA CHAMA [CHA MAPINDUZI]..KWA SALUTI...HUKU BENDI YA SHULE IKIPIGA...NILIKUWA MPIGA NGOMA KUBWA[MAPIGO SABA]...KILA SHULE ENZI HIZO ILIKUWA LAZIMA KUWA NA BENDI...[WAMEHARIBU SIKU HIZI..NASIKIA]

  BASI TULIKIMBIA MCHAKA MCHAKA ...BAADA YA HAPO GWARIDE..THEN TUNATOA KIAPO CHA UTIII..[KUMBUKENI SUPREMACY OF THE PARTY...]..

  TULIAPA HIVI.....

  KIAPO CHA CHIPUKIZI KIAPO[kiongozi wa gadi]

  KIAPOOO...[WOTE]


  WEWE NI NANI....[kiongozi]

  mimi CHIPUKIZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI ..

  NAKITUMIAKIA CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI...

  VIONGOZI WETU NI NANIII??? [kiongozi]

  NYERERE NA ABDUL JUMBE....[WOTE]

  [baadaye waliapa ..nyerere na mwinyi....then ikaja mwinyi na warioba..etc]

  MARA KWA MARAAAAA...MUNGU SAIDIA!

  .......Kweli malezi kipindi kile yalikuwa ya kijamaa.....lakini yalituunganisha!!

  sidhani kama watoto wa leo ukiwaambia waape kwa jina ..la KIKWETE NA KARUME...WATAKUBALI..!!..sio ajabu ukiwauliza viongozi wako ni nani???..wakakujibu.....KIKWETE NA MAFISADI.....[jokin]
   
 10. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi napendekeza salamu iwe hii
  "MAFISADI WOTE WANYONGWE"
  "SHKAMOO MWALIMU"
   
 11. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Hivi siku hizi wanatumia kibwagizo gani kabla ya salamu?
   
 12. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MAFISADI BILA TANZANIA INAWEZEKANA,VIONGOZI WAJINGA BILA TANZANIA INAWEZEKANA,Shkamooooo mwaalimu! Naona hii itakuwa njema
   
 13. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Philemon, Umenikumbusha mbali. Nami nilikuwa kwenye bendi ya shule ...basi nakumbuka tulivyokuwa tunawahi hiyo ngoma kubwa tulikuwa tuinaiita 'mdundo'.

  Kuna mtoto wa jamaa yangu anasoma hizi shule za kisasa " academia" kaja mbio yuko darasa la tano anasema " baba, baba, tumefundishwa wimbo mpya leo ...Tazama ramani utaona nchi nzuri..." nilishangaa sana nikasema mbona hayo mambo yalikuwa ya kawaida enzi kuimba patriotic song toka shule za 'vidudu' je ni kizazi kipya kinapotea njia au ndo mambo ya Generation X.
   
 14. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ahahahaah mzee hii imetulia. Natumaini waziri wa elimu anatusoma hapa. Mama Waziri 6, naomba uijadili hii kwenye 'cabinet meeting' jumatatu.
   
 15. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Ndio maanake mkuu.Si rahisi mafisadi na viongozi wabovu kuisha duniani.Lakini si lazima wawepo Tanzania.Ndio maana Tanzania bila hawa inawezekana!
   
 16. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu, Nakubalina na wewe... Vita hii mwisho wake ni ushindi kwa wananchi.suala la kujiuliza ni lini ushindi huo utapatikana?
   
 17. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tunaweza pia kuibadili kidogo ikawa hivi: - "Siasa ya kunyanyapaa kikabila na kidini ni Unyama ...."
   
 18. m

  mbele New Member

  #18
  Dec 8, 2008
  Joined: Dec 5, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na siku hizi tungeanza na salamu "ufisadi ni unyama shikamoo mwalimu.
   
 19. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  philemoni,,, mwana wa mikaeli,,,,wacha hiyo. Jamani wakati huo huko kijijini, mzee mmoja aliangukiwa na jiwe kisa wimbo wa taifa. Ile inaanza tu,,,,,, Mungu ibariki Tanzaniaaaaa,,, Mzee wa watu kaachia mawe aliyoyabeba akaangukiwa na jiwe lakini hakulia mpaka wimbo unaisha! Nakumbuka pale shuleni kwetu,,, pale aulizwe Gabriel Mkamba anakumbuka vizuri huyu,,, kaka mkuu wa shule,,, alikuwa kimbelemble sana siku hizo,,, yuko wapi sijui na manispaa gani huko dsm.

  Pamoja na viapo vyote lakini naamini kuwa hawa bongo fleva wetu hawajui hata waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania yetu. Labda Salamu itakayofuta:-
  MAFISADI TANZANIA WAFANYWEJE? labda sijui,,, nasema sijui,,,,
   
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mimi napendekeza kwamba hiwe " ufisadi na unyanyapaa kikabila na kidini ni unyama...shikamoo mwalimu"!!
   
Loading...