Mnaikumbuka hii ya Tundu Lissu? Ilikuwa ni session ya asubuhi. Risasi 16 ndani ya mwili wake ilikuwa zimlaze ndani ya futi sita!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Nilikuwa napitia archives ya YouTube, nikakutana na hii hotuba yenye maneno makali kwelikweli ya Tundu Lissu dhidi ya watawala.....

Ilikuwa ni Septemba, 2017 alipopata nafasi ya kuchangia azimio lililoingizwa na wabunge wa CCM ndani ya bunge kumpongeza Rais Magufuli....

Ni kuhusu zile kamati za uchunguzi za akina Prof. Osoro na Mruma kuhusu mikataba ya uchimbaji na sekta ya madini kwa ujumla....

Wakitegemea kuwa jamaa (TL) ataiabudu na kuisifia sanamu iitwayo "MEKO", mambo yalikuwa tofauti sana....

Jamaa alishusha nyundo za uhakika za kuuponda uamuzi huo wa Meko na kamati husika huku akitumia facts, takwimu na historia....

Hii iliwaudhi sana wanaCCM wa ndani na nje ya Bunge. Nadhani hii ndiyo ilichangia sana kuharakisha mission ya kumuua siku hiyo hiyo ambayo kwa uwezo wa Mungu Yehova, ili- fail vibaya.....

Kiukweli Bunge kukosa wabunge kama hawa is a big tragedy na sisi wafuatiliaji wa bunge tumekosa ladha nzuri ya bunge halisi....

Hebu mtazame na msikilize wewe mwenyewe ktk video hii hapa chini.....

Hiyo ya dakika 11 na sekunde 29 alichangia asubuhi na mchana akapigwa Risasi....!!

Hii
 
TL ni moja ya maajabu ya mungu,Tukio la September 7 ni dhahiri kuonyesha kwamba mungu yupo,16 risasi za SMG mwilini,kupoteza 90% ya damu,Siku mbili yupo comma lakini ali survive ,Big Up Kamanda Mbowe na timu nzima ya makamanda waliokuwa dodoma kwa support yenu.
 
..Zile taarifa ni kweli zilikuwa RUBBISH.

..na ndiyo maana tumeachana na madai ya usd 191 billion.

..pia hatujalipwa kishika uchumba cha usd 300 million.

..pia hatujaweza kuwashtaki Accacia popote pale.

..Accacia amerudia status yake ya miaka ya 90 ambapo waliingia nchini kama Barrick.

..na kwasababu ripoti zilikuwa dhaifu ndiyo maana Prof.Kabudi na timu yake walizidiwa ktk majadiliano kiasi cha Prof kukata tamaa na kujaribu kujiuzulu.

NB.

..Prof.Mruma na Prof.Ossoro walikuwepo kwenye timu iliyokuwa ikijadiliana na Barrick. Kama ripoti zao zilikuwa za kweli kwanini wameshindwa ku-deliver usd 191 billion walizosema tunawadai Accacia?
 
Kiukweli Bunge kukosa wabunge kama hawa is a big tragedy na sisi wafuatiliaji wa bunge tumekosa ladha nzuri ya bunge halisi....
Naunga mkono hoja

P
 
TL ni moja ya maajabu ya mungu,Tukio la September 7 ni dhahiri kuonyesha kwamba mungu yupo,16 risasi za SMG mwilini,kupoteza 90% ya damu,Siku mbili yupo comma lakini ali survive ,Big Up Kamanda Mbowe na timu nzima ya makamanda waliokuwa dodoma kwa support yenu.
Mungu yupo. Am a medical professional. Lakini Mungu yupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa napitia archives ya YouTube, nikakutana na hii hotuba yenye maneno makali kwelikweli ya Tundu Lissu dhidi ya watawala.....

Ilikuwa ni Septemba, 2017 alipopata nafasi ya kuchangia azimio lililoingizwa na wabunge wa CCM ndani ya bunge kumpongeza Rais Magufuli....

Ni kuhusu zile kamati za uchunguzi za akina Prof. Osoro na Mruma kuhusu mikataba ya uchimbaji na sekta ya madini kwa ujumla....

Wakitegemea kuwa jamaa (TL) ataiabudu na kuisifia sanamu iitwayo "MEKO", mambo yalikuwa tofauti sana....

Jamaa alishusha nyundo za uhakika za kuuponda uamuzi huo wa Meko na kamati husika huku akitumia facts, takwimu na historia....

Hii iliwaudhi sana wanaCCM wa ndani na nje ya Bunge. Nadhani hii ndiyo ilichangia sana kuharakisha mission ya kumuua siku hiyo hiyo ambayo kwa uwezo wa Mungu Yehova, ili- fail vibaya.....

Kiukweli Bunge kukosa wabunge kama hawa is a big tragedy na sisi wafuatiliaji wa bunge tumekosa ladha nzuri ya bunge halisi....

Hebu mtazame na msikilize wewe mwenyewe ktk video hii hapa chini.....
View attachment 1369164
View attachment 1369176
Hakika Mola Yu pamoja nae. Hakika Yu Hai Yu pamoja nasi. Jina la Bw Lihimidiwe Milele. AMEN.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona wengi hawajasikiliza vizuri clips zote mbili,tungelisikiliza kwa makini tungelia kwa jinsi tulivyo wa hovyo,tunatunga sheria zinazopingana zenyewe kwa ushabiki tu sijui tunakwenda wapi? na bado hao wanaotumulikia tunawafukuza bungeni,sijui baada ya 2020 nchi itakuwaje kama wapambe wa chama kimoja watajaa bungeni yaani MSIBA unalisubiri Taifa letu.
Pascal Mayalla
 
Tutapata wapi kifaa kama hiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya pili imekaa kizalendo mpaka machozi yanakaribia kutoka.

Hasa hapo mwishoni anapomalizia kwa kusema, "maneno yangu yanaweza kuwa makali Sana, lakini Nani hapa anayeweza kuniambia haya ninayoyasema hapa Ni ya uongo? Nani hapa anayeweza kusema haya yaliyofanyika Ni sahihi? Maangamizi ya bunge letu yanatokana na hiki kibwagizo pendwa kinachoitwa hati ya dhararura".

Aisee so touching.. hata bunge zima wakiwemo CCM walinyamaza kimya kutafakari uzito wa kauli ya TL

Ni miaka mingapi itapita kumpata mbunge wa namna hii Tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom