Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani aridhishwa na uwezo wa kijeshi wa Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani aridhishwa na uwezo wa kijeshi wa Tanzania.

jeshi(6).jpg

Majenerali na wakuu wa majeshi ya nchi kavu kutoka nchi za bara la Afrika walikutana Arusha kujadili changamoto za kiusalama katika nchi za Afrika wameshudia mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa na jeshi la nchi kavu la Tanzania yaliyofanyika katika eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli.

Miongoni mwa makamanda walioshuhudia mazoezi hayo ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani Jenerali Mark Milley na makamanda wengine ambao kwa muda wote walionyesha kushangazwa na uwezo mkubwa wa matumizi ya dhana za kisasa walionao askari wa Tanzania.

Wakizungumzia baada ya mazoezi hayo baadhi ya makamanda wa Jeshi la Tanzania waliwaeleza majenerali hao kuwa mafanikio na uwezo wa Jeshi la Tanzania ambalo limekuwa likisaidia nchi mbalimbali za Afrika ni nidhamu na umakini wa namna ya kuwapata vijana wenye sifa ya kuwa wanajeshi.

Majenerali na Makamanda wakuu wa majeshi ya nchi kavu kutoka nchi za Afrika wanatarajiwa kutoa mapendekezo yao ya nanma ya kudumisha usalama katika nchi za Afrika hapo kesho.

Chanzo : ITV
 
Kudos TPDF KUDOS!!!!
Najua huu UZI utaharibiwa na majuha wanajiita wazee wa MAJUU.
Wataanza kulinganisha na NAVY SEALS sasa hivi utadhani wamewahi hata kukiona kifaru kwa macho.
Wabongo wana akili kama za PAKA (Wanajisaidia kwenye Unga wakati wana njaa)
Mungu alisaidie Taifa.

Ila hata bila kutusifia huyu mzungu jeshi la TZ ni noma.
Hapa siongei ushabiki. Kuna siku nilikuwa natembea sehemu fulani tukakutana na Wanajeshi fulani wa Belgium walisema wamekuja kufanya special commando training bongo. Nikashangaa sana, wakathibitisha kwamba bongo wako vizuri saaana.

Mark my words UncleBen wewe utaona tu.
 
Unajua bana wazungu wanajua sana jinsi ya kututeka akili, kila mtu anapenda jeshi letu liwe imara zaidi, lakin hii inategemea pia na uchumi wetu. Percapita income ya chin ya dola 1000 ya yetu nchi yetu ni kielelezo tosha ya jinsi gani jeshi letu sio imara, kifupi kwa wasiolewa mambo ya economy ni kwamba hata jeshi letu lingekuwa imara vip kuna economic indicators ambazo zinaonesha sustainability ya huo uimara. Ni sawa na familia ambayo pato lake kwa mwaka halizid milion moja, halafu haina potential assets ikatokea mmoja wa wanafamilia akaugua kwa mwaka mzima amelazwa hospitali hii familia lazima ita suffer tu.
Sio kwamba siipendi nchi yangu, ila tusidanganyane kirahis rahis, sis bado sana.
Ukweli utabaki kuwa ukweli, mambo mazuri kila mtu anapenda kuyasikia, ila lazima tuwe wakweli.
 
Well said...uwezo wetu kuendesha vita ni mdogo,ujanja ujanja wa kizamani na helkopta zinazodondoka bila kutunguliwa na vindege vya zama za kale vya urusi
 
Sasa itv kwa akili za mchana kweupe walitegemea jamaa angesema kwamba wako mdebwedo????

ni lazima angesema hivyo tu.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Rais Kikwete aliwekeza sana sana kwenye JWTZ miaka yote 10, Dr. Magufuli asipuuze vyombo vya ulinzi hata kidogo. Bajeti ijayo 46% (2016/17) yote imepelekwa Wizara moja tu ya Ujenzi!
 
Back
Top Bottom