"Unaambiwa watakufanyia vituko mpaka uondoke"Kama upo busy na kushindwa kuwepo site Tafuta fundi mkuu muaminifu ndio solution ,ukitafuta mafundi njaa atakupiga balaa.
Dawa ya kutopigwa ni kuwepo site mafundi wakijenga.
Yaaan hii ndio kitu naitumia mimi hadi sasa kwenye ujenzi wangu...kila kitu nanunua mwenyewe na bagaini mwenyewe fundi analetewa vifaaa...navyo nampelekea kidogo vikipelea naongeza..sema changamoto yake ni kwamba utagharamikia usafiri mara kwa mara ila sio mbaya maana unacho okoa ni kikubwa kuliko usafiriHata wewe wakati unatafuta hela ya kujengea kuna sehemu lazima ulipiga. Iwe ni ofisini bas ulifanya upigaji kwa madokezo ya uwongo na mambo kama za milungula lazma zilihusika. Kama mfanyabiashara bas ulipiga kwa namna yako hukutoa risiti, ulizidisha beii...uliuza na kununua magendo. Maisha yako hivyo, usimbane sana fundi lazima atakuibia tuuu. Japo hutakiwi ku relax ukaibiwa vingi.
Kama unaanza kujenga nyumba anza kujenga fensi kwanza kudhibiti utoroshaji wa vitu kokoto, mawe, tofali mbao, na vingine
Halafu mambo za "Matirio" inatakiwa kwenda fronti wewe "kabageini" dukani kanunue mwenyewe, fundi akisema cement kumi leta 8, bati mita 460 weka 410, marumaru box 100 weka 70.. mbao 320 weka 250... gypsum board 150 weka mia; vitu vikipelea unaongezea.
Tunapenda sana kutumia kampuni ila hela ngumu...unakuta ujenzi unafanya hata miaka 5 ..ukipata unafanya hili ...kampuni si watataka hela yao yoteTengeneza BOQ lipa kampuni ya ujenzi watakukabidhi funguo nyumba ikiwa imekamilika.
Labda jiulize bank wanaibaje na pesa zote zipo kwenye hesabu na kuna wasomi nguli wa mahesabu?