Mnada wa TRA wa mtandaoni- Changamoto na maoni yangu

Asante.

1. Yard ya ubungo iko nyuma ya business park pale shekilango.

2. Magari yanayouzwa ni aina yote....used za japan na used za bongo ili mradi uwe linashikiliwa na tra na uwe umeshindwa kulipa cha zakayo au kwa sababu ingine.

3. Sizijui yard zote zilizoko dsm ila nafahamu baadha kwa majina tu....kuna kwa bakresa, icd mivinje nadhan....kwa ufupi sizijui zote.
Nina maswali kidogo kwako mkuu
1. Yard ya ubungo iko maeneo gani?
2. Magari yanayouzwa ni used kutoka Japan yaliyoshindwa kulipiwa bandarini au hata used bongo yapo ?
3. Kwa hapa Dar yard nyingine ya TRA iko wapi?
Jibu maswali yangu then issue ya Wambura niachie mimi
 
Yule wa TFF siku hizi simsikii,
Hahah yule alikuaga anapenda makesi kesi balaa,kitu kidogo tu anakimbilia mahakamani.

Sasa awamu hii wakampa ile kitu aliyokua anaitafuta,kapigwa likesi huko la uhujumu uchumi akakaa ndani kama miezi 8 ndo akatoka na akatakiwa kulipa fine ya mil 100,baada ya hapo mpk leo amekoma kupenda makesi nadhani hata barabara za karibu na mahakamani atakua anazipita kwa speed hataki hata kugeuka.
 
Wadau wa uchumi wa kati- nawasalimu.

Nianze kwa kutoa pongezi za dhati sana kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuanzisha mnada wa kuuza bidhaa mbalimbali mtandaoni ( Online Auction). Binafsi nimefaidika na huduma hii mara kadhaa. Kwa hakika hii ni moja ya hatua nzuri sana kwa TRA. Pongezi sana kwako Kamishna Mkuu na taasisi yote kwa ujumla.

Hata hvyo siku za karibuni nimeanza kupatwa na mashaka jinsi mnada unavyomalizika.

Kinachonitia mashaka ni muda wa mnada kuisha kabla ya wakati ulioainishwa kwenye mtandao. Mfano tarehe 12/10/2020 mnada ulifungwa dakika moja na sekunde karibu 40 kabla ya muda. Hii si sawa hata kidogo.

Jambo la mnada kuisha dakika moja au sekunde kadhaa kabla ya muda ni suala ambalo nimeliona mara kadhaa sio katika tarehe tajwa pekee.

Kinachotia shaka hapa ni kwamba, kufunga mnada kabla ya muda kunaweza kumaanisha kwamba watu wenye "connection" wanawasiliana na watu wa "IT" ndani ya TRA ambao kwa ujuzi flan flan ama wanazima network au wanasitisha mnada sekunde kadhaa kabla ya muda.....hii inapelekea mtu mwenye "connection" kushinda kabla ya kuisha mnada.....yaani yeye ndio anakuwa mtu wa mwisho wa kuweka dau.

Changamoto hii haikuwapo wakati mnada huu unaanza desemba mwaka jana. Kipindi cha nyuma mnada ulikuwa ukisemwa unaisha saa 3 kamili basi ni saa 3 kamili...sio kasoro wala nini.

Hii binafsi inanipa mashaka na pengine ni kiashiria cha janjajanja ndani ya mfumo wa mnada. Lakini pengine kuna maelezo ya kiufundi....ambayo yanaweza kuondoa mashaka haya.

Binafsi napendekeza Commission General TRA atupie jicho eneo hili. Tuwekane sawa. Fursa iwe sawa kwelikweli.

Changamoto ingine....ni swala la invoice za mtandaoni kukosa control number ya malipo. Yaani ukishinda mnada unaprint invoice unakwenda TRA- wao ndio wakupe control number. Nadhan timu ya ufundi TRA ilitizame hili jambo, invoice itoke ikiwa kamilifu ili mambo yaende kidigital kweli kweli.

Changamoto ingine ni swala la magari haya kuuzwa kabla ya kuwa na kibali cha ubora kutoka TBS. Yaani unanunua gari unalipa kila kitu kisha unaenda TBS walikague kama linafaa kuingia au kutumika nchini.

Hili swala la ukaguzi maanake ni kwamba kuna uwezekano ukanunua gari mnadani kisha TBS/NIT wakasema halifai kutumika TZ ikapelekea mteja kupata hasara.

Napendekeza kwamba, NIT/TBS wakakague mali zote zinazouzwa kisha gharama zao za ukaguzi zijumuishwe kwenye bei ya mnada....ili kuepuasha uwezekano wa mteja kupata hasara ikiwa mali aliyonunua haifai kutumika nchini.

Changamoto ingine....ambayo sijui ni ya TRA au TPA au nani. Ni swala la upigaji picha wa mali zinazouzwa hasa magari.

Kuna nyakati unaona picha hata unashangaa kama mpiga picha alikuwa ana nia ya kupiga picha au lah!!. Yaan picha zote zinaonesha eneo moja tu la gari.....ama matairi tu au pengine mbele tu nk.

Hili la picha linaambatana na taarifa zisizotosha kuhusu gari au kifaa kinachouzwa....mfano unakuta gari inauzwa ila haioneshi ni manual au auto, aina ya mafuta inayotumia, eneo ambalo gari ipo, ukubwa wa injin n.k. Nadhan hizi ni taarifa muhimu sana kwa mnunuzi. Tunaomba improvement eneo hili.

Changamoto nyingine ambayo nimeiona....ni swala la namna ya kumruhusu mtu mwingine (third party) kuchukua mali uliyokwisha kulipia kwa niaba yako.

Mfano nimeshinda na kulipia mali iliyoko Bukoba nami niko Mtwara....natumia utaratibu gan ili mtu mwingine aweze kuchukua hiyo mali kwa niaba yangu?

Nadhan hili haliko wazi sana....napendekeza liwekwe bayana sana ili tuweze kununua na mali popote TZ bila kulazimika kwenda kufanya clearence sisi binafsi.

Changamoto nyingine ya ziada ambayo sio ya TRA kama taasisi ....nadhan ni ya mtu binafsi, ni kuhusu utaratibu wa kukagua magari na bidhaa pale yard ya ubungo.

Pale ubungo...pana mlinzi anaitwa Wambura....huyu bwana ni mnyanyasaji wa wateja sana. Amejaa kiburi na kisirani sana. Yaani ukienda pale kukagua mali zinazouzwa hadi uruhusiwe ni shida sana.

Tunabembeleza sana kupata ruhusa ya kuingia yard ...kiasi kwamba inakuwa ni kama msaada kukagua mali wakati kanuni za mnada zinaruhusu kukagua mali kabla ya kununua.

Napendekeza kwamba huyu bwana ama afundishwe namna bora ya kuhudumia wateja au abadilishwe apelekwe eneo ambalo si lazima kukutana na wateja. Pia pawekwe ratiba maalumu ieleweke ni muda gani wateja wanaruhusiwa kuja kukagua mali badala ya kutegemea hekima ya walinzi.

Namaliza kwa kusema, licha ya changamoto zote tajwa hapo juu, bado mnada huu wa online ni bora mara 1000 zaidi ya kile kilichokuwa kinafanyika zamani.....kwa hili nawapa kongole sana.

Pamoja katika uchumi wa kati.
Nina maswali kidogo kwako mkuu
1. Yard ya ubungo iko maeneo gani?
2. Magari yanayouzwa ni used kutoka Japan yaliyoshindwa kulipiwa bandarini au hata used bongo yapo ?
3. Kwa hapa Dar yard nyingine ya TRA iko wapi?
Jibu maswali yangu then issue ya Wambura niachie mimi
Asante.

1. Yard ya ubungo iko nyuma ya business park pale shekilango.

2. Magari yanayouzwa ni aina yote....used za japan na used za bongo ili mradi uwe linashikiliwa na tra na uwe umeshindwa kulipa cha zakayo au kwa sababu ingine.

3. Sizijui yard zote zilizoko dsm ila nafahamu baadha kwa majina tu....kuna kwa bakresa, icd mivinje nadhan....kwa ufupi sizijui zote.
Shukrani
 
Hivi ili la TBS na NIT niliona wametoa tangazo kuwa kuanzia mwaka huu hawatahusika na gari zinazotoka Japan kitu kama iko na sehem ingine nmeisahau
 
Hivi ili la TBS na NIT niliona wametoa tangazo kuwa kuanzia mwaka huu hawatahusika na gari zinazotoka Japan kitu kama iko na sehem ingine nmeisahau
Ni kweli kabsa, kwa utaratibu wa sasa, ukishanunua gari unaenda polisi (baada ya kuitoa yard) upande wa usalama barabarani, wanafanya ukaguzi wa hali ya gari ikiwa ni pamoja na taarifa zake (namba ya chasis, engine nk) kisha unaenda TRA kufanyiwa usajili wa chombo chako.

Kwa hakika nawapa kongole sana TRA, TPA, POLICE, sijawahi kupata changamoto ya process ukiondoa changamoto ndogo ndogo za personalities za watu maofisini. Lakini kwa maana ya process, iko very perfect for me.
 
Kipindi naendelea kudadisi ili nishawishike kuingia kwenye mnada bwana mmoja akanambia kwamba TRA watataka pia zile kodi za kuingiza gari nchini hili la kweli? Na lingine kwamba bidhaa zinachaguliwa na wanaohitaji ndio zinawekwa katika mtandao.. hili sikumuamini.. ikoje kwa hapa.?
 
Jibu rahisi ni kwamba yote uliyoambiwa sio sahihi.

1. Mali inayouzwa mnadani...bei unayoona imewekwa ndiyo kila kitu...hakuna malipo ya ziada. Mfano kama bidhaa haina ushindani na inauzwa shilingi lak moja basi waweza kuongeza tsh 1 tu na ukawa umeshinda.

2. Bidhaa zinazouzwa pale mnadani maanake zimekidhi matakwa ya kisheria na kanuni za serikali za kunadisha bidhaa zilizokaa bandarini kwa muda mrefu.

Bila shaka umeelewa sasa. Shiriki mnada bila hofu ila la msingi ukishinda hakikisha unalipia bidhaa husika...vinginevyo unakuwa umetenda kosa kisheria na unaweza kushitakiwa mahakamani.

Karibu.
 
Asante boss
 
Wakuu habari
Naomba kuuliza hivi ukishinda mnada wa gari au pikipiki unaweza kumtuma mtu kukuchukulia? Vigezo ni vipi?
 
Yashauzwa mengi tu mapya...sina picha zake kwa sasa kwa sababu sikuzichukua.

Palikuwa na haya mapya kabsa...kwa maana ya used ya nje

1. Subaru foresta
2. Range rover
3. Pajero
4. Hyundai
5. Bmw.

Hizi baadhi ya gari zilizokuwapo quality na bei nzuri sana.

Over...out.!
Dah embu tupe na bei basi ilikiwaje kwa kila gari?? Kiufupi navutiwa sana ila sijui pakuanzia
 
Wakuu habari
Naomba kuuliza hivi ukishinda mnada wa gari au pikipiki unaweza kumtuma mtu kukuchukulia? Vigezo ni vipi?
Nimeona hii hapa
Screenshot_20230929-105659_Adobe%20Acrobat.jpg
 
Wakuu habari vp...
Me naomba kuuliza ni nini kinatokea kwenye mnada unapokua unaendelea pale TRA ONLINE AUCTION. Maana oktoba tano nimeshiriki mnada wa gari kama mbili hivi lakin kina wadau wakanizidi gap mbali sana nikajua ndo washindi hapo sina changu.. mnadq ukaisha muda wake.. cha kishangaza leo mnada umerudi tena nmeona karibia gari 3 zimerudi mnadani shida inakua ni nini?
View attachment 2777068View attachment 2777069View attachment 2777070
 
Back
Top Bottom