Mnada mali za Makamu wa Rais Equatorial Guinea, Teodoro Nguema: Urais Afrika ni mtamu kwa marais kama hawa

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,157
2,000
Serikali nyingi katika bara letu ni vikundi vya wahuni/wajanja wachache wanaowakamua wanyonge kwa manufaa yao binafsi kupitia kodi. Ila pia wanawakamua wazungu kupitia misaada wanayotoa kwa mataifa ya bara hili.
Mali asili zote na vivutio vya utalii ni vitega uchumi vyao binafsi.
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,576
2,000
Tishio la uviko kwenye hiyo nchi ni kubwa kiasi hicho hadi mpunga wote wauelekeze kwenye chanjo?

Kama hao wananchi tunaambiwa ni masikini na wana hali ngumu, hawana mahitaji mengine ya muhimu zaidi yanatakiwa kwa sasa kuwanusuru kuwapa wepezi na ahueni ya maisha?

Kama sie tumepewa mkopo/ msaada kwa ajili ya chanjo za uviko, huo msaada usingetumika kwa hao jamaa pia?

Hao wazungu nao wanaweza kuwa wezi vilevile sema wametofautiana mbinu tu.
Mkuu the Monk huko sahihi. Unajua Rais wa Cameroon, Paul Biya, pamoja na Rais wa Gabon Ali Bongo na Rais wa Equatorial Guinea Obiang wote ni kabila moja ila nchi tofauti iliyogawanywa na mipaka na hawa wazungu.

Ndio Obiang na familia yake ni wezi kosa walilofanya ni kutaka kuingia mkataba na kampuni ya kirusi kuchimba mafuta ndo maana yote haya yanatokea. Kumbuka Obiang alienda kula bata Moldavia ya upande wa urusi ilikuwa pia kujenga uhusiano na makamu I ya Urusi.

Jiulize kwa nini Paul Biya hawamuwekei vikwazo wakati binti yake anamali za kutisha Marekani na ulaya. Juzi wakameroun walililamika binti ya Biya new York analipa Teksi dollar za Marekani 2000 umbali wa kilomita moja hadi Teksi driver flani mzungu a kataa hela nakumpeleka polisi?

Paul Biya mda mwingi kwa mwaka haishi Cameron lakini anaishi uswisi hotelini na kwa siku analipa dollar elfu kumi.

Ukija Gabon washaimaliza Gabon kwishaa. Aliyekuwa rais wa ufaransa Jacque Chirac aliisafisha kabisa Gabon yeye na marehem Omar Bongo.

Familia ya Paul Biya Cameroun na Omar Bongo wenyewe hawajaweka vikwazo kwasababu ni vibaraka wa Ufaransa Uingereza na Marekani. Lakini ndugu yao kuroka kabila moja tuseme wamasai wa Kenya na Tanzania au wakuria wa Kenya na Tanzania tatizo lao ni kutaka kumgawia Urusi mikata ya kuchimba mafuta.

Sepo Blatter aliyekuwa Rais wa Fifa angekuwa Rais hadi leo kosa alofanya ni kuipigania Urusi hadi kuwaandaa na kuwa mwenyeji wa world cup 2018
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,576
2,000
Huo ukanda wa Africa ya kati Congo zote mbili, Gabon, Central Africa Republic Cameroon na Equatorial Guinea kuna mali na madini mengi ya kutisha. Ukiondoa madini kuna misitu ya hatarii na ardhi nzuri kwa kilimo.

Makampuni mengi ya ulaya yamewekeza huku na wana influence kubwa sana na wanasiasa kwa kuwa Linda. Viongozi wao wengi ni wezi wakubwa ambao wana kula na haya Makampuni ya Magharibi.

Mfano Paul Biya kajaza serikalini na jeshini watu wa kabila lake. Marais wote wa hizi nchi wana jeshi ndani ya jeshi la nchi.

Obiang alikuwa anaiba vizuri tu wa Magharibi tatizo alivyoanza uhusiano na Putin lakini ajachelewa vyanzo vinadai ameshamkana sasa hivi Putin huenda wakamsamehe
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
19,862
2,000
Watawala wa kiafrica ni wezi, mafisadi,wauaji, washirikina,wazinzi.Ni Afrika pekee ndipo unaweza fanya case study ya bad leaders.
Wameshindwa kuwaletea waafrika maendeleo wamejifichia kwenye lawama za kuwalaumu wengine juu ya matatizo yaliyosababishwa na wao.Kwao ni fahari kutibiwa,kusomesha ulaya,
Kila siku wanasingizia mabeberu Hata siku moja huwezi kuwasikia wakitoa mfano wa Rais bora. Utasikia wanamsifia Putin na china.

Ni washenzi woote kasiro Kenyata na Hakainde
 
Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
4,398
2,000
hujui tu mkuu.wakoloni ndo wakulaumiwa kuja kutuingiliamaisha yetu na utamaduni wetu!! zamani babu zetu waliishi Kama jamii moja yenye upendo na kushirikiana,walikuwa na Sheria pia kusimamia maisha na usalama wa watu wao,maisha yalikuwa muurua kabisaaa,unaoa hata wake 2,au 3 safiii kabisa,na wote wanakuwa na upendo mmoja.wazungu wakaja wakaleta tamaduni zao,wakatufundisha kujipenda ,na kula bata,huku wakitukarilisha upuuz vchani mwetu,ili baadae wakiondoka na kutuacha bado wachote kiulaini Mali zetu.matokeo yake ndo hayo sasa.wakulaumiwa ni mkoloni.

Unaoita upuuzi ndio hadi leo unatumia kuanzia elimi yao hadi teknolojia yao
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,696
2,000
Afrika itakuwa na maendeleo siku watawala wa kiafrica watakapoishia jela,Kinga ya kutokushtakiwa ni ruhusa ya kutenda uovu
 
Trillion

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
2,642
2,000
Tishio la uviko kwenye hiyo nchi ni kubwa kiasi hicho hadi mpunga wote wauelekeze kwenye chanjo?

Kama hao wananchi tunaambiwa ni masikini na wana hali ngumu, hawana mahitaji mengine ya muhimu zaidi yanatakiwa kwa sasa kuwanusuru kuwapa wepezi na ahueni ya maisha?

Kama sie tumepewa mkopo/ msaada kwa ajili ya chanjo za uviko, huo msaada usingetumika kwa hao jamaa pia?

Hao wazungu nao wanaweza kuwa wezi vilevile sema wametofautiana mbinu tu.
Si anasaidiwa asiekuwa na hela mkuu, hao watu wana hela inachezewa na watawala , ni sawa tu irudi kwa mahitaji ya chanjo.
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,696
2,000
Mimi huwa nasema hata kansa katoliki kuwa strong vile ni kwa sababu viongozi wa juu duniani ni wazungu. Siku papa atakapokuwa mwafrika basi kanisa kwishney.
Kanisa katoliki ni strong sababu ya mifumo yake strong ya uongozi.
Watawala wa kiafrica wapo kama wapangaji awafikirii future ya waafrika zaidi ya familia zao.
Angalau kidogo nchi za afrika ya kaskazini ya waarabu hawa wanayaona matunda ya UHURU na kilichowasaidia ni mfumo wa dini ya kiislamu,hii angalau mtawala na mtawala wote ni daraja moja ktk imani.
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,420
2,000
Mkuu the Monk huko sahihi. Unajua Rais wa Cameroon, Paul Biya, pamoja na Rais wa Gabon Ali Bongo na Rais wa Equatorial Guinea Obiang wote ni kabila moja ila nchi tofauti iliyogawanywa na mipaka na hawa wazungu.

Ndio Obiang na familia yake ni wezi kosa walilofanya ni kutaka kuingia mkataba na kampuni ya kirusi kuchimba mafuta ndo maana yote haya yanatokea. Kumbuka Obiang alienda kula bata Moldavia ya upande wa urusi ilikuwa pia kujenga uhusiano na makamu I ya Urusi.

Jiulize kwa nini Paul Biya hawamuwekei vikwazo wakati binti yake anamali za kutisha Marekani na ulaya. Juzi wakameroun walililamika binti ya Biya new York analipa Teksi dollar za Marekani 2000 umbali wa kilomita moja hadi Teksi driver flani mzungu a kataa hela nakumpeleka polisi?

Paul Biya mda mwingi kwa mwaka haishi Cameron lakini anaishi uswisi hotelini na kwa siku analipa dollar elfu kumi.

Ukija Gabon washaimaliza Gabon kwishaa. Aliyekuwa rais wa ufaransa Jacque Chirac aliisafisha kabisa Gabon yeye na marehem Omar Bongo.

Familia ya Paul Biya Cameroun na Omar Bongo wenyewe hawajaweka vikwazo kwasababu ni vibaraka wa Ufaransa Uingereza na Marekani. Lakini ndugu yao kuroka kabila moja tuseme wamasai wa Kenya na Tanzania au wakuria wa Kenya na Tanzania tatizo lao ni kutaka kumgawia Urusi mikata ya kuchimba mafuta.

Sepo Blatter aliyekuwa Rais wa Fifa angekuwa Rais hadi leo kosa alofanya ni kuipigania Urusi hadi kuwaandaa na kuwa mwenyeji wa world cup 2018
Sio kila jambo lazima waafrika tusubiri hadi mizungu itufanyie.kwasababu wazungu nao ni banadamu na lazima wawe na interest kwa mambo kadha wa kadha.mambo mengine inapaswa tutumue akili zetu wenyewe kujikomboa na kujisimamia.Lakini huu ujinga wakukaa nakusema mbona pale ulifanya vile na hapa hufanyi kamwe haiwezi kutusaidia kama waafrika.
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,420
2,000
Huo ukanda wa Africa ya kati Congo zote mbili, Gabon, Central Africa Republic Cameroon na Equatorial Guinea kuna mali na madini mengi ya kutisha. Ukiondoa madini kuna misitu ya hatarii na ardhi nzuri kwa kilimo.

Makampuni mengi ya ulaya yamewekeza huku na wana influence kubwa sana na wanasiasa kwa kuwa Linda. Viongozi wao wengi ni wezi wakubwa ambao wana kula na haya Makampuni ya Magharibi.

Mfano Paul Biya kajaza serikalini na jeshini watu wa kabila lake. Marais wote wa hizi nchi wana jeshi ndani ya jeshi la nchi.

Obiang alikuwa anaiba vizuri tu wa Magharibi tatizo alivyoanza uhusiano na Putin lakini ajachelewa vyanzo vinadai ameshamkana sasa hivi Putin huenda wakamsamehe
Hayo yote ni matokea ya ujinga wetu kama waafrika.wazungu wanatutumia kwasababu wanatuona tuna matatizo ya ujinga na ubinafsi.Ila pia wizi wa mzungu una afadhali mara mia kuliko wizi wa miafrika menzetu.mzungu anachukua kwako anapeleka kwao anaenda kuzalisha maradufu alafu kiasi anakurudishia ili nawewe unufaike ila muafrika akiiba anaiba kwake anaenda kuficha kwa wazungu na hakuna chochote kitakachorudi kunufaisha watu wake.
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,420
2,000
Ujinga na ubinafsi ndo matokeo ya hayo yote.Sasa mtu unajimilikisha mavitu yote hayo tena nchi za watu wakati kwenu kuna dhiki hiyo ni akili au ujinga.ndo maana mimi bado nasema kua muda wetu wakustaarabika bado haujafika.Afrika inawezekana tuna tatizo la kiasili ambalo bado hatujalijua.
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,576
2,000
Hayo yote ni matokea ya ujinga wetu kama waafrika.wazungu wanatutumia kwasababu wanatuona tuna matatizo ya ujinga na ubinafsi.Ila pia wizi wa mzungu una afadhali mara mia kuliko wizi wa miafrika menzetu.mzungu anachukua kwako anapeleka kwao anaenda kuzalisha maradufu alafu kiasi anakurudishia ili nawewe unufaike ila muafrika akiiba anaiba kwake anaenda kuficha kwa wazungu na hakuna chochote kitakachorudi kunufaisha watu wake.
Umesema kweli mkuu. Gabon sasa hivi mafuta yote yamekwisha mfaransa anazidi kupeta na makampuni yake. Gabon inahuzunisha sana Kwiiishaaaa
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,822
2,000
Si anasaidiwa asiekuwa na hela mkuu, hao watu wana hela inachezewa na watawala , ni sawa tu irudi kwa mahitaji ya chanjo.

Mie sina tatizo na kudaiwa au kupokonywa pesa hao wezi kwa jina la madaraka.
Kwa maelezo ya report, wananchi wana hali mbaya sana na nchi ipo kwa lindi la umasikini. Si wangewafanyia mambo ya msingi na chanjo wakawapa kidogokidogo?
 
Trillion

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
2,642
2,000
Mie sina tatizo na kudaiwa au kupokonywa pesa hao wezi kwa jina la madaraka.
Kwa maelezo ya report, wananchi wana hali mbaya sana na nchi ipo kwa lindi la umasikini. Si wangewafanyia mambo ya msingi na chanjo wakawapa kidogokidogo?
Watawala wa hovyo hivyo huwa wananyimwa misaada.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,822
2,000
Watawala wa hovyo hivyo huwa wananyimwa misaada.

Nafikiri kuna mahali tunapishana. Hizo pesa hao wazungu wamezichukua na kuamua kuwapelekea wananchi chanjo, si zingewasaidia kwa mambo mengine ya muhimu zaidi?

Hata kuwapelekea chanjo na madawa bado ni msaada. Kwanini wawachagulie cha kuwafanyia?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom