icca
Senior Member
- Nov 8, 2014
- 180
- 169
Habarini za asubuhi wana jamvi, Msaada wa mawazo kidogo.
Ni mda wa miezi zaidi ya miwili sasa nakaa na rafiki yangu, Tulikutana eneo la kazi mimi na yeye tukiwa ndo wanawake io hali ikatufanya tuwe marafiki, tunasaidiana katika mambo mengi na ni mtu mzuri.
Miezi miwili iliopita mambo yake hayakwenda sawa akaniomba aje akae kwangu kwa mda mfupi akijipanga ili aende kupanga, Ila sasa naona kabisa uvumilivu umeniisha na sijui anaondoka lini na naona nikimuuliza atajisikia vibaya.
Ratiba ya kwangu imebadilika kabisa, mimi si mtu wa kutoka napenda kuwahi kurudi nyumbani na kupata mda mwingi wa kupumzika, yeye anachelewa kurudi akirudi ni hekaheka atataka tuongee nisipomjibu anajisikia vibaya, atabamiza milango, uo usiku ndio atataka apike, kunakua hakuna utulivu na kachumba ni kamoja tu,..najikuta tu nina hasira na kisirani.
Mnachukuliana vipi na watu wa haina hii?