Mnaangalizia wapi JF jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaangalizia wapi JF jamani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaniki1974, Jun 24, 2009.

 1. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kazini, nyumbani, internet cafes, simu za mkononi au wapi? Ni kutaka kujua maana watu hadi posts 15,000? Inakuwaje? Wengine 24/7? Mnabalance vipi na mambo yenu mengine? Hakuna walioathirika vibaya na hii kitu? Hebu tuambiane ukweli basi..I dare to talk openly?
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Yo-Yo: ''Wanaume wanaotumia muda mwingi JF hawana mashori wazuri''
  Itabidi tuitishe FJ Bash tuone kama Yo-Yo yuko sahihi.
   
 3. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwikwikiwiiiii!
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Aisee kweli bwana, JF is as addictive as heroin! Bila dozi ya 'angalau' saa moja ya JF unaweza kosa usingizi ati!
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  sio siri mimi na jf nikama samaki na maji. kwanza ndo home page yangu.kwa kifupi mimi naangalizia kwenye ka laptonga kwangu huku mbele (oslo) ambako napiga shule.
  huwa napata taarifa kibao.
  Nyani ngabu wewe vp?
   
 6. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuangalia JF kunawiana vipi na kuwa na post 15,000? Ili ufikishe post hizo lazima uandike na kupost kwenye thread mbalimbali.

  Pia ili ufikishe posts 15,000, lazima uanze na kupost post moja. So worry not, iko siku nawe unaweza fikisha idadi hiyo ya post. Kama umejiunga JF jana au mwaka jana usijilinganishe na mtu aliyejiunga hapa mwaka 2006.

  Zaidi ya hayo, kama wewe ni bank teller, na baada ya kazi unaenda kupata kilaji, usijilinganishe na mtu ambae kazi yake ni kuandika na kufanya uchunguzi, muda wake mwingi anautumia kutafuta habari na kuzianalyse, kutunga habari na kuzichapisha na mambo kama hayo.

  Usiige tembo kunya, utapasuka....
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  I wonder what is your motives. At the end of the day where do you want to take us to? Worry not about statistics, mind their contributions and learnings from great JF people. One posting can mean a lot than 15,000 posts. Mind the contents rather.
   
 8. GP

  GP JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  teh teh teh kwi kwii kwii!
  kuna tofauti kubwa ya lini mtu kajiunga na idadi ya post zake, mtu wa 2006 na 2009 ni tofauti, kuna mtu mmoja wa 2006 (jina kapuni) hajafikisha hata post 500!, yupo wa March 2009 anapost zaidi ya 1000!, ukiangalia hapo utakuta wengine wanapost hata pumba tu, ili mradi aonekane ana posts nyingi, bora upost hata 2 zenye akili kuliko 100 zenye matope!

  kuna wazee wa kukopi na kupaste, hawa hawafikirii kwa akili zao, bali ni kunakili what others did, wanaonekana vichwaaaaaaaaaaaa kumbe hawana lolote
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tumtendee haki muuliza swali. Mwenzetu anataka kujua watu wanaangalizia JF wapi? kazini, nyumbani, shuleni na wana balance vipi majukumu yao ya kila siku na JF addiction.

  Ndugu yangu... wewe angalia unataka kushiriki JF kwa lengo gani.Je ni kujifunza na kubadilishana uzoefu na wenzako? Ni njia ipi bora itakufanya ufikie azma yako?Ukiwa kazini kwa vyovyote unatakiwa ufanye kazi kwanza kabla ya kukimbilia JF vinginevyo kazi yako itaathirika kwa hasara yako mwisho wa siku.Kama wewe ni mwanafunzi, ukishinda JF ujue shule itakushinda. Kwa maneno mengine tenga ,muda wako... unaweza kutumia muda wako wa lunch au mapumziko kutembelea JF.

  Kuna swala la gharama. Ukisema uende internet cafe kila siku na kila wakati, je ushiriki wako JF unalipa kiasi cha kuweza kubeba gharama za internet? Ushauri wangu ni kutumia nafasi uliyo nayo kufanya vitu kadhaa kwa wakati mmoja. Ukiwa uko kwenye internet unafanya mambo mengine yenye kukuletea pesa unaweza ukaunganisha na ushiriki wako JF. Labda uwe na budget maalum ya kujifurahisha na badala ya kwenda kwenye unywaji basi tumia budget hiyo kufanya kitu chenye manufaa zaidi kama kushiriki JF.

  Kilevi chochote kinaweza kuwa na madhara. Hivyo ndugu muuliza swali ukae ukijua kuwa JF ni nzuri lakini pia inaweza kukuathiri kama laivyosema ndugu yetu SMU.

  Kila mtu JF ana mchango wake na kwa aina tofauti. Kuna wenye kuuliza maswali kila kukicha wakitaka ushauri, kuna wenye kuleta mizaha na utani na hii pia ni muhimu kusaidia watu ku relax, kuna wenye kuleta mada moto zenye kuhitaji michango na analysis, kuna wenye kutafuta na kubandika habari kutoka vyanzo mbalimbali. Hawa tena mimi naweza kuthubutu kusema kuwa ni muhimu mno maana kuna watu hawawezi kupata habari hizo kwa urahisi. Hivyo ni makosa kubeza watu kwa michango wanayoitoa JF.

  Ndugu yangu, usihofu kuchangia kwa style yoyote kwa maana kila mchango ni muhimu hapa JF.
   
 10. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nilitaka kumuuliza pia huyu mkuu....
   
 11. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwikwikwiiiiii anayemuiga tembo kufanya hivyo, mjinga sana....hope haumuigi tembo pia teh teh teh. You got it bad!
   
 12. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli Mkuu, wengine ni matusi tu, wanapewa ban lakini wakirudi tu post yao ya kwanza ni matusi, sasa sijui wingi wa post una maana tena hapo!
   
 13. Madam Koku

  Madam Koku Senior Member

  #13
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ila kuna mtu alishauliza siku za nyuma swali almost similar na alilouliza Kaniki kwamba watu wanafanya kazi zao sangapi maana wanatumia muda mwingi JF? akajibiwa kuwa kuna watu ambao kukaa kwenye mtandao (kama JF) ndo kazi yenyewe. Kama ni kweli basi obviously wao watakuwa na muda mwingi na post nyingi zaidi ya wale wanao visit JF kwa kutoa/kutafuta habari, kupumzisha akili, nk
   
 14. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #14
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Duh,

  Kwa mara ya kwanza nasikia hii... Hahahaha, yani mtu kazi yake ni kukaa JF kujibu posts?

  Hata Admin au moderators JF si kazi yao rasmi (as far as I know). Kama wapo wa hivi kweli kazi ipo....
   
 15. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ha!ha!ha! Mkuu Max.....nadhani hapa wadau watakuwa wanarefer washkaji wa UWT na kuna wale wengine ambao wanaweza kuwa sponsored just ''kuspoil mazingira'' hapa!
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hehehe
  Maxence umeniacha hoi.
  Hujui kwamba kuna viumbe humu kazi yao kutwa kuchwa ni kujua nani kapost nini na wamjibu vipi na kisha wanacompile report then haoooo wanaipeleka kunakohusika?

  Mie huwa naangalia JF kila mtandao unapoconnect. I mean huwa nina mambo yangu muhimu nayafanza kisha kila nukta nikaapo net huwa nalog in ili kupata kitu kipya kwa ajili ya ufahamu na akili yangu. Yaani nikiamka manane na nikakosa usingizi huwa naingia mtandaoni na kuzungumza na wakeshaji wenzangu.

  Ila kiukwelii kuna walumendago humu ni wababe hata wakanywe vipi ila kwa kuwa ndo jamii yenyewe, bila wao hakuna sisi.

  niko adiktive kiukwelii
   
 17. n

  nyashi Member

  #17
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna watu humu ni kama vile hawana kazi ingine zaidi ya jf hata kama ni kutafuta habari na ku anaanalyse i think it's abit too much
   
 18. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni mtazamo,

  Kwa kusoma replies nyingi hume ndani sijaona hata mmoja ambaye anasema yeye ni online 10 hours p.d, hii inamaanisha wengi huingia kwenye net kwa kubahatisha, pia inaashiria swala la internet penetration katika bongo bado ni ndoto.

  Internet ni nzuri ila kama vitu vingine ukitumia sana unakuwa adictive, kwa wale waliojiunga na JF kwa ridhaa zao bila kushurutishwa wanaweza kuaccess pahala popote home, work place, phone just like breathing.

  Kuna mtu anaitwa joyceline mhh....
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Jun 25, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi matawi ya juu. Niko wired 24/7...

  Wengine tuko hapa muda mwingi na wengine wako facebook 24/7 wakianika mambo yao binafsi....
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Swaadaat....wanashinda hapa 24/7 walio wengi wanajaza Pumba
   
Loading...