"mnaacha mazuri tuliyotenda, mnachukua mabaya tuliyoyaacha" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"mnaacha mazuri tuliyotenda, mnachukua mabaya tuliyoyaacha"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jacobus, Oct 28, 2012.

 1. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Mie husikiliza TBC 'Taifa' radio hasa kipindi cha WOSIA WA BABA kinachotoa hotuba za BABA WA TAIFA kila siku asubuhi, vipindi vingine ukiacha hicho na vile vya Masoud Masoud ni vya hovyo ikiwemo Taarifa zao za habari. Kilichonifanya niruke hewani ni kuona kuwa hotuba zake mwalimu za hivi karibuni hazichezwi hasa hii iliyokuwa ikiwakumbusha WATAWALA wetu hawa jamaa hawaweki asilani.
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Achana na fikra za walio makaburuni wewe! Mwenyewe ameshindwa kuzitekeleza, kila mtu anafikra zake hapa na mtazamo wake kwanini tuendelee kuthamini mawazo ya watu ambao no more! Tunahitaji kwenda mbele sio kurudi nyuma.
   
 3. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  BinMgen unanishangaza mno, hivi binadamu huishi vipi kama sio HISTORIA? Tuna UKRISTU na UISLAM hapa duniani achilia mbali imani nyingine, sasa WAANZILISHI wake wako WAPI?????????????
   
 4. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,982
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Mbona title yako na maelezo haviendani?
   
 5. c

  cencer09 JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 2,320
  Likes Received: 484
  Trophy Points: 180
  fikra zote zinazotawala duniani waanzilishi wake hawako duniani.na huwezi kwenda mbele bila kuboresha au kubadilisha fikra za waliotutangulia,kuanzia technology HADI ITIKADI ZA KISIASA.aidha hujui usemalo au ni mwanauamsho ambao kwa mapungufu yao hutafuta sababu za kumsdicredit Nyerere.ana mapunguzf yake one being arrogant lakini ni mzalendo
   
 6. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Mkuu sikubaliani nawe hata kidogo,kwa hoja yako.Mwl.Nyerere alitahadharisha na hata maneno yake mengi ameyasema ktk kipindi cha utawala wake to mean he was aware na bado kwa yale aliyoyaweza alifanya bila haya.sasa fikra zake bado zinaishi mpaka sasa,mtu mwenye maono hutamka maneno yenye kuishi na kwa kweli naweza kuita kuwa alikuwa na fikra pevu.

  mwl.Nyerere wakati anaachia ngazi aliasa kuwa yapo mazuri ambayo utawala wake ulifanikiwa na yapo mengine hakufanya vizuri akashauri haya mazuri ni vema yakaendelezwa na mabaya yarekebishwe,nini tunafahamu ni kuwa hakuna kiongozi anaweza kumaliza matatizo ya nchi yake kwa kipindi awacho madarakani,thats why kila baada ya muda hupewa wengine ili waendeleze walipoishiwa wenzao kwa mujibu wa katiba iliyopo ya 1977.Hasa twahitaji kuona serikali ikileta maendeleo si tu kusogeza muda.

  Mwalimu aliyaona haya(uroho wa madaraka with no agenda,wizi,uvinjifu wa sheria,ubaguzi,ubinafsi na n.k) na ndiyo yanatukia sasa,leaders have no agenda for their leadership fight,what they need ni kuwa waonekane nao walitawala.Hatukubaliani na hali hii na ndiyo maana mtoa hoja kaja na uzi huu,nadhani ni vizuri kujadili ktk misingi ya kukua kifikra badala ya mawazo kama yako ya kuturudisha tusikotaka kwenda.

  Mkuu sote tuna wajibu mpana kwa Taifa letu,hatuwezi kuendesha nchi pasi ya utaratibu,hatuwezi kuendesha nchi kwa mawazo ya mtu mmoja na kutegemea na alivyoamka hili si sawa.Lazima tuwe na utaratibu na tuusimamie na si kujenga hoja dhaifu kuwa kila mtu ana mawazo yake. Basi utawala wa aina hiyo ni fujo na hauna la kutusaidia watz.

  Acha kubeza juhudi za waasisi wa taifa hili,waliojitoa maisha yao kwaajli yetu pasi ya kuangalia ugumu waliopita.

  Mtoa hoja kasema kipindi cha wosia wa baba wa taifa ni muhimu kwa kuwa yeye ni moja ya watu wanaojengwa na fikra za mzazi wa Taifa hili na haoni sababu ya kituo hiki cha Taifa kufutilia mbali kipindi hiki,lakini twajua watawala wanaona wanajikaanga wenyewe kwa kuachia hotuba hizo kusikika.Hatuhitaji kuzibwa masikio wala kufungwa midomo kama Watz tunazo haki za msingi ikiwa ni pamoja na uhuru wa habari,kutoa na kupokea habari alimradi hatuvunji sheria. Uwe na jumapili njema!
   
 7. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Nashukuru wengi hapa wamenielewa kuwa katika vipindi vya TBC'Taifa' radio pana kipindi KIZURI mno wao wamekiita WOSIA WA BABA, lakini mie msikilizaji wao huwa nasikia marejeo ya mara kwa mara ya hotuba za Baba wa Taifa zihusuzo WANANCHI na SIO zinazowahusu watawala wetu na mfano wa hutuba hizo ni hiyo iliyopo kwenye title niliyoiweka. Kama uliishaisikia TBC nifahamishe. Angalia sasa mambo ya FUJO kwa kisingizio cha UDINI yanavoshamiri nchi, ni hatari kweli kweli.
   
Loading...