MMU Thread Collection - General Topics discussed and posted in the Forum before Sept 2012

Status
Not open for further replies.

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,078
Habari wana MMU na JF as whole,

Kutokana na malalamiko ya baadhi ya members na mimi mwenyewe kuunga mkono malalamiko hayo nimeomba kwa mkuu Invisible katika thread ya Ngabu kuweza andaa thread ambayo itakusanya thread zote ili kupunguza idadi ya Stickys ambazo zote zitakuwa katika sticky thread ambayo ni hii nimeandaa.

Nimechukua nafasi kuandaa hii thread ikilenga ku upadate mara kwa mara thread ambazo zimejadiliwa hapa MMU ziwe hazikubaliki ama kukubalika kwa wote mradi ziwe ndani ya yale ambayo yanafanywa katika jamii na kwa namna moja ama nyingine hizo thread in a way ziwe zina elimisha/burudisha/ongeza ufanisi ama uelewa nakadhalia.

Nawaomba wanafamilia wote wa MMU tukumbushane ni thread gani ambazo zinatakiwa ziwe updated katika thread hii. Nilichofanya hapa ni kuchukua links ya thread zote zilizoluwa zimebandikwa hapo na kuongeza nyingine kadhaa ambazo nakumbuka na baadhi ambazo zimekuwa suggested kwa an alternative (pm) na kuziweka hapa.

Naamini na kujua kuwa kuna threads zipo nyingi mno. Hivyo kuna zile kwa wewe kama my fellow member ukiziweka in a post kukumbusha kwa namna moja ama nyingine inakuwa inaturudisha nyuma na kutukumbusha huko. Nitaomba ushirikiano wenu wa dhati katika hili, na natanguliza shukrani kwa ushirikiano wenu.

  1. Utatu wenye utata - umri, pesa na mapenzi - JamiiForums
  2. Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wa maisha - JamiiForums
  3. Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada - JamiiForums
  4. Mwanaume KAMILI - JamiiForums
  5. Tofauti ya umri katika mahusiano na kwa wanandoa (mume na mke) - JamiiForums
  6. Haya huchangia Mwanaume kuwa mchovu kitandani - JamiiForums
  7. Matumizi ya simu katika Mahusiano - JamiiForums
  8. Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi? - JamiiForums
  9. Kwani lazima kuoana? - JamiiForums
  10. Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa - JamiiForums
  11. My thoughts, what are yours? - JamiiForums
  12. Wajua jinsi ya kumdhibiti mpenzi anayepiga mizinga? - JamiiForums
  13. KITCHEN PARTY BUBU.. Nafasi ya MKE ndani ya NDOA (Kwa wanawake tu!!!) With Love to You Cheusie - JamiiForums
  14. Umuhimu wa chakula katika mapenzi/mahusiano - JamiiForums
  15. Do you feel LOVED? - JamiiForums
  16. NDOA: Zamani vs Siku hizi - JamiiForums
  17. Wazazi/mzazi wa binti - JamiiForums
  18. Tahadhari kwa wanawake walioolewa - JamiiForums
  19. Mafanikio kimaisha - JamiiForums
  20. Mtizamo: Let love lead the way - JamiiForums
  21. To revive 'intimancy' in your marriage - JamiiForums
  22. Eti hatujui... kipimo gani kinatumika? - JamiiForums
  23. Aina za ndoa - JamiiForums
  24. Usha flirt naye sana - JamiiForums
  25. Bi dada... Utafanya nini? Mmeo anatembea na binti wa Salon...! - JamiiForums
  26. Mdahalo: Kids Vs Spouses - JamiiForums
  27. Sisi ndio wanaume bwana! - JamiiForums
  28. Nani kama Mama Vs Nani kama Baba - JamiiForums
  29. In love, its about teamwork - JamiiForums
  30. Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo) - JamiiForums
(Hii thread hii should be a closed one aisee, alter Roulette hebu fanya mambo kama hongo nitakupa)

The guide: Ukishaamua kuwa na 'nyumba ndogo' - JamiiForums (same applies hapa The Boss....:canada:)

  1. Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA' - JamiiForums
  2. Zawadi ya ngono - JamiiForums
  3. Mwanaume mtaalamu jikoni - JamiiForums
  4. Can Men and Women Be Friends? - JamiiForums
  5. The best way to breakup. Is there any? - JamiiForums
  6. Kumdhalilisha Mpenzi/Mke/Mme - JamiiForums
  7. The Power of Letting Go.... - JamiiForums
  8. Mawasiliano katika mahusiano - JamiiForums
  9. When Women Take Charge..! - JamiiForums
  10. Mahusiano na Wakwe/Mawifi Nini kifanyike? - JamiiForums
  11. "A man should provide for his wife. PERIOD" - JamiiForums
  12. Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...! - JamiiForums
  13. Fumanizi: Kwanini wanawake hupenda kuwalaumu wanawake wenzao? - JamiiForums
  14. Mwanamke: Je, unatafuta mchumba? Fuata kanuni hii hakika utapata mchumba mwenye tabia uzitakazo - JamiiForums
  15. Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe? - JamiiForums
  16. CONFESSION: Madhara ya Vidonge vya Uzazi Wa Mpango - JamiiForums


Take Note:-

Nilikuwa nikienda katika profiles za members mbali mbali ambao nimekumbuka haraka haraka na ku copy links tokana na topic head. Nyingi hapo sijaangalia content hivyo kama haifai tutaambiana tu. It should be noted as plenty as possible zaweza kusanywa. Ilikuwa ziwe kwa mtiririko wa topic name but nikashindwa na hivo kuziweka randomly.

Pamoja Saana with Love,

AshaDii.
 
Thank goodness!

It's about time the forum gets cleaned up.

I am glad you approve Ngabu. Na Thanks to you too hili limefanyika.

Good idea,kuna jukwaa moja huko mafichoni sticky nazo zimezidi,hii idea ingefaa pia

Niliahidi kufanya hivi kwa jukwaa hili na la Doctors, hayo mengine nadhani wengine wanaweza jitolea pia. On second though nitafanya hivo na kwa Jukwaa la Wakubwa lol.

Excellent it has been long dear, I hope you are well and good.

Asante sana AshaDii
ngoja tuendelee kuangalia MMU tuone topic ambazo zinafaa ziingie hapa
Asante sana

You are welcome R. Uzuri wa hii ni kuwa yeyote anaweza compile threads in a post. Mradi ipo katika hii thread ni rahisi wadau kuiona.
 
Ahsante sana ADii,

Naunga mkono wazo hili. Hata hivyo, nilishindwa kukubaliana na hoja za awali kwa sababu kulikuwa na dalili za ku-ofend baadhi ya watu. Inapotokea mtu kachangia kwenye thread na kuiponda kwamba haina mshiko halafu anakuja baadaye kuomba iwe miongoni mwa zile ambazo siyo sticky, inaleta mashaka kwenye nia ya huyo mtu.

Hata mimi nilishaona kuwa baadhi ya thread. Thread ambazo ziliwekwa ili zionekane wakati wote, hazikuwa na viwango vya kukidhi haja.

Ila naona sasa kwa kuziweka kwenye thread moja, hata wewe umeweka nyingi mno kiasi kwamba unaweza kutengeneza collection ya thread nyingi sana na mwisho wa siku ikaturudisha kule tulipokuwa.

Kama ni kura labda zipigwe au tukubalii kuwaachia baadhi ya watu wafanya kazi ya kuchambua thread vinginevyo lawama zitakuwepo tu!

Ni hayo kwa sasa,

Babu DC!!
 
Kaka DC,

Nimekupata vema. Mie nakumbuka (tokana na thread ya Ngabu) thread yako ni moja ya zilizogusiwa. Nililoelewa pale kuhusu thread yako ni kuwa zilikuwa ni moja kati ya tatu zilizo orodhwesha zenye kujadili kitu kimoja. Kimsingingi kaka DC hili ni kweli. MMU ni kisima cha habari nying mno zilizojadiliwa.

Mie pamoja na kumaliza kwangu mwaka hapa karibuni najua bado kuwa kuna mengi yalinipita na ndio maana nimetoa uwanja mpana kila mmoja asema. Tukizungumzia viwango vya thread hio nayo ni muhimu... Ila naomba kumbuka kuwa mara nyingi tuna vipimo tofauti kama wanadamu (tokana na sababu mbali mbali) za kupima ubora wa kiwango cha thread. Naweza ona thread ni kiwango sana lakini mwingine akaona taofauti.

DC kuhusu uwingi wa threads ambazo nimeorodhesha naona hilo sio shida kabida. Kucopy na kupaste thread kumeboreshwa kiasi kwamba mtu kamba hujaifungua unajuwa wazi kuwa hio thread ina husu nini. Kwa maoni yangu (thou I stand to be corrected) naona kuwa hata zikiwa nyingi hapo zikafika hata 100 haina shida. Ni rahisi kujua ni nini unataka na ni tofauti kabisa na Stickys zikiwepo.

Sijui ila logically na realistically sion kabisa haja ya kura, ila maoni, ushauri na mawazo mbali mbali ni muhimu ili kuwezesha thread ifanye vile ambavo tumelenga na kutarajia. Na ndio maana nimesema kuwa ni rahsi, mwingine anaweza pia kuamua kupost link zake katika hii thread ili kuonesha ni thread gani ambazo yeye kaona ni bora na zianafaa watu wapitie...

Naona kuwa zimeshafanyiwa kazi na wametowa hizo 'Stickys' hapo nje ambazo zilikuwa ni nyingi mno na kuboa wengi. Sijui kama umenipata vema kaka. Naomba utanielewesha ama kuniuliza popote pale ambapo sijaeleza vema. Kama kawa, pamoja saaaana.
 
Niliahidi kufanya hivi kwa jukwaa hili na la Doctors, hayo mengine nadhani wengine wanaweza jitolea pia... On second thot nitafanya hivo na kwa Jukwaa la Wakubwa lol.

Excellent it has been long dear, I hope you are well and good.
Mi nipo but nimetingwa na mambo kiasi flani ila nipo na nitakwepo
 
Sijaelewa elewa hasa nini hapa kinajadiliwa
but between Ashadii NN na Dark City nafikiri kuna kitu useful kinajitokeza
 
Sijaelewa elewa hasa nini hapa kinajadiliwa
but between Ashadii NN na Dark City nafikiri kuna kitu useful kinajitokeza


Why Boss, kuhusu my posts na DC ama kuhusu thread yenyewe? Sijakupata vema...
 
Sijaelewa elewa hasa nini hapa kinajadiliwa
but between Ashadii NN na Dark City nafikiri kuna kitu useful kinajitokeza


Tatizo mkuu hapa kuna coincidence ya mambo ambayo hawezi kutuacha bila mashaka.

But, mie nitakubaliana na matakwa ya wengi,

Babu DC!!
 
Ahsante sana ADii,

Naunga mkono wazo hili. Hata hivyo, nilishindwa kukubaliana na hoja za awali kwa sababu kulikuwa na dalili za ku-ofend baadhi ya watu. Inapotokea mtu kachangia kwenye thread na kuiponda kwamba haina mshiko halafu anakuja baadaye kuomba iwe miongoni mwa zile ambazo siyo sticky, inaleta mashaka kwenye nia ya huyo mtu.

Dah! I didn't know you were this hypersensitive. No one intended to offend you. And If you took offense you could have just spoken up about it and we could have hashed things out.

Anyway, kwenye hiyo mada yangu bandiko langu la kwanza niliandika hivi:

Hizi mada zimekuwa nyingi mno sasa hadi zinakera.

Zinafanya surfing kwenye hili jukwaa na mengineyo isiwe ya kupendeza kabisa.

Ili upate mada mpya inabidi u-scroll weeee hadi mtu unapatwa kizunguzungu.

Jaribuni kuzifanyia mapitio tena hizo mada mlizoziwekea sticky muone kama bado zinastahili kuendelea kujaza nafasi

Baadaye ndiyo Elizabeth Dominic akaniuliza ni mada gani ambazo ningependa ziondolewe na kwa sababu gani? Nikatoa mfano wa mada tatu, moja ikiwamo ya kwako, ambazo kimsingi zina maudhui sawa lakini ambazo zote zilikuwa na sticky.

That was a valid argument and I'm disappointed that you didn't see beyond your personal grievances that you have with me to appreciate its validity.
 
Why Boss, kuhusu my posts na DC ama kuhusu thread yenyewe? Sijakupata vema...


Ndo maana na mimi nilisema sijaelewa haswaa ni nini hapa mnafanya

anyway ni hivi
nakubaliana na NN kuwa threads za sticky ni nyingi mno
na nyingi hazistahili au hatujui ni vigezo vipi zikawekewa sticky.

Lakini bado nafikiri kuna threads zina 'tofauti' hata kama kuna mwingine alisema theme hiyo hiyo. Mfano thread ya DC ya mwanaume wa kiafrika binafsi sioni kama inafanana na zingine, mfano ile ya mwanaume kamili......hazifanani so kuziunganisha pamoja sio sahihi.

Tatu hii idea yako ya kuzi combine threads zenye 'value' fulani MMU....ni nzuri
wasiwasi wangu ni kuwa still baadhi ya threads nzuri zinaweza zisiwepo
na zingine pengine sio nzuri saana zikawepo sababu....it is Ashadii 's taste.

Sio general members taste but then again kupata general members taste nayo sio rahisi. So ngoja nisubiri nione all in all a good idea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom