MMU Mmenisaidia kuandika Script ya Ukweli

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Huwezi kujua mchango wako mpaka pale taadhira zake (Impact) zinapoonekana. Wana MMU mjue kuwa kuja kwangu humu mmenisaidia sana kuandika Script ya Movie ya ukweli. Michango yenu imeonyesha kwa undani kabisa jinsi watanzania wanavyoyachukulia mahusiano na tofauti zetu za mitizamo hata na majirani zetu wa Kenya.

Nimewashawishi na marafiki zangu nao wawe wanatembelea humu ili waondokane na kuendelea kuandika Script ambazo hazitoi taswira za watu wa "Buguruni kwa Mnyamani" ambao ndiyo wengi. kuwemo kwangu humu kumeonyesha kumbe tafsiri yetu kuhusu mahusiano kwa sehemu kubwa sisi waandika Script iko mbali sana na ukweli.

Nimejifunza ni vitu gani watanzania tunaviona vinaonekana vinawezekana kutokea na vingine hata kwa mtutu wa Bunduki hawawezi kuvikubali. Movie yangu ijayo nitai i- dedicate kwa Member wa humu MMU. Alamsiki!!
 
Katika hiyo dedikesheni, usisahau kumtaja Babu mpenda maujiko Asprin a.k.a ODM. Vinginevyo haitauza sana.

Kila la kheri.
Tumrekodie na ile sauti ya weweeeeeee nafikiri hapo itauza sana, Kigarama usisahau kututafutia scene ya kucheza kwenye filamu Asprin anapenda kucheza kwenye scene za ukabaji
 
Tumrekodie na ile sauti ya weweeeeeee nafikiri hapo itauza sana, Kigarama usisahau kututafutia scene ya kucheza kwenye filamu Asprin anapenda kucheza kwenye scene za ukabaji
Weeeuuuuweeeee! Ndiyo iwe taito ya hako kamuvi, afu avatar ya ODM ndo inakuwa picha ye mbele. Isipouza, akaogee magadi.

masharti ya ODM kutajwa ni kurejesha huduma ya ukaguzi..
Hebu angalia muda wako hapo, Sasa hivi saa ngapi vile? Haya, come this way..........
 
Kama kweli utafata ushauri wa humu basi kutakuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye tasnia ya filamu zetu na hata sisi wengine tutaanza kuziangalia. Nakutakia kila la heri.
 
Sasa akiniweka mimi akamsahau soulmate wangu.......... labda kama anatoa singo la taarab....khanga Mokko! vinginevyo albam zitakuwa picha za ukutani

umeona eh? Yuu mai taksi draiva!

daaah hivi binamu hajambo.................
 
waigizaji utawatoa wapi sasa?? au ndo hao hao kina anko Ezekiel!???

Tatizo letu Bongo ni wadosi, unajua hawa jamaa wananunua Movies za kina Ray na Kanumba mpaka kwa Milioni 40 au 50, lakin kwa wale wasiofahamika wenyewe wanawaita "underground" umeuza sana tena kwa mbinde wananunua picha yako kwa Milioni 20.

Ukienda Steps Entertainments unapewa hela ya Movie Shooting na Location kuanzia Milioni 3 hadi 10 kutegemeana na Script Synopsis unayopeleka kwa mdosi. sasa hapo ndiyo kina Aunt Ezekiel wanapoingia.

Na wakati mwingine siyo Script Director au producer na Location manager wanaochagua scene iwe na nani au ipigiwe wapi bali ni wadosi wenyewe. Hivi hujiulizi ni kwa nini kuna baadhi ya production Companies shootings zao zote zinafanyikia Giraffe Hotel au Lamada?

kwenye Film Industry ya bongo wadosi ndiyo kila kitu kama ilivyo kwenye muziki. Kina aunt Ezekiel tutaendelea kuwa nao kwa sana tu.
 
1. Asprin - Huyu anacheza scene za ukabaji na wizi
2. Gaga - Huyu anacheza scene za kukwiba soulmate
3. Blaki Womani aka Yuu - Huyu anacheza scene za mamakubwa
Asije akatoa movie ya ile story yangu ileeeeeee, nitaachika, lakini atleast ninae soulmate kanipenda hivohivo
 
Sasa mbona unacheka afu hujanigongea kale ka-apetaiza kanakoitwa LIKE? Hebu ka-do ze needful bana.

ooh si unajua kale ka thnks walikitoaga
ila i like it na nimekugongea na daily huwa nakugonge au we unakataa
sema wazi huku JF wasikie kama kweli mie sikugongeagi..ahhahahaaaa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom