MMU hii ni hatari:- Afa akijaribu kupunguza kitambi kwa dawa za kienyeji.

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,683
8,830
Ndugu zanguni wana MMU nawasalimuni salamu za upendo wa dhati kabisa.NAWAPENDA SANA.
Jamani hapa mtaani kwetu kuna dada mmoja alikuwa na mpenzi wake wakaachana, lakini siku za jirani kapata katoto ka Kiarabu.
Kaarabu hako kakamwambia yule mdada apunguze tumbo,m dada mbiombio akaenda kwa Wamasai.
Wamasai wakampa dawa na maelekezo namna ya kutumia.
Mdada kanywa dawa hiyo jioni baada ya kutoka kazini. Dada kaharisha usiku kucha na mpaka asubuhi akawa ameishiwa na maji kabisa mwilini,
walipo mpeleka hospitali akafa madaktari wakiwa kwenye heka heka za kumuwekea drip.
Jamani bora tutumie njia nyingine kuliko hiyo mijidawa.
Nawatakieni siku njema.
 
Ngoja nikachukue kwenye ile sredi ya let love lead the way...
Pole kwa msiba.
 
khaaa! Rip mdada, alichanganyikiwa na mwarabu au?... Toka lini dawa za kimasai zikapunguza kitambi?
 
Akafa kwani ye ng'ombe..?

Amefariki binadamu..

Anyhow nampa pole huyo mwana kwa
Kumkosa mama ..
 
Pole kwa wafiwa. Hao masai ni kweli huuza dawa za kupunguza vitambi. Weshawahi kuniapproach pale mlimani city. Jamani mazoezi ndio njia bora hata hivyo tulizike jinsi tulivyo hii ndio miili yetu hapana haja ya kuruhusu presha toka nje ati mwili wako uwe kama fifty cent ama aaliyah
 
Wamasai wa siku hizi ni noma, wanadawa za kuzuia ndevu zisiote, wa naotesha nywele kwenye vipara, pia wana dawa ya kufanya gari lako lisitumie mafuta mengi
Hahahaha! Hiyo ni kali... Ila ndo hvyo dawa zinaua...au watumiaji ndo wanakosea masharti?..
 
Duh atakuwa alizidisha dozi ili apungue haraka maskini, ila wanawake tunashida na hii miili yetu!kama mtu kakupenda hivo ulivyo kwa nini anakwambia upunguze tumbo tena?
 
Inaitwa serikali legelege haina tofauti na wale wa ohio wanapitiwa na mtu yeyote ilimladi hela yako tu. Poleni mliopoteza dada yenu
 
kitu chochote kikzidi kipimo(doze) hugeuka kuwa sumu(toxic) dawa zinaweza kuwa ziko sawa ila doze alizidisha nway pole kwa msiba wa jirani
 
hawa waarabu nao,utakuta yeye ana mtambi pakacha nyuma jamani dawa za kimasai zinatibu kitambi kweli?dah
 
kweli maisha magumu mjini plus kutojitambua...namuonea huruma huyo mtoto aliyeachwa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom