TANZIA Mmoja ya wamiliki wa mabasi ya Sumry, Humud Sumry afariki dunia

Naona mmepost picha ya Salum Sumry wakati aliyefariki ni mdogo wake
Kweli watu watulie wanapoweka taarifa za namna hii:


24 Oct 2017
Msipazi Farm
Sumbawanga
Nkasi Rukwa Tanzania



Utajiuliza imekuaje Milionea Salum Mohamed Sumry akauza Mabasi yake yote 80? nini kilisababisha? AyoTV imempata Milionea Sumry aliekula hela zetu sana kwa kupanda Mabasi yake lakini sasa hivi hataki kusikia tena biashara ya Mabasi... kajichimbia wapi?
Source: millard ayo


WATAALAM WA KILIMO RUKWA WASHAURIWA KUWA KARIBU NA WAKULIMA WAO


Source : mbeyayetuonlinetv

Mwekezaji mwenye magunia 110,000 ya mahindi Rukwa atafutiwa soko.​

thumb_2380_800x420_0_0_auto.jpg
Imewekwa Tar: July 31st, 2018
Mkurugenzi wa shamba la Msipazi lililopo katiika kijiji cha China, kata ya Kate, wilayani Nkasi, Salum Summry ameiomba serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa rukwa kuona uwezekano wa kumtafutia soko la mahindi aliyovuna mwaka jana na mwaka huu ili kujiendeleza kibiashara.

Summry alisema kuwa tani 7200 za mahindi yaliyopo yamejaza maghala na hatimae mahindi yanayoendelea kuvunwa huwekwa nje jambo ambalo litahatarisha usalama wa mahindi hayo endapo mvua zitaanza kunyesha mwaka huu.

“Tunaiomba NFRA iweze kununua tani zaidi za mahindi maana yake mwaka huu wamenunu tani 5200 tu, tunaomba kutafutiwa soko, sisi peke yetu tuna tani 7200 kwenye maghala yetu na mengine tunaendelea kuvuna na kuyahifadhi hapo uwanjani kutokana na upungufu wa ma-godown (maghala), na mpaka sasa gunia 250 zimeharibika ila tutazigeuza kuwa pumba, hivyo hatutapata faida wala hasara,” Alisema.

Summry amesema kuwa wameona umuhimu wa kujaribu kupanda zao la alizeti katika ekari 1000 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya Mkoa katika kuliimarisha zao hilo huku ekari 3200 akiwa amepanda mahindi.

Ametoa maombi hayo alipotembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ikiongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Joachim Wangabo pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo na kamati yake ya Ulinzi ili kuona maendeleo ya mwekezaji huyo na kuona namna ya kufikisha huduma muhimu katika eneo hilo ambalo linatariwa kujengwa kiwanda cha mafuta ya alizeti, chakula cha kuku, pamoja na unga.

Mh. Wangabo alisema kuwa serikali ipo pamoja na wawekezaji katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa asilimia 100 na kamwe haitawaangushga wawekezaji hao na kumtaka Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda kuwa karibu na mwekezaji huyo ili kuwezesha kusaidia kutimiza ahadi ya viwanda 100 kwa kila Mkoa.

“Nimeona kuna mlundikano mkubwa wa mahindi ya mwaka jana na mwaka huu, serikali ipo pamoja nawe katika kuhakikisha tunakupunguzia haya machungu, hivi karibuni Rais wetu alizungumza na shirika la WFP na wao wamesema kuwa wataongeza idadi ya kununua mahindi zaidi kutoka Tanzania, hivyo wasiliana na WFP kupitia NFRA ili nuwe wakala na kujihakikishia soko, lazima ujisajili nili uweze kuwasaidia na wakulima wengine kupata soko.”Alisema.

Pia Mh. Wangabo alitoa pongezi kwa mwekezaji huyo kwa kuunga mkono juhudi za mkoa katika kufufua zao la alizeti na kujenga bkiwanda cha mafuta hayo na kumuhakikishia kuwa kiwanda hicho kitapata malighali ya kutosha kutoka kwa wakulima wengine mkoani humo.

Source : Mwekezaji mwenye magunia 110,000 ya mahindi Rukwa atafutiwa soko.
 
Back
Top Bottom