Mmoja wa 'Think Tanks' wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Mzee Warioba 'anatiririka' leo katika Kipindi cha dakika 45 cha ITV

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,869
Nimebahatika Kusikilizishwa 'Kiduchu' aliyoyasema ( kwani ni Kipindi kilichorekodiwa ) na kitaruka leo Jumatatu Saa 3 Kamili Usiku na kwa nilivyomsikia ni wazi Mzee Warioba kuhusiana na Suala la Katiba mpya ni kama vile kaamua 'Kujilipua' na kwamba kama noma na iwe noma tu.

Tafadhali natoa Angalizo mapema tu kuwa Mzee wa Watu kwa yale mtakayoyasikia juu ya shauku yake pia kutaka Katiba Mpya siyo muanze 'Kumchukia' na kuona si mwana CCM au hampendi 'Mama' bali Maoni yake yaheshimiwe mno.

Nawapenda sana Wazee wasiokuwa Wanafiki, Waoga na siyo Watu wa Kujipendekeza na kuwa 'Chawa' kwa Viongozi ( Watawala ) kama akina Mzee Warioba, Butiku na hata Msekwa bila Kuwasahau wengine wachache kama Mimi pia Mzee Mtarajiwa GENTAMYCINE.
 
Warioba hajawahi kuwa think tank ya Nyerere..

Nyerere alikasirishwa mno na serikali ya Mwinyi ambayo Warioba alikuwa Waziri mkuu
Kwa kuwa legevu kwenye rushwa...

Kibaya zaidi Warioba aliona jinsi Nyerere alivyo zima kabisa hoja ya serikali tatu
Wakati wa G 55 na ikawa taboo kabisa ndani
Ya CCM kuleta hoja za serikali tatu..
Kwa ukaidi wake Warioba akaenda kuweka hoja za serikali tatu kama kipaumbele cha Kwanza kwenye katiba..ikapelekea katiba yake kupigwa chini..

Warioba hajawahi kuwa part of the solution popote pale..
Only part of the problem
 
Mijadala imerudi sio kama kipindi kile cha yule kamanda wa sungusungu kutoka chato
 
Yale maoni ya wananchi ilitakiwa yeye na baadhi ya taasisi waende Serengeti/ngorongoro wakajifungie waje nakatiba yakupiga kura.
Huu uhuni wa bunge la mivutano hatutapata katiba inayokidhi Taifa.
 
Warioba hajawahi kuwa think tank ya Nyerere..

Nyerere alikasirishwa mno na serikali ya Mwinyi ambayo Warioba alikuwa Waziri mkuu
Kwa kuwa legevu kwenye rushwa...

Kibaya zaidi Warioba aliona jinsi Nyerere alivyo zima kabisa hoja ya serikali tatu
Wakati wa G 55 na ikawa taboo kabisa ndani
Ya CCM kuleta hoja za serikali tatu..
Kwa ukaidi wake Warioba akaenda kuweka hoja za serikali tatu kama kipaumbele cha Kwanza kwenye katiba..ikapelekea katiba yake kupigwa chini..

Warioba hajawahi kuwa part of the solution popote pale..
Only part of the problem
Nyerere siyo nabii, mawazo yake yasiyofaa yanapingwa na kubadilishwa tu bila wasiwasi wowote. Mfano mmojawapo ni tulivyozima na kufutilia mbali azimio la kimasikini la arusha
 
Na sheria wanazobadili wahuni hawa ni zile ambazo wanufaika ni wao na si Watanzania. Zile ambazo wanufaika ni Watanzania hawataki hata kusizikia.

Nimependa pale Warioba anaposema; "hawataki Katiba Mpya lakini kila siku wanafanyia marekebisho sheria zilizopo", akiwa anamaanisha Katiba iliyopo imepitwa na wakati.
 
Na hapo ndiyo najua patamuumiza sana Mama wa Kizanzibari Mkuu kwani ni kama vile Mzee Jaji wa Watu 'Kamkaanga' Kiaina.
 
Nimebahatika Kusikilizishwa 'Kiduchu' aliyoyasema ( kwani ni Kipindi kilichorekodiwa ) na kitaruka leo Jumatatu Saa 3 Kamili Usiku na kwa nilivyomsikia ni wazi Mzee Warioba kuhusiana na Suala la Katiba mpya ni kama vile kaamua 'Kujilipua' na kwamba kama noma na iwe noma tu.

Tafadhali natoa Angalizo mapema tu kuwa Mzee wa Watu kwa yale mtakayoyasikia juu ya shauku yake pia kutaka Katiba Mpya siyo muanze 'Kumchukia' na kuona si mwana CCM au hampendi 'Mama' bali Maoni yake yaheshimiwe mno.

Nawapenda sana Wazee wasiokuwa Wanafiki, Waoga na siyo Watu wa Kujipendekeza na kuwa 'Chawa' kwa Viongozi ( Watawala ) kama akina Mzee Warioba, Butiku na hata Msekwa bila Kuwasahau wengine wachache kama Mimi pia Mzee Mtarajiwa GENTAMYCINE.
Utolewa na mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Warioba hajawahi kuwa think tank ya Nyerere..

Nyerere alikasirishwa mno na serikali ya Mwinyi ambayo Warioba alikuwa Waziri mkuu
Kwa kuwa legevu kwenye rushwa...

Kibaya zaidi Warioba aliona jinsi Nyerere alivyo zima kabisa hoja ya serikali tatu
Wakati wa G 55 na ikawa taboo kabisa ndani
Ya CCM kuleta hoja za serikali tatu..
Kwa ukaidi wake Warioba akaenda kuweka hoja za serikali tatu kama kipaumbele cha Kwanza kwenye katiba..ikapelekea katiba yake kupigwa chini..

Warioba hajawahi kuwa part of the solution popote pale..
Only part of the problem
Warioba amejipambanua kuwa yeye ni free person kwa kuekeza kile anachoona kinafaa kwa taifa .
Akiwa kama Msomi ,mwanasheria bobezi na Muandishi wa Katiba Ya wananchi ya 2013 ,ameweza kubeba ajenda ya Watanzania walio wengi kwa uadilifu.
Inaonesha wewe Ni Mpinzani wa katiba ya wananchi.Bali unaunga mkono ile ya Chenge -Pendelkezwa
 
Na sheria wanazobadili wahuni hawa ni zile ambazo wanufaika ni wao na si Watanzania. Zile ambazo wanufaika ni Watanzania hawataki hata kusizikia.
Hili suala bila wananchi kuwa serious tutaendelea kuchezewa sana, wanafanya hivyo sababu bunge wameliteka wao.
 
Na hapo ndiyo najua patamuumiza sana Mama wa Kizanzibari Mkuu kwani ni kama vile Mzee Jaji wa Watu 'Kamkaanga' Kiaina.
Mama "asijishtukie" mbona hiyo imekuwa ni tabia ya viongozi wote wa CCM walioko madarakani.
 
Warioba amejipambanua kuwa yeye ni free person kwa kuekeza kile anachoona kinafaa kwa taifa .
Akiwa kama Msomi ,mwanasheria bobezi na Muandishi wa Katiba Ya wananchi ya 2013 ,ameweza kubeba ajenda ya Watanzania walio wengi kwa uadilifu.
Inaonesha wewe Ni Mpinzani wa katiba ya wananchi.Bali unaunga mkono ile ya Chenge -Pendelkezwa
Ile rasimu yake ya Katiba ilikuwa first class, no one can dispute that labda awe mlevi wa madaraka.
 
Back
Top Bottom