Mmoja wa polisi waliouwa afikishwa mahakamani leo

ngonani

JF-Expert Member
Aug 27, 2012
1,366
596
Habri niliyoipata hivi punde nikiwa mjini Iringa ni kuwa askari mmoja kati ya sita waliokamatwa amefikishwa mahakamani,ni yule aliyefyatua bomu.Wengine watano ambao nao walimpa kipondo marehemu wameachiwa.

Hii inatokana na maombi ya mtuhumiwa mwenyewe kuwa yeye ndiye aliyeua na wengine waachiwe.Kutokana na ombi ilo alipelekwa kwa mlinzi wa amani Ijumaa na confession yake kuchukuliwa na mlinzi wa amani.Leo hii kapelekwa mahakamani.

Wadau tisijadili ili suala kwani tayari liko mahakamani, lakini naona haki haijatendeka inabidi na hao watano na RPC wao nao washitakiwe.
 
Kamuhanda yupo wapi? Na iweje apelekwe mahakamani kabla TUME YA NCHIMBI HAIJATOA MAJIBU? Polisi Wamekurupuka!
 
Habri niliyoipata hivi
punde nikiwa mjini Iringa ni kuwa askari mmoja kati ya sita waliokamatwa
amefikishwa mahakamani,ni yule aliyefyatua bomu.Wengine watano ambao
nao walimpa kipondo marehemu wameachiwa.Hii inatokana na maombi ya
mtuhumiwa mwenyewe kuwa yeye ndiye aliyeua na wengine waachiwe.Kutokana
na ombi ilo alipelekwa kwa mlinzi wa amani Ijumaa na confession yake
kuchukuliwa na mlinzi wa amani.Leo hii kapelekwa mahakamani.Wadau
tisujadili ili suala kwani tayari liko mahakamani,lakini naona haki
haijatendeka inabidi na hao watano na RPC wao nao washitakiwe.

sasa mbona wewe umejadili?
 
Bomu moja lilipuliwe na watu wangapi?
Hlf yeye ataiamriaje mahakama? Kwamba hawa wengine waachiwe na mahakama ikubali maombi yake??????? Wale wote walishiriki sasa walitaka
 
Haiwezekani, huu ni uonezi, wanaotakiwa mahakamani ni polisi wote waliokuwepo eneo la tukio ama kwa kesi ya kujeruhi ama kusababisha mauaji ama kuua, hakuna hata mmja anayetakiwa kuachwa hapo. Lazima tupige kelele kwa hili, kuanzia rpc mbaka yule mkuu wa upelelezi wafikishwe mahakamani, nasisitiza hatakiwi kuachwa hata polisi mmoja kila mmoja ana kesi ya kujibu hapo
 
Habri niliyoipata hivi punde nikiwa mjini Iringa ni kuwa askari mmoja kati ya sita waliokamatwa amefikishwa mahakamani,ni yule aliyefyatua bomu.Wengine watano ambao nao walimpa kipondo marehemu wameachiwa.Hii inatokana na maombi ya mtuhumiwa mwenyewe kuwa yeye ndiye aliyeua na wengine waachiwe.Kutokana na ombi ilo alipelekwa kwa mlinzi wa amani Ijumaa na confession yake kuchukuliwa na mlinzi wa amani.Leo hii kapelekwa mahakamani.Wadau tisujadili ili suala kwani tayari liko mahakamani,lakini naona haki haijatendeka inabidi na hao watano na RPC wao nao washitakiwe.

Hivi huyo Mlinzi wa Amani ndo nani?????/
 
ijazie nyama hii habari: kafikishwa mahakama ipi? ya mwanzo ,ya hakimu mkazi au kuu?
 
Alyaua ni mmoja tu ambaye alifyatua hilo bomu na wengine wote walikuwa mashuhuda.
 
Kama ilivyokuwa kwenye kesi ya Zombe ndio iwe kwa kesi ya hawa polisi wa Iringa (nazungumzia utaratibu uliotumika) tofauti ni maamuzi ya mahakama tu (wasiachwe huru kama kina zombe kwani ushahidi upo wa kutosha). POLISI WOTE WANAKESI YA KUJIBU HAO!
 
In police force, Things works in orders, so the Command in charge is responsible who was at the scene!! so where is He? That is Kamuhanda!! Hii itakuwa Danganya toto!!
 
Kwa Kiingereza anaitwa justice of peace,ni hakimu wa primary court au mtendaji kata etc.Kisheria anaruhusiwa kuchukua confession ambayo uwa tendered mahakamani kama kielelezo.
 
Jeshi makini safi sana big up wenye viherehere tu ndo tutawaona wakiendelea kupiga domo
 
Hivi huyo Mlinzi wa Amani ndo nani?????/

MLINZI WA AMANI NDIO NANI? Anatokea JESHI GANI? Maana sisiem wanae kada mmoja anajiita MWANAHARAKATI WA AMANI, JE WANAMAHUSIANO YOYOTE NA HUYU MLINZI? It sound like twins!
 
Polisi kama ilivyo majeshi mengine ya ulinzi na usalama hufanya kazi kwa kutekeleza amri za senior kijeshi, Tumeambiwa kuwa kamuhanda aliwaamuru polisi kutokukurupuka, wasubiri ORDER kwa utekelezaji, ukweli huu una maanisha kuwa wameandaa gape la mtuhumiwa kushinda kesi kwa maelezo kuwa alipewa amri na comander ku-pull triger wakati barrel imempoint "mateka"

wakati hukumu hii inasomwa, kamuhanda atakuwa amesha staafu, amepewa mafao yake yote. na maneno aliyoyasema yatakuwa kweli kwamba hataki kuvuruga pensheni yake, lazima atekeleze maagizo ya. . . . . .
 
Ndio tatizo la polisi kuwa waendesha mashitaka, wapelezi na watuhumiwa

Kwa nini tusiwe na DISTRICT ATTORNEYS AMBAO NI LAW ENFORCERS ktk system yetu? D.A wa Nchi kama USA wanafanya kazi ya DETECTIONS SIO HAWA WETU WANALALA MAHAKAMANI WANASUBIRI POLISI WAHARIBU KESI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom