barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Majuma kadhaa yaliyopita,mwananzengo mwenzetu humu jukwaani madam Rihana alileta kisa chake na jamaa zake kuvamiwa na majambazi huko Tegeta Machakani kwenye grocery moja walipokuwa wanapata moja moto na moja baridi.
Tulivyovamiwa na majambazi eneo la Tegeta Machakani
Kwa habari zile za madam Rihana anasema mmoja wa waliokuwa naye alipigwa risasi moja ya paja.Ilikuwa ni jambo la huzuni kwa bwana Dula aliyeleta "kaubishi" kidogo.
Habari nzuri ni kuwa leo mmoja wa majambazi wale wamekamatwa na kuuwawa.Taarifa nilizozisikia kupitia Kamanda Sirro ni kuwa hao majambazi walikamatwa na kutakiwa kwenda kuonyesha sehemu walipoficha silaha yao,walipowapeleka polisi eneo walipofukia,wakati polisi wakifukua na kuikaribia silaha,jambazi mmoja akaanza kukimbia ili atoroke.
Polisi walipiga risasi za juu ili kumpa tahadhari asimame,hakutii agizo,na baadae polisi wakampiga risasi ya "paja",na jambazi huyo alikufa "wakati akipelekwa hospital".
Hizi habari ziliambatana na taarifa ya polisi kumkamata mwanamke mmoja aliyekuwa anatengeneza kadi bandia za homa ya manjano kwa ajili ya watu wanaosafiri nje ya nchi.
Habari za majambazi hayo ndugu yetu Rihana anaweza kuja hapa na kututhibitishia.Hongera kwa jeshi la Polisi,inawezekana waliitilia mkazo habari ile ya uvamizi baada ya kuiona hapa Jf.
Get Well Soon kaka Dula...Njugu ya paja si kitoto.