Mmoja auawa, mwingine anusurika kwa tuhuma za kuiba baiskeli mkoani moro

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Kijana aliyenusurika akiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa wananchi. ...Kijana huyo akiwa mikononi mwa wananchi.Vijana hao wawili waliosadikiwa kuwa vibaka wakiwa kwenye gari la polisi.Pikipiki inayodaiwa kuibiwa na vijana hao.

KIJANA mmoja ameuawa wakati mwenzake anayesadikiwa kuwa ni Ustadh kwa mavazi aliyokuwa amevaa, akinusurika kuuawa baada ya kutuhumiwa kuiba baiskeli eneo ya Kihonda mkoani Morogoro jana jioni. Kwa mujibu wa jeshi la Polisi, mtuhumiwa huyo aliye hai amelazwa katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa kwa matibabu.

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    35.1 KB · Views: 61
  • 2.jpg
    2.jpg
    45 KB · Views: 65
you may have the guts to condemn mob justice kama hujawahi kulizwa na wezi,but once you have fallen to be their victim, your anger towards them will be unmeasurably great!
 
na MAFISADI tungekuwa tunawapa kichapo hivi, lazima nchi ingenyooka
 
you may have the guts to condemn mob justice kama hujawahi kulizwa na wezi,but once you have fallen to be their victim, your anger towards them will be unmeasurably great!
Na haya unaweza kuyasema kama hujawahi kusingiziwa/kuzushiwa kuiba!

Yaliwahi kunitokea mahali fulani kuna mtu kwa kukosa umakini alinizushia kumwibia simu yake....kwa bahati simu ilipopigwa ikaita ikiwa mifukoni mwake! Kwa mazingira yaliyokuwepo, ilikuwa ni haki kwa mwenye simu kudhania mimi ndiye niliyeiiba lakini kiukweli simu haikuibiwa.

Lilikuwa funzo kubwa sana kwangu katika utoaji wa haki na hasa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa.
 
you may have the guts to
condemn mob justice kama hujawahi kulizwa na wezi,but once you have
fallen to be their victim, your anger towards them will be unmeasurably
great!

Tatizo linakuja pale mtu anapoitiwa mwizi kwa sababu tu eti kalamba mke wa mtu! je haki!? tuache jazba jamani!
 
Mmmh baiskeli inatoa mtu roho, tena labda chakavu....shida mbaya, si bora arudi kijijini kulima?

CCm na serikali yake imetufikisha hapa ambapo sasa binadamu bei yake ni sawa na baiskeli chakavu!! Nchi ingekuwa na uchumi wa uhakika watu wangepata ajira na wasingeshawishika kuiba/face mob justice!!
 
Na haya unaweza kuyasema kama hujawahi kusingiziwa/kuzushiwa kuiba!

Yaliwahi kunitokea mahali fulani kuna mtu kwa kukosa umakini alinizushia kumwibia simu yake....kwa bahati simu ilipopigwa ikaita ikiwa mifukoni mwake! Kwa mazingira yaliyokuwepo, ilikuwa ni haki kwa mwenye simu kudhania mimi ndiye niliyeiiba lakini kiukweli simu haikuibiwa.

Lilikuwa funzo kubwa sana kwangu katika utoaji wa haki na hasa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa.

Mkuu pole sana kwa kunusurika na hicho kitu sio cha kuombea hata kidogo m2 ahisi umemuibia mbele ya umati wa watu au in any public.

Pia naomba nikufahamishe hakuna mtu fundi wa kujitetea na kuprove hajaiba kama Kibaka. Yani ukimpa nafasi ya kujitetea umeumia mkuu.
 
Asante mkuu. Tatizo hata kumjua (kwa uhakika) kuwa huyu ni kibaka/mwizi au la si rahisi mara zote. So katika hao wawili wanatuhumiwa kuiba baiskeli unaweza kukuta pengine ni mmoja tu ndio amehusika, huyo mwingine labda wala alikuwa hajui kinachoendelea!

Washambuliaji wengine wanafuata mkumbo tu, wala hawaulizi! Sasa katika huo mfano wangu ilikuwa ni bahati ilitokea katika mazingira ambayo nafahamika vizuri so haikuwa shida sana (inagwa nilikuwa embarrassed sana!).

Kwa vyovyote vile, hili la kuchukua sheria mikononi (hasa kama adhabu inayotolewa ni kifo), ni suala la hatari sana na kuna wengi wanauwawa kwa style hiyo bila ya hatia yoyote kabisa.
 
Ya kiukweli hii kitu ni hatari sana. Halafu huwa kuna hii trick ya wezi kukimbia huku wakisema mwizi unajikuta na wewe unakimbia na kusema mwizi wakati humuoni huku ukimfata jamaa. Kwa vyovyote vile ni rahisi watu kukushuku ww pia ni mwizi coz utakuta sehemu uko peke yako aliyekua akisema mwizi humuoni lazima watu wakushambulie wewe.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom