Mmoja anusurika kuuawa na polisi kwenye msafara wa Mh. Mohamed Bilal mkoani Mbeya

Sikwepeshi

Senior Member
Jan 26, 2012
162
18
Ni habari ya kuhuzunisha iliyotaka kutokea mkoani mbeya nusu saa iliyopita.kulikuwa na msafara wa mh Bilali uliokuwa unatokea tunduma kuja mbeya mjini,wakati askari wamesafisha barabara tayari maeneo ya kadege gari dogo ilikuwa inatokea maeneo ya Beaco Resort inaingia barabaran kuelekea upande wa iyunga bila kujua nini kinaendelea,gafla likapita gari lingine la polisi waliokuwa kwenye msafara na kupiga risasi kuelekea kwenye lile gari bila kujua kuwa yule mtu ni adui au la,pongez zangu ziende kwa trafic aliyekuwepo pale baada ya kujitoa muhanga wa kumuokoa yule mtu pale alipoenda kusimama mbele ya gari ya msafara na kuonesha ishara ya kuwazuia kuendelea kufyatua risasi japokuwa baadae aliondoka na yule mtu kuelekea central police station.
Ombi langu naomba wale usalama wa taifa na viongoz watakaosoma thread hii waboreshe jinsi ya kuiendesha misafara mikoani ili isihatarishe maisha ya raia wema
pili wapunguze idadi ya magari ya misafara maana nilichokishuhudia mbeya leo ni aibu magari zaid ya 70 kwenye msafara tena yanapita kwa inteval ya dk nyingi hivyo kuwapotezea wananchi muda wa kuendelea na shughuli zao.
TENGENEZENI MAZINGIRA YA WANANCHI KUWALINDA SIO KUWAPIGA MAWE
 
kuna raia aliingiza ng'ombe kwenye msafara wa rais alipata kipigo na kufa siku kadhaa baadae.very sad story lakini inaonyesha ni jinsi gani vyombo vyetu vya usalama vilivyokosa weledi.
 
kuna raia aliingiza ng'ombe kwenye msafara wa rais alipata kipigo na kufa siku kadhaa baadae.very sad story lakini inaonyesha ni jinsi gani vyombo vyetu vya usalama vilivyokosa weledi.

dah jamani,hadi wa ng'ombe inteligencia yao ikashindwa kuonesha kuwa yuko decent,dah Mungu amrehemu.
 
Ndio maana wengine mungu aliamua kuwapenda zaidi kwenye msafara wa jamaha huyu huyu kule Tanga
 
Back
Top Bottom