Ushauri: Mama mdogo anamsema vibaya mchumba wangu kumbe anajihusisha naye kimapenzi!

huyo mama mdogo hana adabu yaani amemwona huyo mchumba wako tu??heb achana na huyo mwanaume kwani km ameweza fanya huo ushenzi wake mkiwa hamjaoana ujue ukikubali mkaoana atahama ht nyumba...
 
heee,pole mamii,kitendo anachokifanya mamaako mdogo ni kichafu,na huyo mchumba ako hajatulia,na hana aibu,juu ya yote,uamuzi ni wako,maana ndoa ni safari ndefu,ukiwa nae huyo mtu ujue pressure zitakuwa juu juu,maana hatotulia,ata hangaika tu.pengine ni heri yako,mungu amekuonyesha mapeema huyo mchumba ni wa aina gani.jee umemwambia maako mdogo?na yeye anasemaje?.w.me sijui wakoje jamani,wewe ndio wenye uamuzi wa mwisho.muulize mchumba kulikoni na kwa nini anafanya hivyo?inavyoonyesha hakupendi,asingekufanyia hivyo.
Zingatia ushauri huu kwani ndio unaokujenga vizuri kimaisha
 
Mweleze mamdogo ucimfiche anachofanya c kizuri kabsaa!

Na huyo mchumba mueleze ajue kosa lake then chukua hatua
Huu pia ni ushauri mzuri sana kwako, waeleze wote wawili kila mmoja kwa wakati wake kisha achana na mchumba wako huyo kwani atakuja kukusaliti hata utakapokuwa kwenye ndoa. Kama ameweza kutembea na mama yako ambaye wewe mwenyewe ulimtambulisha, itakuwaje kwa wanawake wengine ambao huna undugu nao?
 
Hana akili timamu asituchefue hapa, michelle unatisha umemkumbuka huyu

sisahau vitu vya wiki iliyopita....especially vile amavyo ni strange kwa jamii yetu....kama kutafuta mume wa mkataba....:A S 13:
 
mwache, tena mwache haraka, kwasababu hapo mmeshafanya laana, wewe na mama yako mdogo mmeingiliwa na mwanaume mmoja, yaani u.boo. ulioingia kwako ndo uouo unaingia kwa mama yako mdogo..sasa hapo amekula kuku na mayai na vifaranga.....uchafu huo..kimbia..hata ukiolewa, utakuwa unajua moyoni kuwa unaishi na mtu ambaye alishawai kulala na mama yako mdogo, haitakuja itoke maishani mwako...pia, kama uyo jamaa hata kwenye ndoa hajaingia anakula hadi wakwe, akiingia itabidi umweke na mama yako mzazi na bibi yako mbali naye, anaweza kuwa baba yako huyo...kwenye send off tu na ndoa anafanya hivyo, kwenye ndoa je, na utakuwa umeshapiga pingu za maisha, hadi kufa kama wewe ni mkristo, utaishi na donda ndugu maisha yote....pole.
 
huu sasa umekuau ukumbi wa stori za kutunga. Nami nna yangu. Jana nimeota nimelala na mlinzi mmoja wa gadafi, alikuja kujificha tz baada ya kukimbia libya. Je nimwambie waifu, au ataona wivu? Nishaurini[ Bora ww unashaurika!
 
Hivi ni wewe au nimesahau kuwa wiki iliyopita ulikuwa hapa unatafuta mpenzi wa muda( wa mkataba)? leo huyu unaye miaka miwili?

ulikuwa unatafuta mwingine wa nini?

michelle una memory,naikumbuka hiyo issue ila nilikuwa sijui kama ni huyu.sasa sijui niamini kipi,kama hii story ni ya kweli au si ya kweli
 
Asanteni sana wandugu kwa ushauri wenu mzuri ingawa wengine wananiponda, kuni2kana, na kuninyima raha. Niwaambie2 kwamba binadamu 2natofautiana "kilam2 anastaili yake ya maisha" there is someone's who can eat rice, beans, meat, chapati, vegetable and others at the same tym
 
Asanteni sana wandugu kwa ushauri wenu mzuri ingawa wengine wananiponda, kuni2kana, na kuninyima raha. Niwaambie2 kwamba binadamu 2natofautiana "kilam2 anastaili yake ya maisha" there is someone's who can eat rice, beans, meat, chapati, vegetable and others at the same tym

hongera sana,una uwezo wa kipekee sana mdogo wangu. kila la kheri!!
 
Wandugu naomba msaada. Mimi nina mchumba wangu 2ko ktk process za harusi. alishanitambulisha kwao na nikakubalika. Mimi ninaishi na mamdogo. Mamdogo ndiye aliyenilea so nikama mamangu. SO Nilimpeleka Mchumba wangu kwanza kwa mamdogo kumtambulisha kabila ya ha2a nyingine na mamdogo ndiye aliyewaambia ndugu zangu wengine. na akasema kuwa atagharamia kichen party na send off kwa kuwa mimi nikama mtoto wake. ndugu zangu karibu wote wanamjua huyo kijana.sasa cha ajabu mamdogo ameanza kunikatisha tamaa. ananiambia mbona huyo mwenzako anaoneka haja2lia? Nimzuri 2 wasura hana kingine hakufai mwanangu. Tafuta mwingine mbona wanaume wako wengi? na maneno mengine mengine kibao. Mimi nikamjibu nampenda hivyo hivyo alivyo mamdogo.baada ya kuona sielekei kumwacha akaanza kumwaga upupu kwa ndugu zangu wote kwamba yule kaka hanifai. Ndugu zangu wakaanza kumchukia huyu kijana. Cha kushangaza naona mamdogo yuko karibu sana na mchumba wangu nikimuuliza anasema wanashughulikia mambo ya ndoa ye2. Siku moja mawifi zangu (ukweni) wakaniita na kuniuliza hivi huyo ni mamdogo wako kabisa? Nikawajibu ndio. yeye na mamangu ni wa2mbo moja walishangaa na kusema mbona sasa anafanya mambo ya ajabu vile? Nikawauliza mambo gani hayo wakasema nisubiri niolewe kwanza ndo wataniambia coz wanaogopa kuuvunja uhusiano we2. (mimi na kaka yao) katika chunguza yangu nimegundua mamdogo ananichukulia mchumba wangu. Nimuachie mchumba wangu au Nifanyeje??
wewe ni muongo au unatunga story ,we si tarehe 26 mwezi wa pili ulipost thread inasema nahitaji mpenzi?
 
Asanteni sana wandugu kwa ushauri wenu mzuri ingawa wengine wananiponda, kuni2kana, na kuninyima raha. Niwaambie2 kwamba binadamu 2natofautiana "kilam2 anastaili yake ya maisha" there is someone's who can eat rice, beans, meat, chapati, vegetable and others at the same tym

Sasa kwanini unaleta michezo humu jukwaani? Au ulikuwa unapima watu kama wanakumbukumbu humu ndani? Na ulisahau kuwa humu kuna akina Michelle wenye kumbukumbu zao nzuri tu. Kuwa serious basi young lady!
 
Asanteni sana wandugu kwa ushauri wenu mzuri ingawa wengine wananiponda, kuni2kana, na kuninyima raha. Niwaambie2 kwamba binadamu 2natofautiana "kilam2 anastaili yake ya maisha" there is someone's who can eat rice, beans, meat, chapati, vegetable and others at the same tym

Weka kumbukumbu vizuri mie nahisi wewe unacheza na akili za watu tu haya kila la heri
 
Hebu tujikumbushe ID zake zote

N4G,
Boflo,
notenough,
.............
.............
 
Back
Top Bottom