Mmmh!!!....hivi hii kweli ndio sababu ya mtoto kunyonya kidole???

Ha ha ha mi nilidhan cause ni kukosa malezi ya kutosha ya mama yao kila mmoja hakupata muda wa kutosha kuenjoy maziwa ya mama so wali2mia kusuck vidole vyao kama nyonyo mbadala

Kweli angesema ivo ingekuwa na mantiki
 
Wanajf habari zenu!! Brothers wangu watatu wana watoto wasiopishana sana kiumri,yaani kama miaka 5,miaka 4 na mwingine miaka 3. Hawa watoto wote wananyonya vidole. Mwanzoni mwa huu mwezi wameletwa home likizo baada ya kufunga chekechea zao. Juzi kati kuna rafiki yangu alikuja home akawaona wakinyonya vidole,akaniambia eti sababu ya watoto hao kunyonya vidole ni kwamba mama zao walinyonywa sehemu za siri kwenye tendo lililosababisha mimba za hao watoto. WanaJF,kuna ukweli wowote hapo? Wajuzi tiririkeni

Hapo nilipobold, haya ni maneno ya mitaani na hayana ukweli wowote ...
Kitaalamu, watoto wengi wanaozaliwa huwa wana natural urge to suck. Kwa baadhi ya watoto, hali hii huanza kupungua baada ya miezi 6. Wengine huenda mpaka miaka 5, na cha kushangaza kuna watu wengine huendelea na hii tabia mpaka ukubwani!!!

Hali ya kunyonya vidole kwa watoto hutokea na kugeuka kuwa ni tabia ambayo huwafanya wajifariji na kujisikia vyema hususani wanapojisikia njaa, hasira, hofu, woga, utulivu, usingizi au kuchoka.

Hakuna uhusiano wowote kati ya ulichokieleza na matatizo ya watoto kunyonya vidole. Ila kuendelea kwa watoto kunyonya vidole kunaweza kuwa na madhara ya kimwili kidogo na kisaikolojia. Ni vyema kuwaona madaktari wa watoto kwa ushauri zaidi badala ya kuamini maneno maneno ya mitaani!!!
 
Back
Top Bottom